Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Mnatuvuruga sana wewe Kubenea. kaeni ktk chama toeni tamko acheni upuuzi wa kuchanganya wanachama kwa matamko ya kila mtu! ujinga mtupu!
 
Na aende tu.
Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu sana.
Taifa limegawanyika kabisa
 

Lusungo uko sahihi sana kwenye andishi lako. Lowassa ni mtu mwenye siasa za kistaarabu kwa mujibu wa mtazamo wako na hata mimi hilo sipingi. Ila cdm kinaendesha siasa ngumu ambazo sio mtindo wa Lowassa. Ili tusimkwaze ndio tunataka aondoke aanzishe chama chake cha kistaarabu, ama ajiunge na TLP au UDP nk kwani hivyo vinamuunga mkono rais wazi wazi. Na kwakuwa tunaaminishwa ana wapiga kura 6m watamfuata huko aliko, aiche cdm na siasa zake za hovyo.

Hayo unayoamini kwamba Magufuli anayafanyia kazi na anakubalika yalipaswa kuonekana kwenye uchaguzi juzi. Lakini unyama uliofanyika ni bora hata enzi za JK ambaye hakuwa na sifa za huyu. Kuwa na siasa za kistaarabu haimaanishi uwe mjinga. Hizo kata 3 unazosema Slaa alipata ni katika mazingira yaliyochangia magari mengi ya polisi kuletwa wakati wa uchaguzi wa 2015. Aliyekudanganya CUF walishindwa kwa siasa zao muambie aendelee kukupa hadithi hiyo hiyo. Kilichotokea uchaguzi wa 2015 ni kituko kingine huko ZNZ. Narudia, simtukani Lowassa, lakini cdm sio sehemu sahihi kwake.
 
Kwa wasiofahamu tu ni kwamba Lowasa na Kubenea wana ukaribu wa miaka mingi hivyo inawezekana kabisa anachoongea kina baraka zake
Mshana.Embu tuliza kichwa tafakari kwa kinaa .weka picha ya ccm iliyokwama kisiasa aina fikra mpya tena .na mbinu pekee iliyobaki ni kuzuia chama chochote kisiwapite walipo kwamia kwa kutumia marufuku ya siasa,Polisi,bunge,mahakama,kukosolewa kuanzia vyombo vya habari mpaka mwananchi wa kawaidi .achilia mbali marisasi na kutekana .embu tafakari alafu linganisha na uamuzi wa Maalimu Seifu wakati ule na Ccm na Cdm wakati huu tulio nao
 
Ni vyema Saed Kubenea akajikita kwenye taaluma yake iliyopelekea akamwagiwa tindikali, mbali na hilo binafsi natambua bila shaka Kubenea ni mojawapo wa wanufaikaji wa pesa alizozitoa Edo.
 
Mtu yeyote aliyekulia Ccm hawezi kudumu upinzani
 
Utapataje tume huru, katiba mpya, tra, tiss na polisi huru bill kuwa mwanaharakati? Magufuli hajabeba uanaharakati Bali ameugandamiza Sana kwa kuwaua wanaharakati na kudampu miili yao cocobeach na pia amezuia na kupiga marufuki mikutano ya kisiasa na majukwaa mengine yote yanayowakutanisha wanaharakati
 
Nikweli kuna mambo mengi yanayo mkabili lowassa ktk binafsi yake, ila kwanini asi wasiliane na uongoz wa cdm, ili iwe ziara ambayo baadaye inakuwa ni rahisi kuwapa majibu wa tanzania?*
 
Easier said than done.
 
Mbona membe, nape, bashe etc wametofautiana sana na Magu.
Lakini you was complaining kwanini wale wabunge wasimuunge mkono wakiwa chadema. Sasa Lowasa amemuunga mkono akiwa chadema, mnalalamika
 
Hizo siasa shindani za kukosoana nendeni mkazifanye Somalia.
Unafikir somalia hapajawahi kuwa na amani? Unafikiri walianza siku moja kufika walipofika? Endelea kuamini kuwa yanayotokea somalia hapa hayawezekani ukidhani una mapolisi na wanajeshi wa kutosha tena wanaouwawa kama vifaranga huko mkuranga na kongo
 
Unafikir somalia hapajawahi kuwa na amani? Unafikiri walianza siku moja kufika walipofika? Endelea kuamini kuwa yanayotokea somalia hapa hayawezekani ukidhani una mapolisi na wanajeshi wa kutosha tena wanaouwawa kama vifaranga huko mkuranga na kongo
Mbona unaanza kuweweseka?
 
haya Team ulipo tupo kwa ufupi wewe ni virus mkuu
 
Kubenea umeeleza vizuri lakini umetupa mfano wa Malim Seif na Karume katika kumbukumbu zangu Seif hakusimama na kuongea na media. Tatizo wa wanachadema hawatendewi haki katika nchi yao.

CCM wajanja sana. Walichokuwa wanatafuta kwa CDM ni kucheza na akili za wanachadema. Angalia igizo lote pale Ikulu mpaka Lowasa a naingia kwenye gari. Ina maana walimwita ili wapate kitu fulani kutoka UKAWA na MZEE wetu hakutambua ya kuwa wanachadema wanahasira namna hii.

Wangekuwa wamemwita kujadili mambo ya maendeleo wasinge ambatana nae vile na kupiga mapicha wakati wanajua kuna mambo ya kurekebisha kati ya Serikali na Ukawa.

Tuangalie wapambe wa CCM walivyolipokea kama Msukuma, Gambo na wengineo. Yaani nikama vile wanamsubiria Lowasa kwa hamu kubwa au wanatafuta amani fulani kwa Ukawa ili ionekane kwamba watanzania tunashirikiana.

Lengo langu ni kwamba Mbowe ndiye M/kiti wa chama na ametoa tamko la chama na tumelisikia. Sisi tuendelee kulikazia lile tamko mpaka hapo atakapofunguka na kueleza kilichotokea mpaka akaongee hayo maneno na kwa Nini alienda bila kuwajulisha viongozi wa Ukawa hata kwa simu.

Wala haina haja ya kumtajataja tena. Punguzeni hasira na haina haja ya kumfukuza tutapasua chama tumwache kama mwanachama na uongozi watahangaika nae kama Shibuda alivyoondoka bila kupasua chama. Ila na sisi tuangalie mzalendo wa Kweli 2020.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…