Kucheza kwa mtoto tumboni....

loupa

Senior Member
Jul 22, 2016
124
78
Wadau mtoto anaanza kucheza tumboni kuanzia mda gani? Maana mke wangu ana ujauzito wa miezi karibia sita na hakuna dalili za kurusha mateke tumboni . au kuna tatizo mwenye ujuzi tafadhari
 
Wadau mtoto anaanza kucheza tumboni kuanzia mda gani? Maana mke wangu ana ujauzito wa miezi karibia sita na hakuna dalili za kurusha mateke tumboni . au kuna tatizo mwenye ujuzi tafadhari
Nenda watampiga utrasound na watapata majibu
 
Ni kuanzia miezi mitano/sita, na kama ukiwa na wasiwasi basi ni vizuri kumuona daktari kwani kwa kipindi hiki matatizo ni mengi
 
Naomba niwarekebishe kidogo tu wachangiaji waliotangulia, lugha sahihi kutumika kwenye uzazi ni wiki na sio miezi kwa sababu wa wiki 20 atasema miezi mitano na wa wiki 23 atasema miezi mitano wakati kuna mabadiliko makubwa hapo katikati.
Mtoto kucheza inatofautiana kutokana na mimba kama ni ya kwanza kwa mama au amewahi kubeba mimba hapo kabla.
-Kwa mimba ya kwanza ni wiki ya 18 mpaka 20

-Kwa mimba ya pili na kuendelea ni wiki ya 16 mpaka 18
 
Ni wiki 22 for sure regardless ni mimba ya ngapi labda kama umekosea tarehe. Na kwa wakati huu unatakiwa uwe umefanya ultrasound ya kwanza.
 
Back
Top Bottom