Ningekuwa mimi ni POLISI,ningeangalia hili jambo kwa jicho la pili.Yani Ninge-suspect maadui zaidi kuliko tunaowahisi.Kwa mtazamo wangu,mimi nahisi kuwa kubenea ana maadui wengi.Sasa kuna mmoja sasa anajifanya ni rafiki yake au ni adui wa chini chini.Baada ya kubenea kupatwa na dhahama ile ya mwanzo sasa yeye huyo adui wa siri anataka kutumia hiyo nafasi ili jamii iseme kuwa labda aliyepiga hiyo simu ya vitisho ni huyu adui tunae mfikiria.
Tutake tusitake,huyo mpiga simu lazima anapitia hapa JF kusoma news.Huyo wa mwanzo aliyemwagia tindikali nae nahisi anapitia hapa JF kusoma news na ktk hali ya Ujambazi wa kawaida LAZIMA anaogopa ama anahisi kuwa jamii tayari inamjua,so hawezi tena kuendelea kupiga simu za vitiso.
Ila kama ni jambazi aliyekubuhu basi huyo mmwaga tindikali ndo mpiga simu,kitu ambacho sitarajii sana kwa ujasiri wa waTZ.Namshauri kubenea kukaa chini na kuanza kuorodhesha ANAO WAHISI NI MAADUI ama wana TOFAUTI zozote.Namba moja awe ni yule anaemhisi kwa asilimia ndogo zaidi na wa mwisho Awe adui wake wa wazi ambae kila mtu anamjua na ambae obvious hawezi kumpigia simu ya vitisho.
Tatizo la Polisi wetu wa bongo ni blah blah nyingi.Yani utafikiri walinzi wa sungusungu vile.Wao kukurupuka tu.Ukitaka kuamini wewe fuatilia wanavyomhoji mtu kukiwa na tukio serious.
Yani wako shallow kweli.
© Ningesema siwapendi ilaisemi tena
Hiyo ndiyo hasara ya kutotoa kipaumbele ktk masuala ya usalama, hao polisi ni form four au six failures. Wanaofanya vizuri darasani hawaajiriwi polisi. Hili ni tatizo la kimfumo. Nchi zingine km vile US, UK wale New scotland yard ni wale walikuwa vichwa darasani. Lazima Serikali ibadili mfumo huu, ili kuwashawishi watu wenye upeo mkubwa kujiunga polisi.
Niliwahi kuanguka somo zito na mnenene mmoja mambo ya ndani ni Commissioner wa Polisi alikuwa ni mtupu hadi anaongea kisukuma mie nikanawa na kuondoka.Uelewa wao ni mdogo sana sijui vipi hawa watu .
I call upon the gvt kuprovide uyu ndugu yetu na kaulizi,ivi polisi kazi yao si ni kulinda usalama wa Raia,sasa kama mtu anapigwa bit huoni kuwa anastaili kulindwa.
Polisi wanaweza ku trace kirahisi sana mtu aliyempigia simu Kubenea kama wakiamua. Makampuni yote ya simu yana rekodi kila simu inayopigwa na kupokelewa.
Hata kama mtu akiweka "private" kwenye simu yake, bado ukienda kwa kampuni ya mtandao anaotumia Kubenea wanaweza ku - print namba za simu zote alizopigiwa na wakajua ni namba ipi ilimpigia muda huo. Hata kama aliyepiga simu alitupa "chip" ya yenye namba hiyo mara tu baada ya kupiga simu, bado anaweza kukamatwa. Kinachoweza kumfanya asikamatwe ni kutupa vyote, handset na chip. Endapo ataweka "chip" nyingine kwenye "handset" ile ile bado anaweza kuwa traced na kukamatwa.
Nampa pole Bw. Kubenea, Muhimu ni kwa vyombo vya usalama kutafuta namna ya kumlinda na kuweka mtego wa kuwakamata hawa jamaa. Ni wazi kwamba wanatumwa kufanya hivyo na Mafisadi.
Kwa TZ yetu kutrace namba ya simu ni ngumu sana, maana Laini za simu zinauzwa kama karanga. mtu ananunua laini anakutishia akimaliza anaitupa.
Polisi wanaweza ku trace kirahisi sana mtu aliyempigia simu Kubenea kama wakiamua. Makampuni yote ya simu yana rekodi kila simu inayopigwa na kupokelewa.
Hata kama mtu akiweka "private" kwenye simu yake, bado ukienda kwa kampuni ya mtandao anaotumia Kubenea wanaweza ku - print namba za simu zote alizopigiwa na wakajua ni namba ipi ilimpigia muda huo. Hata kama aliyepiga simu alitupa "chip" ya yenye namba hiyo mara tu baada ya kupiga simu, bado anaweza kukamatwa. Kinachoweza kumfanya asikamatwe ni kutupa vyote, handset na chip. Endapo ataweka "chip" nyingine kwenye "handset" ile ile bado anaweza kuwa traced na kukamatwa.
Ninachoogopa ni haya mambo ya kuhisi tunaishi kwenye Police State.. inanikumbusha maisha chini ya Hastings Kamuzu Banda... Hivi huku ndiko tunakoelekea?