Kuchangia au kutokuchangia? Hilo ndilo swali..

Hii ni silaha nyingine wamewapa vyama vya USHINDANI.
Kama nilivyosema kwenye post ya "nini kifanyike;;;" wanatakiwa wakaitumie kwenye kampeni zao kuwaeleza wananchi kuwa CCM vipaumbele vyake ni maslahi ya chama na sio wananchi. Kama wanaweza kuhamasisha uchangishaji wa pesa zote hizo kwa ajili ya chama chao, kwanini wasichangishe kwa ajili ya maendeleo ya wananchi???


Moringe wote ni Wamasai lakini sio kila Mmasai ni Moringe
 
e mungu nashukuru kwa kunipa akili kidogo

ila kwa uelewa wangu hata kwa bunduki sichangii si heri hii pesa nikatoe sadaka kuliko kuichangia CCM jamani ningekuwa sifanyi kazi serikalini au kweny haya mashirika yao ningeshika bago wajue msimamo wangu tatizo wametubana kweli wakikufahamu tu utaona memo zina kuja kasi kweli .


we have to do something to stop this kwanza wamenitumia sms kuniomba mchango ingekuwaa kunasehemu ya kujibu ningejibu jibu baya sana
 
Hapa ndio pale elimu ya uraia na wapiga kura ya kweli inapohitajika. Maskini wadanganyika bila kujua kwanini wanachangia, watachangia kwa nguvu zote. Halafu zile watakazochangia zitarudi kwa wachache wao wenye kelele kwa njia ya Kofia, na T-shirt bila kugundua hawajakamilishiwa cha kuvaa chini na hivyo wapo utupu! Na watajisifu kwamba wamekula pilau za bure na hivyo wapo radhi kuwapa kura. Mwaka mmoja baadae watalia kilio cha mbwa mdomo juu maisha magumu!

Tanzania...Tanzania...kwa nini wanakufanya hivi?
 
.

we have to do something to stop this kwanza wamenitumia sms kuniomba mchango ingekuwaa kunasehemu ya kujibu ningejibu jibu baya sana

Loh! Nashukuru nimeona hayo usemayo maana ningepata sms yao bila kujua wengine pia wanapata ningeitupa simu yangu kwa kuona imenisaliti!
 
Back
Top Bottom