Kubenea amwaga chozi

Nilijua Kubenea ni Bonge la Mwamba

Kumbe Mlaini tu

Chozi Alilomwaga Kashindwa Hata Kumalizia Shukrani Zake kwa Waandishi Wenzie wa Habari Waliojitoa Kumkomboa

Kweli Sheria ya Utakatishaji Noumer

====


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo imemuachia kwa dhamana Mgombea Ubunge wa Kinondoni kupitia ACT-Wazalendo, Saed Kubenea ambapo kesi inayomkabili itatajwa September 21, 2020.

Kubenea ambaye pia alikuwa Mbunge wa Ubungo (2015-2020), alifikishwa Mahakamani juzi baada ya DPP Biswalo kuidhinisha mashtaka dhidi yake ya kutuhumiwa kuingiza nchini fedha za kigeni bila kutoa tamko na pia kuingia Tanzania kinyume na sheria za uhamiaji.
View attachment 1566836
Msaliti huyo kima..
 
Nimefurahi Kubenea ametoka angalau kwa dhamana kwasababu kila mshitakiwa anastahili uhuru wake hadi hapo mahakama itapomtia hatiani. Lakini nauliza mbona wako wengine wengi wenye kesi za utakatishaji pesa wamenyimwa dhamana, wapo mahabusu kwasababu eti shitaka lao halidhaminiki?
 
Saed Kubenea sasa umebaini awamu hii haitakiwi kusifiwa hata kidogo, ona ni upinzani ndiyo waliokukimbilia kukupatia dhamana na msaada wa kisheria.
 
Kwa hiyo kubenea ni jiwe kwamba hana moments za hisia kama binadamu yoyote yule?
Alikuwa kwenye brink ya kupoteza kila kitu kwa kesi iliyomkuta... kuponea nalo ni heri.
Sisemi kuwa alie lie hovyo.. hapana. But this near life threat situation mwaume akitoa chozi sishangai
Hii haikuwa "near life threat" kama ulivyoiita bali ilikuwa ni "life threat halisi"
 
Mkuu Unacheza Na Rumande Wewe....

Mkuu Tena Uko Ndani kwa TUHUMA za Kutakatisha Fedha....

Acha Kabisa Mwana!!

Ana Haki Ya Kumwaga CHOZI zaidi ya kipindi kileee ALICHOSHAMBULIWA akiwa na Akina Ndimara Tegambwage!!
 
Ndio maana Lissu anasema kwenye kampeni zake kuwa Magu ni katili.
huyu ndo anayejua kuropoka siku hiyo atalia machozi ya damu,wapo kimya hao jamaa wanaongezea tu makosa juu ya yale anayo ya kuropoka huko nje,kuruka dhamanA,kejeli kwa rais JPM,USALITI,KUHUJUMU UCHUMI.
Iko siku tu amuulize mwenyeji wake huko Ubelgiji Rusesabagina huwaje kajikuta jela huku ana nobel prize ya amani
 
Wacha alie tu, yeye ambaye alikuwa Mbunge anafahamu sheria za nchi, kutoka na kuingia nchini ni lazima taratibu zote zifuatwe. Vile vile anafahamu kabisa swala la kuingiza pesa nchini bila ku-declare. Zito hakwenda Kenya? Then mnasema JPM ni katili,kwani yeye ndiye aliweka hizo sheria? Rais anachaguliwa kulinda katiba na sheria tulizojiwekea. JPM fanya kazi kelele za mlango zisikunyime usingizi.
 
Ndio maana Lissu anasema kwenye kampeni zake kuwa Magu ni katili.
Hahahaa usiguate sheria kisha usingizie magufuli?
Hii nchi mnataka iendeshweje?
Wasipofuata sheria mnalalamika wakifuata sheria wana roho mbaya, nyie ni watu wa namna gani?
MTU kama kubenea ni mtu maarufu, sasa anawezaje kwenda kenya kwa njia za magendo?
Pia huyohuyo anaetaka aende kwa magendo utamkuta anasema serikari haifuati sheria akiwa kwenye majjukwaa,

Sasa anataka serikari ifuate sheria kwa nani kama sio kwa yeye na wengine?
Acheni kuishi kwa mazoea.
 
Ila kuwa mpinzani inataka moyo sana ... there is alot to give ... Mungu awasaidie
 
Back
Top Bottom