Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Nimependa maelezo yako na inaonekana unauzoefu au ujuzi wa jambo hili,Naomba niwarekebishe kidogo tu wachangiaji waliotangulia, lugha sahihi kutumika kwenye uzazi ni wiki na sio miezi kwa sababu wa wiki 20 atasema miezi mitano na wa wiki 23 atasema miezi mitano wakati kuna mabadiliko makubwa hapo katikati.
Mtoto kucheza inatofautiana kutokana na mimba kama ni ya kwanza kwa mama au amewahi kubeba mimba hapo kabla.
-Kwa mimba ya kwanza ni wiki ya 18 mpaka 20
-Kwa mimba ya pili na kuendelea ni wiki ya 16 mpaka 18
Naomba nami kuuliza : vipi kuhusu mtoto kuchezea sana eneo la chini ya kitovu mara nyingi kuliko upande mwingine, kuna tatizo lolote!?
Na vipi kwa mama anayelala chali japo kwa saa moja kwa siku, anaweza kusababisha madhara yoyote!?