kiukweli barabara nyingi nchini hasa Dar kwa sasa ni mbovu sana , hasa baada ya hii mvua ilyonyesha hivi karibuni, barabara nafikiri sio jukumu la mbunge kujenga, mbunge kazi yake ni kuhamasisha na kuhakikisha serikali husika inafanyia kazi kero hiyo, ila kitu kingine hawa watu wanaopewa tenda za kukarabati barabara ni majipu, kila mwaka tunafukia mashimo yale yale, na mvua ikinyesha yanarudi tena na inakuwa dili nyingine, wanafanya chini ya kiwango kwa kuhakikisha kazi hizi zinapatikana kila mwaka, huu ni ufujaji wa kodi za wananchi.