Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,402
- 12,792
Nimejiandaa kwa kuomba ushauri na kuongea na watu mbalimbali ambao tayari wameshaipita hiyo njia.
Tajiriba yao pamoja na hekima na busara zangu ndo zitakuwa mwongozo wangu.
Halafu ndugu na wazazi si lazima mchangie damu. Na undugu wa damu si kila kitu. Ingekuwa ni kila kitu basi kusingekuwepo na mifarakano ya ndugu ambayo hupelekea hadi watu kupoteza maisha.
Mimi kwangu ndugu ni yeyote yule anayenithamini, kuniheshimu, na kunijali kwa nyakati zote, iwe shida au raha.
Na maishani kuna watu wengi tu mioyo mizuri ambao wamewahi kuwasaidia watu baki kuliko hata ndugu za hao watu baki.
Cha muhimu hapa ni ubinadamu. Na hayo ndo maadili ninayomfunza binti wangu na namfunza kwa matendo pia. Siyo maneno tu.
Na hili suala la kuasili ni mojawapo ya funzo la matendo.
Mwenye Enzi Mungu, Muumba wa Mbingu na vijazavyo akujaalie Maisha marefu yenye hekma na moyo wa kusaidia kama ulivyodhamiria...akuinue na kuwa viongozi wa wengine ambao hawana maono kama haya ili kupitia wewe na wao wimbi la watoto wanaoishi kwenye mazingira yasiyo rafiki kwa sababu mbali mbali lipungue na hatimaye liishe kabisa!