Kuchangia harusi kukomeshwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuchangia harusi kukomeshwe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ramos, Jun 19, 2010.

 1. R

  Ramos JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nasikitika kwanza kuwa pendekezo hili naliweka katika maneno ambayo hayajadailutiwa hata kidogo. Kwa maoni yangu, umefika wakati sasa wa kusema no kwa michango ya harusi, ama fedha au mda. Maoni yangu yanazingatia kuwa kwanza kuoana ni uamuzia na muhimu kwa wanaooana. Yapo mambo mengi yenye faida ambayo tunaweza kuchangiana kama vile ada za watoto mashuleni, kuhudumuia wagonjwa na kadhalika. Kama anadhani anataka kufanya harusi, basi aandae kwa fedha zake na awaalike watu waje wamuunge mkono kusheherekea, sio kuwakalisha watu kwa zaidi ya masaa 400 (e.g vikao 5 x masaa mawili kila kikao x wanakamati 20) eti wakiumiza vichwa na hela ili mtu aoe!
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Wabongo tunavyopenda kujionyesha nani katoa mchango mkubwa kwenye harusi ya fulani na kutaka harusi za kifahari na gharama kubwa sijui kama hili litawezekana lakini nakuunga mkono kabisa katika pendekezo lako. Ukiwaambia watu wachangie elimu au kufanya usafi katika maeneo yao wanayoishi ambayo yamekithiri kwa uchafu hupati mtu lakini tangaza mchango wa harusi au kipaimara hapo utaona mashindano ya nani kachangia pesa nyingi.
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Nakuunga mkono kwa silimia 100 kuhusu suala hili. Harusi zinaongoza kwa michango, na mara nyingi michango hiyo huishia kwenye mambo ya kula na kunywa tu mpaka mamilioni yote yaishe. Ingekuwa pengine nusu ya michango hiyo wanapewa wanandoa wapya waanzie maisha ingekuwa ni jambo la busara. Lakini unakuta sehemu nyingi (walau hapa ninapoishi) pesa karibu zote: ni KULA na KUNYWA. Hakuna zaidi! Tunahitaji kubadilika, na kuwa na vipaumbele katika kuchangia maendeleo: elimu, afya, nk. Ni uhakika michango ya harusi ingeelekezwa katika shughuli za maendeleo kungekuwa na mabadiliko makubwa katika jamii yetu.
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Hii ni moja ya industry inayofanya vizuri sana bongo. Kuna wapambaji, photoshops na wapiga picha za video na zile za kawaida, kuna matarumbeta, ukumbi nyingi za kufanyia sherehe etc. Ukiangalia sana sometimes hizi harusi zetu tuna overdo bila sababu za msingi. Kuna haja gani y kufanya harusi ya milion zaidi ya kumi wakati maharusi hawana hata pa kuanzia!! Kama nia ni kuwasaidia, huo uwe mtaji basi badala ya kuuangamiza wote kwa siku moja.
  Kwahili mimi nakuunga mkono mtoa hoja....harusi tunazofanya zimepitwa na wakati. Tuanze kuchangia mkono mambo kama elimu,ugonjwa etc kuliko kupoteza fedha nyingi kwenye harusi ambazo nyingine huwa zinaishia njiani pasipo kujari gharama zilizotumika kuzikamilisha.
   
 5. doup

  doup JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  tatizo wabongo usipo wapa maakuri na ze laga utasikia watakavyo ponda, heti bora hata nisingekuja. nimeshuudia harusi nyingi tu na kuwa mwanakamati; kuna moja ya harusi bwana harusi alikaataa ze laga; wadau walilalamika sa mwisho wa siku walikuja na za kwao.

  na inavyo elekeawatu wengi hutimia harusi kama sehemu ya mtoko wao; kwa mantiki hiyo kama alitakiwa awe rose garden siku hiyo hakita haribika kitu, kwani masanga atayapa tu harusini.
   
 6. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kwani mwenzetu ulishaoa nini? kama teyari inabidi uwalipe waliokuchangia tusikomeshe kuanzia hapo.
   
 7. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkuu hili bonge la point nilianzishaga thread kama hii hapa jamvini nikaishia kuambulia matusi na kejeli inaonekana watu wanapenda sana sifa za ku pledge na kulilia michango na kuchukia wale wasio kuwa na uwezo wa kuchangia maharusi.
   
 8. C

  Cool Member

  #8
  Jun 21, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kweli kabisa. Hii michanog ya harusi kwa sasa imekuwa ni kero. Hebu fikiria kwa mwaka unachangia harusi jumla sh ngapi. Katika michango yako jumlisha zawadi na hela ya mafuta au nauli ya TAX ya kuhudhuria harusi maana huwa zinafanyika usiku.

  Baada ya hapo fikiria iwapo una wazazi wako kule kijijini je, kwa mwaka unawasaidia kasi gani cha fedha? Au msikitini au kanisani unamtolea Mungu wako kiasi gani?
   
 9. P

  Paul S.S Verified User

  #9
  Jun 21, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu point ipo sana katika topic yako ila sasa utekelezaji, unajua haya mambo nimambo tunazaliw tunayakuta yanakaa vichwani kiasi tunaamini hizi ndio taratibu husika za maisha, kubadilisha fikra zetu ghafla inakuwa ngumu.
  toka enzi na enzi shughuli kama harusi, misiba, jando, arobaini nk, zinahesabika ni shughuli za kijamii watu hushiriki kwa kushirikiana na baadhi ya sehemu hupima ushiriki wako ktk jamii kwa mambo haya na kama ushiriki unatengwa na jamii husika.
  Wakati mambo ya maana kama masomo, matibabu, nk yanachukuliwa ni mambo ya kibinafsi. Kunawakati nilimsikia Padri Karugendo anasema watu hawataki kuchangia mambo ambayo hawata faidi direct kama masomo. wanachangia harusi wanajua watakunywa na kula ingawa ni kwa masaa machache, lakini masomo wanachojua wakiuchangia mafanikio yatakuwa yako na ndugu zako,
  Kiukweli huwezi kukomesha hapa swala ni kujaribu kuanzisha utaratibu wa kuchangiana kwa shughuli zingine
   
 10. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,778
  Likes Received: 20,713
  Trophy Points: 280
  kwa upande mwingine,kuna ubaya gani familia/ukoo ukiamua kumfanyia harusi kubwa kijana wao??harusi ni moja ya hatua kubwa za maisha ya binadamu,it is your big day and u would like to make it as great as it can be.
  kiuchumi vilevile zinatoa ajira na kipato kwa watu wengi tu,zingatia hao watu waliojiajiri kama wedding planners,kuna watu wana magari special for weddings,kumbi nyingi tu za harusi,catering industry.
  kuchangia harusi si jambo baya ila wengine ndio wanaweka utaratibu mbaya mpaka inakuwa kama LAZIMA mtu achangie kiasi kikubwa wakati ilitakiwa iwe hiyari.
   
 11. C

  Cool Member

  #11
  Jun 21, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15

  Kama ni hoja ya hatua kubwa ya maisha kwa mtu, si ufanye wenyewe? Kwanini kuwalazimisha watu kukuchangia kwa lazima. Sasa hivi hadi kipaimara na wengine hata graduation wanalazimisha kuchangiwa. Tena siyo hiari, ni kana kwamba ni lazima. Unakuta mtu kwenye kikao anaambiwa atoe ahadi, halafu akisema 20000 wote wanakamati wanapiga kelele ati hapa kima cha chini ni 70000, Wanajua mshahara wangu hawa? Au wanafahamu mahitaji yangu?
   
 12. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Tooo late to rewind the trend
   
 13. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145

  Mkuu umesahau kuwagharamia ndugu(wa manati) wa maharusi kuja, kuhudhuria sherehe na kurudi walikotoka na na hao waitwao wamekujua kuwa wewe ndugu yao ukubwani na una maisha yako..... FUTILIA MBALI Michango... !! muhimu harusi yenye mapenzi ya dhati!:A S 103:
   
 14. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145


  Mkuu.. Ni kiasi cha wenye harusi kuwa na msimamo na uthubutu!! INAWEZEKANA kubadilisha mfumo huu!!
   
 15. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,415
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  haya mambo yapo na tumeyakuta toka kwa mababu zetu, tazama hata vijijini ikitokea harusi inakuwa na issue ya kijiji kizima huyu analeta mpunga huyu pombe ili mradi mwisho wa siku mambo yaende sawa pia na kwenye misiba na sherehe nyingine (ingawa siku hizi yanafanyika kisasa zaidi) issue kama ya elimu ni ngumu kuchangisha watu kwa kuwa return yake ni ya muda mrefu sana na pia inaweza isiwafikie waliochanga ingawa siku hizi kuna baadhi ya koo au familia wanaanzisha fund kabisa ya kuchangiana kwa issue kama elimu na maradhi ila haifikii extent ya kuchangisha jamii nzima. Nadhani watu wengi wanachangia harusi kwa kuwa nao wanapata kuburudika kutoka kwenye michango yao

  Halafu kibongo bongo hakuna sehemu inayoburudisha watu wengi kwa ujumla kama harusi especially kwa wanandoa ambao kwenda viwanja kama Bills ni adimu kidogo kwa hiyo halafu ni kama out flani hivi
   
 16. 2c2

  2c2 Member

  #16
  Jun 21, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sjaoa na natarajia kuoa kwa harusi,,,,,,,,, lakini swala la kusitisha kuchangiana michango ya harusi naliunga mkono asilimia 200%,,,,, inashangaza sana mtoto anafukuzwa shule kwa kukosa ada ya sh 10,000 alaf m2 anachangia harusi 200,000......
  Ilinishangaza zaidi bwana arusi hana hata senti tano anataka harusi ya milioni 7 mchango wake 0 na pesa za mavazi pia anachangiwa, huu si ulimbukeni,,,,,,, we have tu end this bussiness as soon as possible,,,,,,,,,,even if is for the government to put his hand on this
   
 17. P

  Paul S.S Verified User

  #17
  Jun 21, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  mkuu umeowa/olewa wewe?. I wish unge kuwa bado halafu ikifika uwe wakwanza kudhubutu
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  harusi michango unaambiwa hasa na kiwango kadhaa!

  kwa upande wangu naona ni aibu tu.................sitamchangisha mtu na wala sitamchangia mtu harusi kamwe
   
 19. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,778
  Likes Received: 20,713
  Trophy Points: 280
  soma vizuri post yangu....nimemalizia kwa kusema''kuchangia harusi si jambo baya ila wengine wanaweka utaratibu mbaya mpaka inakuwa LAZIMA mtu achangie kiasi kikubwa wakati ilitakiwa iwe hiyari.
   
 20. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mimi ambacho sielewi ni mtu kuchangishiwa na kufanyiwa sherehe ya bei ghari lakini kesho mtu ana amka na mkewe kwenye hali halisi ya maisha yao. Nadhani sasa michango imekua njia ya watu kuishi japo kwa siku moja katika maisha wanayo tamani badala ya kufanya kazi na kuishi maisha hayo kila siku.
   
Loading...