Kuchapwa viboko wanafunzi wakuchoma mabweni wa mali za shule hakutoshi tuwe na sheria ya KUNYONGA watakaobainika.

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,732
7,611
Nimpe pongezi kidogo Mkuu wa mkoa wa Mbeya.

Adhabu ile haitoshi (angechapa viboko 100) uharibifu ni mkubwa, mno kuchoma mabweni na uharibifu mkubwa wa mali wa namna ile haivumiliki.

Hizi ni kodi za walalahoi Zinazojenga na kuweka Samani Mashuleni.

Ikitokea wapuuzi 2 wavutaji bangi wahamasishe uharibifu wa mali zilizowekwa kwa mamilioni ya pesa yafaa WANYONGWE kwa maana wakiachwa ni tatizo kwa jamii hao ndio wezi na majambazi tusilee ugonjwa ni heri wafe tutatue tatizo (PANAPO FUKA MOSHI ZIMA MOTO CHINI)

Kama taifa tufike wakati tusiendekeze ujinga wa namna hii tukiacha haya matatizo kila sehemu yatakua hatutakuwa na suluhisho maana yatakuwa yameota mizizi ambayo kuikata ni vigumu.

SULUHISHO:
Tuwe na sheria kali ya KUNYONGA kwa wote watakaohusika hata kama ni shule nzima ili mradi imethibitika wamehusika.

Haya ni maoni binafsi lakini ni kwa msitakabali wa maendeleo ya taifa letu kutokuruhusu ujinga ujinga unaoweza kuleta hasara zinazo gharimu Taifa.
 
Ukiwa na hasira sana au furaha ya ajabu usiponyeze alama ya kujumlisha na kuanza kubwabwaja hisia zako.

We tangu lini mtu akanyongwa kiss kachoma shule?

Na aliyeua tumfanyeje?

Aliyebaka je?
 
Duuh kweli?
Ebu fikiria mwanao akawa miongoni mwa watakaobainika halafu hiyo sheria ikawa imepitishwa utakuwa katika hali gani? Wewe fikiria tu.

Kunyonga mwanafunzi sio suluhisho la kudumu na lenye uwiano sawa ingawa umesema ni maoni binafsi
 
Nimempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kuwatandika viboko wanafunzi, haiwezekani tunajenga shule halafu Watoto wanaenda kuchoma, nimemuambia fukuza wote kwahiyo Form 5 na 6 wote wamefukuzwa na Bodi imevunjwa, eti Haki za Binadamu!, Haki za Binadamu watoto wawe na viburi vya kipumbavu!?, hao wa Haki za Binadamu wakayejenge basi hayo mabweni" - Ameyasema Hayo Raisi Magufuli....
 
Nyinyi mbona mmeifisadi hii nchi tangu 1961 mpaka leo, na bado mnatembea barabarani na minguo yenu ya kijani huku mkiwa hamna hata chembe ya aibu?

Si mnastahili kabisa adhabu ya kunyongwa! Majambazi wakubwa nyinyi.
 
Alichapa viboko baada ya watoto kukutwa na simu na si kuchoma bweni watu wanachanganya Sana hii taarifa
 
Wahujumu uchumi ambao wengine wamesabisha hasara ya mabilioni ya shilingi, fedha ambazo huenda zingetosha jenga mabweni ya mkoa mzima hawanyongwi lakini waliochoma madarasa katika shule moja tu wao wanastahili kunyongwa ati?
 
Back
Top Bottom