Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 973
Tangu skendo kubwa kubwa za rushwa zianze kujitokeza nchini, hasa katika kipindi cha Utawala wa Awamu ya Nne, ambazo zilipekekea kujiuzulu kwa Viongozi wengi wa Serikali kusnzia Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wanasheria wa Serikali, mpaka wenyeviti wa Kamati za Bunge. Hata hivyo, mara zote tuhuma hizo zimeonyesha kuwa, hazina umuhimu mkubwa kwa Watanzania linapokuja suala la maadili. Baadhi ya Viongozi waliotumbuliwa, walipokelewa kishujaa majimboni kwao na kuua ile dhana ya awali kuwa, hawakuwa na maadili. Kwa wananchi wao huko majimboni kwao, hawakuona kama maadili ni kitu muhimu kwao, kulinganisha na utumishi wa wawakilishi wao hao. Wapiga kura hao wameonyesha kujali zaidi uwezo wa wawakilishi wao kwao na si maadili ya kitaifa:
Hayo yote ni tisa na cha mtoto tu. Kinachostaajabisha tabia ya Watanzania, ni namna ambavyo Wabunge na Madiwani waliojiuzulu na kuhamia CCM kutoka CHADEMA, walifanikiwa kurejesha nafasi zao tena ikionekana kwa urahisi zaidi kuliko walivyozipata nafasi hizo mwaka 2015. Katika jumla ya Kata zipatazo 188, ni mbili pekee zilizoenda CHADEMA huku nyingine zote zikichukuliwa na CCM. Katika Majimbo nane, yote yamerudi CCM.
CCM ya Magufuli ime-revolutionize Siasa za Tanzania completely.
Nini kinachowafanya wananchi wawakubali tu kirahisi rahisi hivyo? Je hiyo haituonyeshi kuwa, somewhere something is still not yet right? Je, si kweli kuwa wananchi hawajali sana masuala ya kisiasa ya Vyama bali wanajali wagombea? Kama ni hivyo, mbona CCM inaendelea kushindwa kwa urahisi licha ya mara kadhaa Upinzani kuonekana kuwa na wagombea vijana na ambao mara nyingi wako smart upstairs kuliko wa CCM?
- Edward Lowassa alipokelewa kishujaa kwao Monduli alipojiuzulu uwaziri mkuu Februari 2008.
- Andrew Chenge alipokelewa kishujaa kwao Bariadi alipojiuzulu uwaziri wa miundombinu April 2008.
- William Ngeleja alipokelewa kishujaa kwao Sengerema baada ya kujiuzulu uwaziri wa nishati na madini mwaka 2012.
- Nape Nnauye alipokelewa kishujaa jimboni kwake Mtama hadi kupanda migongo ya akina mama baada ya kuondolewa uwaziri wa Habari mwaka 2017.
- Mwigulu Nchemba alipokelewa kishujaa huko kwao Iramba mwaka huu 2018.