Kuchukiwa pasipo sababu...

Hakuna kitu kama hicho! Mtu anayesema anachukiwa bila sababu jaribu kumchunguza yeye ama wanaomchukia.........lazima kuna sababu tu!!!


Kwa hiyo kumbe si kweli ile dhana ya mtu kusema watu wananichukia bila sababu.
 



Da umesema kweli kabisa,haiingii akilini,na wakati mwingine muhusika unakuta anaamini au sijui niseme anajiaminisha kwamba watu wote ndio wenye matatizo,labda wanamuonea uwivu katika jambo fulani na badala ya kujaribu kurekebisha anaendelea na tabia yake ileile ya kuumiza wenzake.
 
LABDA NIANZE KWA KUSEMA USILOLIJUA NI KAMA USIKU WA GIZA
AWALI YA YOTE NI KWAMBA MM NILIKUWA NA DADA YANGU ILA SASA AMESHAPONA MUATHIRIKA WA ISHU HII NA KWA MDA MREFU NIMEKUWA NIKIJARIBU KUFWATILIA KWA NINI , MWISHOWE NIKAGUNDUA HAYA YAFUATAYO,


1~Kama unaamini kuwa watu wote hatufanani basi jua kwamba wapo wenye bahati ya kupendwa/kukubalika na kila mtu bila sababu na wapo wa kukataliwa/kuchukiwa na kila mtu bila sababu na hiyo ndo inaitwa damu ya kunguni. Ukiachilia mbali hiyo wapo watu wengi ambao unakuta baadhi ya watu wanakukubali an baadhi wanakukataa hivyo inakuwa 50-50 na hiyo haina haina shida.

2~Kama huamini juu ya hili ni-contant kwa PM nikuingize shule ya Philosophy juu ya SPIRITY of REJECTION kwa binadamu, mpaka wanyama.


KIUKWELI ANAYEPINGA JUU YA HILI NI KWAMBA BADO NI MCHANGA KIFIKRA ILA UKIKUTA MTU ALIYECHIMBA VITABU NA ALIYESOMA PHILOSOPHY OF ANIMALS ATAKWAMBIA, NA NDIO MANA WAPO ALBINOZ KWA KILA KIUMBE NA MIMEA.
 

"negative vibe about them regardless".
Ina maana hii inaweza ikatokea tu?
 
wapo sana yani kila sehemu yenye mkusanyiko i mean skul,mkutanoni,au popote pale panapokusanya watu lazima mmoja aonekane ana damu ya kunguni ...............yani inatokea watu hawakupendi hata ukichangia kitu wanacheka tu ........ukifurai wanacheka ukicheka wananuna
ila mchungaji wangu alisema kuna roho ya kukataliwa tu bila sababu na kuchukiwa so unaposali basi zikemee zote izo kila siku mana njiani huko maroho mengi huwez jua umelikwaa lipi ulipokua unakatisha mitaa yenu huko.........ni vizur tu hata kama hujalikwaa au umelikwaa kusali usiku na kuyakemea mabaya yote b4 u sleep
 
Kwa hiyo kumbe si kweli ile dhana ya mtu kusema watu wananichukia bila sababu.

Mabaya yake au mazuri yake, yote yaweza kuwa sababu ya mtu kuchukiwa! So, siamini kabisa katika mtu kuchukiwa bila sababu yeyote!!!
 
 
Mie naamini IPO
unakuta mtu hana ubaya kiasi hicho lakini kila mtu hampendi.

Sababu halisi zinapopelekea kuchukiwa bila sababu bado sijazielewa vizuri sana ila mojawapo ni hii

1. Kukataliwa kwa mtoto nz mzazi.
Kuna baadhi ya wazazi wanawakataa watoto wao kuanzia mimba hadi wanazaliwa. Kama mzazi tu anamkataa mtoto basi mtu huyo anakuwa anazongwa na roho ya kukataliwa popote aendako.

Kwa upande mwingine mtu anapokua akijua alikataliwa na mzazi wake ni kama inaleta psychological effect ambapo mtu anajiona hana thamani mbele za watu. Hii inaweza kumfanya awe mtu wa kujishuku kwa hiyo watu wanaomzunguka wanakuwa hawavutiwi naye ukilinganisha na wengine.
 

Kuna ile dhambi ya kukataliwa
 
Hivi unachukia tabia za mtu kutokana na kukosana naye au hata usipokosana naye bado utachukia tabia zake?
Bila kumchukia mtu mwenyewe naweza sana kuchukia tabia yake, hata bila kukosana.
Ila nadhani NN kajibu vizuri hapo (about projection). Na the more anaamini ana damu mbaya, the more anajichukua, na the more ana perceive hivo. makes sense...
 
Love yourself first before you start seeking other people to love or like u.... If u hate ur own self who on earth would like u anyway!!?
 
Anaechukiwa ndio anaeweza kuona hamna sababu, ila anaechukia anakua na sababu hata kama ni ya kijinga. Inaweza kua muonekano wako, tembea yako, ongea yako, fikra zako, matendo yako, vaa yako, ishi yako,attitude yako kwa ujumla n.k
Hii haina tofauti na watu ambao wanapendwa kirahisi, yani sio lazima amfanyie mtu kitu kizuri ndio apendwe, hata attitude,tabasamu lake tu linatosha kufanya watu wampende/vutiwe nae kirahisi.

Muhimu ni wewe kutotilia maanani watu ambao wanaonyesha chuki dhidi yako wakati hujafanya chochote kuwakosea.
 
Hivi kwa nini mtu anapendwa na wengine? Kwa sababu ni "mwenzetu" "anafanana nasi" si kwa sura bali kwa tabia, mitazamo, na fikra. Anajichanganya nasi, na kwa hiyo siyo tishio kwetu. Huyu tutampenda. Kinachofanya mtu achukiwe ni ile hali ya kuwa tofauti sana na wengine kiasi kwamba wanakuona hufit kwao, huko sehemu ya kundi lao kwa namna yako ya kufikiri, kutazama mambo na kutenda. Wengine watakuona kiumbe cha ajabu tu na hivyo kuanza kukutenga na kundi "lao" kwani wewe hufit hapo. Kwa kuwa uko tofauti sana nao wanaweza kukuweka au kwenye kundi la wa watu wa "juu" sana au kutegemea na wanavyokuona au kukuweka kundi la "chini" sana. Wakikuweka kundi la juu sana wataku-label kama mtu mwenye majivuno, majidai, kujiona sana, mtu wa matawi ya juu. Watakuchukia, utaonekana mtu wa damu ya kunguni usibadilika. Wakikuweka katika kundi la chini wataku-label kama mtu mshamba sana, mtu wakuja, mtu usiyeenda na wakati. Kwa hiyo huingii ktk kundi lao. Watakutenga na kukuchukia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…