Kubadilishana lugha ya Kichina na nyingine duniani kunakuza utandawazi na maendeleo

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Kubadilishana lugha ya Kichina na nyingine duniani kunakuza utandawazi na maendeleo

Na Ronald Mutie


Utandawazi unavyozidi kukua ndivyo mahitaji ya kujifunza yanaongezeka kutoka kwa nchi moja hadi nyingine.

Mojawapo ya vikwazo vya kujifunza hata hivyo imekuwa ni tofauti ya lugha na tamaduni.

Lakini sasa maendeleo mapya ya elimu yameendelea kukuza mabadilishano na kujifunza lugha mbalimbali na hivyo kuchangia upitishaji wa haraka wa ujuzi na teknolojia.

Wamarekani wengi sasa wanajinza lugha za Afrika kama vile Kiarabu, Kiswahili na Kihausa ili kurahisisha mawasiliano na biashara.

Na jinsi uchumi wa China unavyokua kwa haraka mahitaji ya kuwasiliana na ulimwengu pia yameongezeka.

Ili kutimiza mahitaji ya kuwasiliana na mataifa mengi duniani wachina pia wanajifunza lugha za nchi mbalimbali.

05131.png

Nchini China karibu vyuo vyote vikuu vinatoa mafunzo ya lugha za kigeni lakini maarufu zaidi ni Beiwai mjini Beijing vile vya miji ya Shanghai, Tianjin, Xi‘an, Guangzhou na Dalian.

Mafunzo hayo yamechangia pakubwa katika uhamishaji wa teknolojia ya China kama vile utengenezaji, matibabu na ujenzi wa miundombinu kwenye nchi nyingi duniani.

Lakini watu wengi duniani wameendelea kujifunza lugha ya Kichina kupitia kwa taasisi za Confucius.

Hadi mwaka 2020 tayari China ilikuwa imeanzisha taasisi 541 za Confucius katika nchi na maeneo162 duniani, Afrika ikiwa na 54.

Lakini sio kwa ajili ya kufunza lugha tu bali pia na kufunza ujuzi na utamaduni kwa kutumia lugha ya Kichina.

Taasisi ya Confucius ilioko katika chuo kikuu cha Egerton nchini Kenya ni ya kipekee kote duniani kwani inatoa sio tu mafunzo ya Kichina lakini pia na kufunza teknolojia ya kilimo kwa lugha hiyo.

Ilianzishwa mwaka 2012 kwa ushirikiano cha chuo kikuu cha Egerton na chuo kikuu cha kilimo cha Nanjing kutoka China.

05132.jpg
Kenya kama zilivyo baadhi ya nchi za bara la Afrika inakabiliwa na changamoto ya kutojitosheleza na chakula kutokana na hali ya anga isiyotabirika.

Lakini kwa kupitia mbinu za kisasa za kilimo sasa uzalishaji wa chakula unaweza kuongezeka sio tu kutokana na mafunzo lakini mafunzo yanayotolewa na wataalam wa China kwa lugha ya Kichina ambayo tayari wanafunzi wa Kenya wanaifahamu.

Na hivi karibuni zaidi wahudumu kadhaa wa afya wa Sudan Kusini walianza kujiandikisha kwa masomo ya lugha ya Kichina yanayofundishwa katika mji mkuu Juba na washiriki wa kundi la nane la timu ya matibabu ya Wachina.

Serikali ya China imekuwa ikiisaidia Sudan Kusini kuboresha huduma za afya katika Hospitali ya kutoa elimu ya matibabu ya Juba, na sasa madaktari wa huko wanakaribisha maendeleo haya mapya wakiyataja kama ukurasa mpya wa ushirikiano.

Moses Maror, daktari wa miaka 42 katika idara ya uzazi na magonjwa ya wanawake katika Hospitali hiyo ya Juba, anasema ana nia ya kujifunza lugha ya Kichina ili kuelewa vizuri utaratibu wa matibabu wa Kichina na dawa.

"Nina nia ya kujifunza Mandarin kuwasiliana vizuri na wenzangu Wachina katika idara ya uzazi na magonjwa ya wanawake," alisema Maror.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Pawil Arop Yor, alishukuru serikali ya China kwa kusaidia kwenye utoaji wa mafunzo kwa madaktari kwa lugha ya Kichina, pamoja na kutoa dawa kwa hospitali kuu ya rufaa.

"Wanafanya mambo mengi hapa. Ningependa kushukuru serikali ya China kwa kutusaidia na dawa na sasa watatufundisha lugha ya Kichina," alisema Yor wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo.

Mifano hii miwili ya utoaji wa mafunzo kwa kutumia lugha ya Kichina na kuongezeka kwa idadi ya wachina wanaojifunza lugha za kigeni, ni ishara kuwa na dunia yenye mwelekeo mmoja kwa mawasiliano, maendeleo, mabadilishano na hatma ya pamoja ya binadamu.
 
Back
Top Bottom