Kubenea, njoo uone barabara zako za Sinza

Ryan The King

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
2,788
2,690
Habari wakuu.

Mimi ni mkazi wa Sinza. Nipo kimasomo.

Kwakweli barabara za hapa Sinza zinatia kinyaa. Barabara ni mbovu mno. Si kwa watembea Kwa miguu wala wenye vyombo vya Usafiri.

Mbunge wa Ubungo mhe. kubenea embu kuja huku ujionee raia wanavyopata shida. Kata kama haina serikali bhana.

Taarifa uzipate.

Nawasilisha
 
Kwakweli hili litamgharimu ifikapo 2020

Kabla ya Kubenea alikuwepo Mnyika. Hakuna cha maana alichofanya na watu walilalamika sana humu na kuapa kutomchagua tena. Alichofanya alienda gombea jimbo jingine na kumwachia Kubenea, naye hakuna la maana linaloendelea. Hilo jimbo bila CCM hakuna atakayelirekebisha; kubali au kataa.

Sitaki mapovu mie sio ccm ila najua chadema wamebanwa hapo hawawezi furukuta.
 
Mimi sijui cha CCM au CHADEMA. Mwenye wajibu Kwa Sasa ni Kubenea
 
mabarabara mengi ya DAr mabovu! ya manisaa na serikali INASIKITISHA KUONA WATU WANAKATWA MAKODI MAKUBWA YA BARABARA LAKINI BARABARA MBOVU , kuna barabara ya Bandari pale ni fupiiii lakini MBOVU MBOVU MVOBU! ni ya Mbunge wa CCM je na yeye atakosa kura? hapa ni kulaumu tu serikali kwanini hawatengenezi hizi barabara JE KODI HAZIKUSANYWI?
 
Habari wakuu.

Mimi ni mkazi wa Sinza. Nipo kimasomo.

Kwakweli barabara za hapa Sinza zinatia kinyaa. Barabara ni mbovu mno. Si kwa watembea Kwa miguu wala wenye vyombo vya Usafiri.

Mbunge wa Ubungo mhe. kubenea embu kuja huku ujionee raia wanavyopata shida. Kata kama haina serikali bhana.

Taarifa uzipate.

Nawasilisha
Mimi sioni kama wabunge wanatujali wananchi, sehemu nyingi tuu miundombinu imeharibika lkn hata mbunge kuja kuwafariji tuu raia inakuwa shida? Wananchi tuwe makini sana na wabunge wetu 2020 tusifanye makosa.
 
Kubenea atatoa pesa mfukoni mwake? Walalamikie watu wa Manispaa ambao wanaweza kujenga kwa pesa zitokanazo na makusanyo mbalimbali ndani ya halmashauri husika ama peleka malalamiko yako kwa Dereva wa Lori ambaye kupitia waziri wa ujenzi anaweza kutenga fungu kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo. Kubenea kazi yake ni kuwasemea wananchi wake ukiwemo wewe pale bungeni.
 
Habari wakuu.

Mimi ni mkazi wa Sinza. Nipo kimasomo.

Kwakweli barabara za hapa Sinza zinatia kinyaa. Barabara ni mbovu mno. Si kwa watembea Kwa miguu wala wenye vyombo vya Usafiri.

Mbunge wa Ubungo mhe. kubenea embu kuja huku ujionee raia wanavyopata shida. Kata kama haina serikali bhana.

Taarifa uzipate.

Nawasilisha
Alijiita Kamanda wakati wa kampeni.
Kubenea hajawahi pita Sinza toka kampeni ziishe.
Sijui anatofauti gani na wanaccm anaowapinga.
 
Mimi sijui cha CCM au CHADEMA. Mwenye wajibu Kwa Sasa ni Kubenea

Umejiuliza kwa nini Kubenea ameshindwa kutengeneza hata barabara? Unafikiri haoni/hataki?. Mnyika amekimbia hapo na machachari yake hakufurukuta. Jimbo la ubungo siasa ndio kila kitu, kuna vizee vya ccm hapo mtu wa chama kingine hawezi fanya lolote. Jaribu kuulizia storia ya hapo utaelewa naandika nini
 
Nyie watu, huu ujinga utaisha lini jamani? kwa nini uiangalie barabara mbovu kisha uanze kumlilia Mbunge????? Bajeti ya ujenzi wa barabara siku hizi imehamishiwa kwa wabunge?????
 
Kwakweli hili litamgharimu ifikapo 2020
Barabara katika jiji la Dar kote ni mbovu. Bahati Mbaya wewe umeangalia Sinza pekee. Ungepita na Ilala, Ukonga, Temeke, n.k ungeshangaa zaidi. Lakini ungeenda na Mikoani, Wilaya na Vijijini huko ungetoa machozi!! Let's face it... Tumefikaje hapa? Yaani kuwa na miundombinu dhaifu kiasi hiki miaka zaidi ya 50 ya uhuru???? hilo ndilo swali la kutafakari kwa makini. Akina Kubenea utawalaumu bure...Tuacheni kutafuta majibu mepesi kwa matatizo makubwa.
 
hivi kuna majimbo yaliyochukuliwa na upinzani, kuna huduma yoyote serikali ya magu ilishapeleka, mie naona inaenda kwenye majimbo ya ccm, lakini upinzani hamna, sasa baadae 2020 kwenye kampeni waje wadanganye wananchi kuwa mumemchagua flani wa chama flani, mbona hajafanya lolote, chagueni kijani muone, na kwa hili upinzani wasitegemee support kutoka serikalini, kama wana wadhamini nje wajitahidi tu wawasaidie, ila sasa wakishaleta hao wahisani kama ya pale kwa lema, serikali itaingilia kati itibue kila kitu,
 
Back
Top Bottom