Kubezwa kwa haki na uhuru hugharimu taifa

Kubezwa kwa haki na uhuru hugharimu taifa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,058
Mabibi na mabwana heshima kwenu.

Umoja na utaifa ni tunu zitokanazo na kuzingatiwa kwa haki na uhuru wa watu. Hizi huakisiwa kimatokeo na hali ya amani na utilivu katika nchi husika.

Kutatizwa kwa umoja na utaifa ndicho adui akihitajicho kupenyeza chochote dhidi yetu.

Halahala na uchaguzi huu na kabla hatujakwenda mbali zaidi. Angalia kinachomkuta Zuchu au kilichowakuta Stars jana. Ni wazi kabisa kuwa umoja na utaifa wetu unapita majaribuni.

Siyo siri Zuchu alistahili kura zaidi kama ambavyo stars walivyostahili uungwaji zaidi mkono, japo hata kwa pole tu.

Chonde wa ndugu brake brake kidogo.

Kweli hatuna cha kujifunza na hata kurekebisha ili kila mtu aweze kuona kuwa ni sehemu ya nchi hii?

Tumefika mbali "eeh mola wetu" ukatujalie tusifike mwisho.
 
Back
Top Bottom