Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
- Thread starter
- #21
"don't let them foool ya' or even try to school ya' "
SOURCE: marehem BOBU MALE.
sijui ni wawapi huyu Marangu au Mkibosho? LOL
"don't let them foool ya' or even try to school ya' "
SOURCE: marehem BOBU MALE.
........ jamani hivi elimu mliyosoma madarasani ikowapi? hiyo sh 500 mnunulie mtoto wako daftari atakusaidia baadae.
Ujumbe wangu unakuhusu na wewe unayetumia internet, hata mimi nimesoma chini ya mti si lazima wa kijijini hata hivyo sizungumzii kura nazungumzia sms kwa vile asilimia kubwa ya simu ziko mjini vijijini hakuna network.Sidhani wengi wa waliosoma madarasani watachangia; hawa wengi wao ndio ambao hawajajiandikisha kupiga kura na kwa wale waliojiandikisha, huwa hawaendi kupiga kura.
Wengi wa watakao/wanaochangia ni wale waliosoma chini ya mti; huu ushauri wako hawatausoma kwani wengi wao hawatumii intanet, kama wanajua kutumia computer.
Nini kifanyike, civic education. Nani afanye, mimi na wewe. Lini, wakati ni huu. Wapi, huko vijijini.
sijui ni wawapi huyu Marangu au Mkibosho? LOL
I HATE CCM!
...and politics...
Bora wachangishane wenyewe wasiguse hela zetu za kodi au BoT.
Mi naona sawa tu maana hiki ni chama na wenye mapenzi nacho wachangie kama tunavyochangia harusi na misiba ya ndugu zetu. Cha msingi wasilete vifyatavyo;
1. Wasianzishe EPA mpya kwa ajili ya uchaguzi.
2. Wasilazimishe watu kwenye mashirika ya umma na vijijini kuchangia kwa lazima
3. Wasichote hela serikalini au hazina
4. Wasitumie magari au vyombo vingine vya Serikali kufanyia kampeni au kutumia muda wao kazini kufanya hivo badala ya ujenzi wa taifa
5. Waweke wazi at least kwa wanachama wao kiasi cha pesa walichopata na matumizi yake
Je vyama vingine navyo viseme wapi vinategemea kupata hela zao za kampeni ni vema vyote viwe wazi. Hii ni hatua nzuri kwa CCM tofauti na uchaguzi uliopita ambapo hawakusema walitoa wapi hela na baadae nyingine kupotea BoT (EPA???)
View attachment 9465
Siyo swali gumu na wala siyo swali la mtego hata kidogo Jibu lake ni rahisi kweli kwani halihitaji uwe msomi wa elimu ya anga za mbali au uliyebobea katika sayansi ya Fizikia ya Nyota kuweza kutoa jibu lake. Ni swali ambalo kila mwana CCM anatakiwa awe na jibu lake na kila Mtanzania kuamua vile vile kulijibu.
Mwishoni mwa juma Rais Kikwete alizindua utaratibu wa kuchangia Chama cha Mapinduzi ili kiweze kushiriki vizuri uchaguzi mkuu na kushinda ili iweze kuongoza taifa letu kwa miaka mingine mitano. Katika uzinduzi huo lengo lao ni kuweza kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 40 ili kuweza kutimiza malengo mbalimbali ambayo yatafanikisha lengo hilo la kufanya vizuri kwenye Uchaguzi. Fedha hizi zikishakusanywa zitatumika:
- Kununua magari 60 kwa ajili ya kampeni
- Kununua pikipiki 170
- Baskeli 23,000
- Kukodi helikopta na ndege
- Matumizi mbalimbali ya makabrasha ya kampeni na uchaguzi
Ili kuweza kuchangia kwa njia ya simu mwana CCM au Mtanzania anayekiunga mkono Chama cha Mapinduzi anatakiwa atume neno "CCM" kwenda Namba 15377 ambapo atakuwa amechangia Shs 300, akituma neno "CCM" kwenda 15388 atakuwa amechangia Shs 500 na akituma neno "CCM" kwenda 15399 atakuwa amechangia Shs. 1000. Ni wazi kuwa CCM itatumia mbinu nyingine mbalimbali kuweza kufikia lengo hilo. Sasa tunajua ni kiasi gani kinahitajika, kitatumika vipi, na namna gani kuweza kuchangia. Baada ya kuyajua hayo hatuna budi kujiuliza kama tuchangie au tusichangie.
Kabla ya kuchangia jiulize!
Kwa vile najua watu wengi ambao ni mashabiki wa CCM watakuwa tayari kuchangia kwa sababu "Rais kasema" na kwa sababu wanataka chama chao kiendelee kutawala na wapo wengine ambao hawataki kusaidia upinzani ukomae na hivyo wako tayari kuunga mkono CCM basi nimeona ni vyema kujitolea kuwasaidia watu hawa ambao wana fedha na vitu mbalimbali ambavyo wako tayari kuviweka kwenye miguu ya CCM kujiuliza maswali kadhaa ambayo wakijibu ndiyo kwa yote mawili inawapasa watoe michango yao.