Kubenea na siasa za Kyela

Status
Not open for further replies.
Balantanda.
Utakuwa kama wafuasi wa Kibwetele wa Uganda.Waliomsubiri sana yesu wakiamini atakuja na mwisho wakaamua kujichoma wenyewe.

Hiyo taarifa imepikwa kila sehemu na hana cha kujitetea.
Mwandishi makini ni yule anaye balance uandishi wa habari zake .Mwakalinga tunaye hapa muda wote na ni mmoja kati ya wana jf wa kwanza.Alishindwaje kumuuliza kabla ya kuitoa hewani?..
Mkuu magoli.
Hayo yapo mengi.

1.Kuna mhariri wa gazeti la majira(namba yake ya simu 0784840808). Yeye ni kiboko.Waandishi wa habari wa mikoani, wakimutumia habari ambayo inaeleza madudu ya Mwakyembe,basi ikifika kwake,yeye ataibadili mpaka hakikishe inamsifia mheshimiwa au hiyo taarifa itawekwa kikapuni.
Hao ndiyo waandishi wa kibongo.

2.Mara nyingine ninakumbuka usemi wa mheshimiwa mwenyewe mwakyembe kuwa elimu zao ni ndugu na serikali iwasaidie.
 
Du, mambo yamekuwa mambo.

Kubenea kadanganya na hawezi kuja hapa kusema chochote. Maneno kama tarehe ya Mwakalinga kuwa Kyela na kuwa jamaa ni Mwanafunzi, ni upuuzi wa hali ya juu. Angelisoma hata zile makala za zamani ambazo tuliandika karibu CV nzima ya Mwakalinga, basi angelifahamu nini kiliendelea.

Wapambe wa Mwakalinga wanafahamika na hata yeye huwa anakiri kuwa ANAFAHAMIANA nao na ANAWASILIANA NAO. Sasa hawa wote wanaokuja na kujifanya ni Mwakalinga timu, ni FEKI.

Mwakalinga, tuombe uzima. Mwakani naweza kuwa Kyela kwa ajili ya kampeni ingawa ntakuwa kwenye majukumu mengine. Vinginevyo ntajitahidi hatimaye NIFIKE KYELA kwa mara ya kwanza maana kuna wengine wanadhani mie ni wa KYELA. Huwa nikiwapigia simu au PM ninawapa majina ya watu na miji ya SAIKONG ndiyo wanaamini. Itabidi nifike Kyela ili nivifahamu hivyo vijiji ambavyo huwa navisikia. Hatimaye itakuwa ni sehemu ya kuifahamu nchi yangu Tanzania na hasa Mkoa wa Mbeya maana ulikuwa Mkoa wangu wa kwanza kuishi hapo miaka hiyoo dada yangu akianza kazi Mbeya.

Malafyale itabidi nikifka huko basi lazima nikutafute maana huku kufahamiana kwa kwenye SCREEN inabidi kuishe. Tuombe uzima WATANI wangu WANYAKYUSA.
 
wadau sijajibiwa swali langu, kuna mtu anajua hatima ya waliommwagia tindikali Kubenea? walifungwa? ni vizuri tukajua maana Kubenea yuko mstari wa mbele kufichua mafisadi , Shigongo yeye yuko mstariwa mbele kufichua wazinzi
 
mkuu fmes,

kwanza niombe msamaha maana nilimsahau mdogo wangu steved katika watu waliosaidia kuokoa jahazi kutoka midomoni mwa mamba wakati mimi nilipokuwa likizo huko tanzania.

Sikonge ndio simsemi maana tumetoka mbali wote. Itabidi akishapata uzoefu wa kyela basi 2015 tuwe wote kule sikonge tukimuuza kwa wapiga kura. Tunataka watu ambao unaweza kuwaangalia machoni na ukasema unachoniambia ni sahihi kwa asilimia angalau 99. Tumechoshwa na watu ambao wanadanganya karibu kila kitu.

Nilikuwa naweza kujitokeza moja kwa moja kama mwakalinga lakini nimeamua nitumie majina yote mawili ili mtu aweze kurudi nyuma na kuangalia kama kuna inconsistence yoyote katika hoja zangu tokea enzi za mtanzania kule business times mpaka leo hapa jf.

Wengine wanaotaka kugombea kyela wanakaribishwa mno maana hiyo ndiyo demokrasia ambayo tunaiongelea siku zote; wananchi wapate nafasi ya kuchambua pumba na mchele.

Mwisho, kwa habari nilizo nazo mimi kwa asilimia zaidi ya 99 ni kwamba mwakipesile hagombei ubunge kyela mwakani. Nimeambiwa hata yeye ameshutushwa mno na hizi habari za kubenea. Wacha tumwachie mwakipesile mwenyewe ajibu.

Mimi nimeongelea ya kwangu tu lakini kwa habari ambazo nazijua kuhusu mwakipesile, hunter na mwanjala, hata huko mkuu kubenea ameboronga mengi tu, amewapaka hao wana kyela wengine bila sababu za msingi. Kwa sasa nitaacha kila mtu ajiokoe mwenyewe.

mimi nilikutetea kiasi cha kufungiwa wiki moja hata pole hukunipa.
 
mimi nilikutetea kiasi cha kufungiwa wiki moja hata pole hukunipa.

Pole sana kanda2. Niliowataja ni wale ambao nafahamiana nao kwenye real life na niliongea nao nilipokuwa Tanzania na wakasaidia kufikisha ujumbe wangu JF.

Kuna wengi walinitetea na nawashukuru sana. Ila Kanda2 si ni wewe uliyesema nimeahidi kutoa laptops shule zote Kyela? Sijawahi kusema kitu kama hicho mahali popote au kwa mtu yeyote. Je ulitoa wapi maneno kama hayo? Kama sio wewe basi samahani sana. Kuna watu wengi tu waliamini mimi nimesema kitu kama hicho hasa kwa wale ambao hawanifahamu. Mimi siahidi jambo lolote na kama kuna kitu nataka kutoa basi natoa kwanza kabla ya ya kuwaambia wananchi. Kule vijijini ukiahidi kitu watu wanategemea utekeleze. Mimi sina uwezo wa kutoa laptops kila shule na kama ningesema hivyo ungelikuwa usanii tu ambao mimi mwenyewe naupinga hapa kila siku.

Kuna wakati nilitaka kuomba shirika fulani huku lisaidie vitabu kule Kyela. Wakanipatia forms zao ambazo ilikuwa ziwekwe sahahi na walimu wa shule husika (shule tano). Na kweli kule Kyela walimu wakasaini na kuzirudisha. Bahati mbaya huo msaada wa vitabu ukaunganishwa pamoja na maombi mengine na kukabidhiwa WAMA ambao nao wakavipeleka kule walikotaka wao. Kule Kyela ikawa kasheshe, pamoja na kuwaambia mwanzoni kwamba tunajaribu na chance ya kupata ni kama 10%, wao waliamini hivyo vitabu vimepatikana. Baada ya muda yakaanza maneno ya chini chini kwamba nimewatapeli. Ikabidi nitoe pesa yangu mfukoni na kuwanunulia vitabu hapo Dar. Hapo ndio maneno yakaisha ila nikawa nimejifunza kwamba huko nyumbani watu wanafikiri kila mtu ni mwizi na kwamba kila ukiomba kitu nje utapewa. Usiahidi kitu hata siku moja maana utawapa matumaini watu bure wakati huenda usifanikishe. Fanya kila kitu kimya kimya na kikiwa tayari ndio waambie.

Hata halmashauri ya wilaya walishawahi kusaini barua yetu fulani ya kuomba msaada fulani ambao kwa leo sitautaja. Baada ya muda wakaanza kusema kumbe nao akina Mwakalinga ni wasanii. Barua zote kutoka chombo cha serikali kilichokuwa kinashughulikia usajili wao walikuwa wanapewa copy lakini bado hawakuamini. Siku tumefanikisha, watu waliona aibu kama nini. Mkuu mmoja ndio akasema wazi kwamba hata yeye alishaanza kuamini na sisi ni wasanii lakini sasa tumemuumbua hata yeye na ni jambo zuri kwetu maana wale wote waliokuwa wanasambaza hayo maneno sasa ndio wanaona aibu kubwa.

Ku deal na watu wa wilayani ni ngumu sana, inatakiwa elimu kubwa ili waelewe na waunge mkono juhudi za kusaidiana nao kujiletea maendeleo yao. Hata michango wanayotoa inatakiwa kuwe na uwazi mkubwa mno ili kila mtu aone kila senti imeenda wapi, vinginevyo watalia ufisadi hata pale ambapo hakuna ufisadi.
 
Mwakalinga, tuombe uzima. Mwakani naweza kuwa Kyela kwa ajili ya kampeni ingawa ntakuwa kwenye majukumu mengine. Vinginevyo ntajitahidi hatimaye NIFIKE KYELA kwa mara ya kwanza maana kuna wengine wanadhani mie ni wa KYELA. Huwa nikiwapigia simu au PM ninawapa majina ya watu na miji ya SAIKONG ndiyo wanaamini. Itabidi nifike Kyela ili nivifahamu hivyo vijiji ambavyo huwa navisikia. Hatimaye itakuwa ni sehemu ya kuifahamu nchi yangu Tanzania na hasa Mkoa wa Mbeya maana ulikuwa Mkoa wangu wa kwanza kuishi hapo miaka hiyoo dada yangu akianza kazi Mbeya.
Sikonge,

Watu sio makini tu maana wakisoma jumbe zako watagundua hutaji vijiji vya Kyela na majina unayoyataje ni manne tu ambayo yote umeyasoma hapa hapa JF. Unataja Mwakalinga, Mwakyembe, Mwakipesile na Mwanjala. Wakati ukiandika ya Sikonge unataja watu mbalimbali na pia unataja miji kama inavyotamkwa.

Kwa mfano ukisoma ya Masanilo utajua ni mtu ambaye ana idea na Kyela lakini sio wa Kyela maana huwa anakosea anapoaandika vijiji vya Kyela. Malafyale unajua ni mtu wa Kyela ambaye amekaa nje muda mrefu maana kuna mambo anayoyaandika yamepitwa na wakati. Ukimsoma Engineer unagundua ni mtoto wa kijueni ambaye ana access na power brokers wa siasa za Kyela na anaishi Kyela.

Kuna jamaa zangu walikuwa wanaamini kabisa Sikonge ni mmoja kati ya wadogo zangu wa kuzaliwa. Imechukua muda kuamini Sikonge ni mtu wa Sikonge, Tabora na kuna wengine mpaka leo hawaamini.
 
Mtake au msitake tutampigia Mwakyembe kura na atakuwa mbunge wetu kwa mara nyingine,wana Kyela hatutaki kushinikizwa na mamluki,historia itajirudia na mnaopiga porojo hapa za akina Mwakipesile naona hamuwajui vizuri watu wa Kyela nahisi nyie ni wakuja,mnahadithiwa tu ,mambo ya Kyela hayajadiliwi London au Loliondo
 
Ha ha ha,

Ongezea Monduli (alikopitia Mwakalinga ili kupata baraka za mzee wa monduli) kwenye list hapo juu.
 
Malafyale,
...

Hayo ya tindikali; katika haya mapambano sitaanzisha vita na mtu yeyote, ila kama mtu kaanzisha vita ni ruksa na mimi kujibu. Watu wengine ni wapuuzi na ndio maana wanamwagiwa acid, narudia kwa mara nyingine. Hata USA walitumia nuclear kujibu mashambuliza ya Wajapani na wajomba zao Wajerumani katika vita kuu ya pili.

Naona pesa za Lowassa sasa zinataka kutumika kununua nuclear.

Masikini Kubenea, sijui kama utapona. Fikiria watu kama Mwakalinga ndio wanaitwa kizazi cha kesho cha viongozi Tanzania! wanatishia kumwaga acid na kutumia tindikali?

Kazi kweli kweli
 
Mkuu,

Moja ya watu wapole duniani ni mie. Ila ningelipewa MADARAKA basi usingeliamini kuwa ni huyu Sikonge unamfahamu.

Mie na homeboy Samuel Sitta hatufahamiani. Ila kama ningelimwambia jina la baba yangu mdogo wa Urambo basi KWA VYOVYOTE VILE ANAMFAHAMU. Kwa maana nyingine, jina la familia yetu Sitta alifahamu. Huyu bwana nimekuwa mpinzani wake mkubwa kwa UFISADI wake tangu awe CDA. Ila kama kuna siku alinifurahisha ni siku alimwambia Kikwete "AWE MKALI KIDOGO". Kwa hili brother Sitta ulizoa maksi nyingi sana kwangu.

Wakati mwingine kwa WAPUUZI kama Kubenea, ningelikuwa Rais basi si ACID tu ila ntafanya kibaya zaidi. Kama anaandika ukweli ambao kwa sababu moja au nyingine unaleta hali ya hewa mbaya kisiasa, ninaweza kumwita na kumwambia kwa nini tunaDANGANYA hivi. Ila kama anadanganya na kupotosha habari, basi lazima afahamu kuwa ACID ni cha mtoto.

Kwa upande fulani ni MPENZI wa siasa za KICHINA, hasa ukikumbuka maneno ya Kikwete mwenyewe kuwa 70% ya Watz ni MIFUATA UPEPO. Ina maana kuwa hawa watu inabidi kuwaongoza kama kondoo. Ukitegemea waende wenyewe basi utasubiri sana.

Rais Msanii na mwenye kuchekacheka muda wote hafai kwa nchi masikini. Hebu fikiri watu wanamwambia Rais aende Mtwara kufungua daraja la kwenda Msumbiji (Kubenea type) na akifika hapo anakuta daraja halijaungana. Anaishia kumtuma Mla panya Membe kwenda Msumbiji kwa kimtumbwi eti kwa sababu yeye hafahamu kuogelea. Hawa liomdanganya Rais wanatakiwa wamwagiwe kitu kibaya zaidi ya Acid. Ila kama wewe kiongozi unachekacheka, watakuwekea vidole machoni.

Kama kubenea kashaamua kuwa Mwanasiasa na anacheza Siasa kwenye uandishi wake, hamna tena huruma. Tutamlima kwa kila upuuzi wake na hatapata huruma tena. Kama alimess up na mke wa mtu zamani basi afahamu kuwa kama kama mwanasiasa sasa yeye ni CHAKULA YETU.
 
Naona pesa za Lowassa sasa zinataka kutumika kununua nuclear.

Masikini Kubenea, sijui kama utapona. Fikiria watu kama Mwakalinga ndio wanaitwa kizazi cha kesho cha viongozi Tanzania! wanatishia kumwaga acid na kutumia tindikali?

Kazi kweli kweli

Mijitu mijinga na yenye wivu wa kike utaijua tu. Hata matumizi ya lugha hawaijui. Wapi Mwakalinga ametishia yeye kumwaga acid au kutumia nuclear? Unaweza kusema Mwakalinga amehalalisha kitendo cha waliomwagia tindikali Kubenea lakini hiyo sio sawa na kusema Mwakalinga yeye anatakishia kumwaga acid au kutumia nuclear.

Tatizo la Mitanzania mingine ni ujinga uliojaa kichwani. Ni sawa na wale waliosema Nyerere amewaambia wao ni mbwa baada ya kutumia maneno "I can't allow my country to go to the dogs" akimaanisha Mrema na NCCR mwaka 1995.

Solomon soma kaka, vinginevyo utaishia kuwa mjinga wewe pamoja na mitoto yako. Kama huelewi misemo ni bora uulize!

Utaishia tu na vijembe vya JF vya pesa za Lowassa lakini unafikiri hilo litamnyima hata usingizi Mwakalinga? Kama unafikiri principal Engineer wa makampuni makubwa kama Lucent na Huawei ataenda kumpigia magoti Lowassa, you must be sick! Kweli unahitaji msaada wa kwenda Mirembe.
 
Sasa huko nyuma ulivyokuwa unabwata kwamba George Mwakalinga sio Mtanzania, ulituona sisi wapumbavu? Hatuko hapa kutafuta nani ni nani, but it was tempting to show that relationship, kwa jinsi ulivyoji-expose mwenyewe.

Baada ya ubabaishaji wote huo, unaamini kwamba wewe unaweza kuwa kiongozi wa kuaminiwa? Utakuwa sawa na akina Nchimbi tu.
:D
sijui kwa kiwango gani unamjua nchimbi mpaka kusema kwamba ni kipimo chako cha ubabaishaji kwenye uongozi............amekuwa mwenyekiti wa vijana,dc,mbunge na naibu waziri............kwko umeona ni mbabaishaji sawa lakini anayo ridhaa ya wananchi kuwawakilisha na sasa mmeanza kuandika kuwa ataanguka uchaguzi..............time will tell kwa wewe mwelevu kuongoza walau kata
 
Mtake au msitake tutampigia Mwakyembe kura na atakuwa mbunge wetu kwa mara nyingine,wana Kyela hatutaki kushinikizwa na mamluki,historia itajirudia na mnaopiga porojo hapa za akina Mwakipesile naona hamuwajui vizuri watu wa Kyela nahisi nyie ni wakuja,mnahadithiwa tu ,mambo ya Kyela hayajadiliwi London au Loliondo

Mtampigia wewe na nani? Hata kama ni mwana Kyela basi una kura moja tu. Labda kama ni dikteta na utamfunga mkeo kwa kamba kwenda kumpigisha kura huko Kyela.

Ya nani atashinda hakuna anajejua ispokuwa hapo August 2010.

Unafikiri mtu mwenye uhakika wa kushinda angelikuwa anahangaika kila siku magazetini kulia lia na kupaka wapinzani wake? Mbona hujamsikia hata siku moja prof. Mwandosya akilalamika? Kama Mwakipesile ameachwa ili awaandame Prof na Dr. iweje ni Mwakyembe pekee ndio kila siku kulalamika?

Ukiona mbunge yeyote analaliamika kila siku magazetini, jua kule kwake kuna cha moto.
 
:D
sijui kwa kiwango gani unamjua nchimbi mpaka kusema kwamba ni kipimo chako cha ubabaishaji kwenye uongozi............amekuwa mwenyekiti wa vijana,dc,mbunge na naibu waziri............kwko umeona ni mbabaishaji sawa lakini anayo ridhaa ya wananchi kuwawakilisha na sasa mmeanza kuandika kuwa ataanguka uchaguzi..............time will tell kwa wewe mwelevu kuongoza walau kata

Huyo Invicible kakimbilia hilo jina ili aonekane ni sawa na Invisible wetu, the Robot lakini kichwani yuko upande ule mbali kabisa wa Invisible wa kweli kweli. Yeye anaona kiongozi bora lazima atoke Kilimanjaro au aoe Kilimanjaro. Huyu jamaa ni mkabila mkubwa mno na ndio maana kila siku ni kutetea CHADEMA tu wanapolikoroga. Ni kupoteza muda kubishana naye.

Kama analaumu wenzake kwasababu huko nyuma hawakutumia majina yao, si na yeye aseme jina lake sasa? Mtu anayeendelea kuficha jina lake ana haki gani kumlaumu mtu ambaye huko nyuma alikataa ku confirm kwamba Mtanzania na Mwakalinga ni kitu kimoja?
 
..............Watu wengine ni wapuuzi na ndio maana wanamwagiwa acid, narudia kwa mara nyingine. Hata USA walitumia nuclear kujibu mashambuliza ya Wajapani na wajomba zao Wajerumani katika vita kuu ya pili.

duuhh!!........haya bana.......

check this one

.............ningelipewa MADARAKA basi usingeliamini kuwa ni huyu Sikonge unamfahamu.

.................Wakati mwingine kwa WAPUUZI kama Kubenea, ningelikuwa Rais basi si ACID tu ila ntafanya kibaya zaidi. ........... lazima afahamu kuwa ACID ni cha mtoto...........

................liomdanganya Rais wanatakiwa wamwagiwe kitu kibaya zaidi ya Acid............

........Tutamlima kwa kila upuuzi wake na hatapata huruma tena. Kama alimess up na mke wa mtu zamani basi afahamu kuwa kama kama mwanasiasa sasa yeye ni CHAKULA YETU.

......mmmhh!!......haya bana

halafu......

natamani JF ingekua mahakama..........hah! hah! hah!

...very interesting.....lol
 
Mheshimiwa Mwakyembe, imekuwaje mwaka huu umesusa hata Xmas Kyela?

Kutoonekana kwako kumesababisha gumzo kubwa huku. Kulikoni mheshimiwa?

Nimemwona Mwakipsile leo pale kwake akitanua na wapambe wake.

Mwakalinga vipi mbona tuliambiwa ungelikuwa Kyela wakati wa Xmas?

Hii ya Kubenea naona amefulia big time! kama anavyosema FMES.
 
Ulitaka kuongea nini? Kama wataka kushangaa basi kashangae Bandarini, Shilingi inazama na hili dude linaelea....
url

Mwisho lazima ufahamu kuwa kuna tofauti kati ya RAIS na KIONGOZI WA DINI. Kama unashangaa Mwanajeshi kufundishwa kuuwa basi pole sana.

Kuna MSEMO wa Kichina unasema hivi "Jasho jingi wakati wa mazoezi, damu kidogo wakati wa vita". Dunia hii huwezi kuepuka kumwaga damu, magereza, POLISI, jeshi nk. Vinginevyo wananchi watakudia vidole vya machoni hadi wewe Rais. Ukiamua kuwa mwana Siasa basi lazima ufahamu kuwa siku moja itabidi ufanye uamuzi wa KIKATILI. Ikibidi kuuwa asilimia 10 ili uokoe 90 basi usisite kufanya hivyo. Ndiyo maana unachaguliwa kuwa RAIS na UNAAPA kuilinda KATIBA ya Tanzania. Yes, unaapa KUILINDA KATIBA.

mbona unaji-contradict ndugu yangu?.......halafu unatoa mifano isiyo lingana na hoja at hand...........

yaani wewe umeona kuhalalisha UHALIFU ndio kupigana vita ili kuokoa 90%........ hiyo logic unaitoa wapi?......."Sikonge/Kyela"?...........then hutakuwa tofauti na Kubenea anayeadaiwa kusema uongo ........

.......ni vizuri pia ukaelewa kuwa misingi ya sheria imo kwenye protection zaidi kuliko punishment ............sidhani kama hata Jeshi lenyewe unalijua...........hata jeshini kuna sheria/kanuni/taratibu zake.......

.......Ziko wapi zile kelele zetu hapa JF za kulilia UTAWALA WA SHERIA........halafu bila aibu unadai mtu akipewa uongozi ailinde katiba........give me a break!
 
yaani wewe umeona kuhalalisha UHALIFU ndio kupigana vita ili kuokoa 90%........ hiyo logic unaitoa wapi?......."Sikonge/Kyela"?...........then hutakuwa tofauti na Kubenea anayeadaiwa kusema uongo ........

Ogah,

Unasema Kubenea anadaiwa kusema uwongo? Ina maana wewe baada ya kusoma hapo juu na yote unayoyajua ya mwakalinga hapa JF bado hujaona kwamba amesema uongo?

Kweli mswahili akipenda chongo huita chengeza. Uzuri wa dunia hii, anayechafuliwa leo ni Mwakalinga na kesho utakuwa wewe au mtoto wako. Tatizo la JF ni hilo miaka yote, hoja zinaangalia uso wa mhusika.

Kama kungelikuwa na utawala wa sheria hao waandishi wangeachiwa kuchafua watu kila siku bila kuwajibishwa? Siku hizi usipojilinda mwenyewe na hawa waandishi njaa, hakuna atakayekulinda. Wanachukua pesa zao na kisha wanaandikiwa nini waandike.
 
Mijitu mijinga na yenye wivu wa kike utaijua tu. Hata matumizi ya lugha hawaijui. Wapi Mwakalinga ametishia yeye kumwaga acid au kutumia nuclear? Unaweza kusema Mwakalinga amehalalisha kitendo cha waliomwagia tindikali Kubenea lakini hiyo sio sawa na kusema Mwakalinga yeye anatakishia kumwaga acid au kutumia nuclear.

Waooo,

Timu Mwakalinga kwa lugha za ajabu, utadhani wametumwa na Kingunge au yule mama mwenye matatizo ya akili (Sophia Simba)

Tatizo la Mitanzania mingine ni ujinga uliojaa kichwani. Ni sawa na wale waliosema Nyerere amewaambia wao ni mbwa baada ya kutumia maneno "I can't allow my country to go to the dogs" akimaanisha Mrema na NCCR mwaka 1995.

Bwa ha ha ha

Eti huyu naye anajiona ana akili kuliko watanzania wenzake

Solomon soma kaka, vinginevyo utaishia kuwa mjinga wewe pamoja na mitoto yako. Kama huelewi misemo ni bora uulize!

Eti ananishauri kusoma ...

Bwa ha ha

Utaishia tu na vijembe vya JF vya pesa za Lowassa lakini unafikiri hilo litamnyima hata usingizi Mwakalinga? Kama unafikiri principal Engineer wa makampuni makubwa kama Lucent na Huawei ataenda kumpigia magoti Lowassa, you must be sick! Kweli unahitaji msaada wa kwenda Mirembe.

Bwa ha ha ha,

Eti principal engineer wa Lucient .. so what? Lucient my foot. Yale yale ya kina Balali na Ndulu (wafanyakazi wa benki ya dunia).

Hii ndio strategy ya Mwakalinga? kurusha rusha hovyo kazi yake na kampuni yake aliyoifanyia kazi? the next thing itakuwa nini - kutaja jina la mke wake na kuanza kumsifia kuwa ni mrembo kuliko mama sophia simba?

Of course sio kwamba Mwakalinga alimpigia magoti Lowassa, alimramba vidole vya miguu pia. Pesa za richmonduli na dowans si mchezo (kwa wafanyakazi wa lucient inaonekana).
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom