Kuasili mtoto

Kuasili mtoto

Hapo red ndo nilichotaka kumwambia comrade wangu Nyani Ngabu .... Binamu yangu mmoja ambaye hakubahatika kupata mtoto wa kiume aliamua kufanya maamuzi ya kuasili. Na kama unavojua mambo yetu ya kiafrika watu walikuwa wakizungumza chini kwa chini... wengine wakimshangaa kwanini hakuamua kumchukua mtoto wa ndugu maskini ili amlee kama mwanae...

Miaka kadhaa baadae yule mtoto akajua yeye si damu ya wazazi wale. Na wale mabinti warembo aliokuwa akiwaita dada sio dada zake wa damu. Aisee...aliwapiga miti wale mabinti (dada zake) ile kinoma..... Mpaka dingi kuja kushtukia ilikuwa too late. Shughuli ndio ikaanzia hapo, dogo haeleweki na baba hana cha kufanya.

Hapa komredi anapaswa awe makini sana. Kiafrika wanaokuja kuharibu mambo ni ndugu. Ila kama ni kwa huko USA baby, yawezekana mambo yakawa tofauti.

Kiafrika, mambo ya kuasili bado hayajakaa sawa kiviile nadhani kwa sababu tushazoea mambo ya extended families. Ndugu zako maskini watamwonea wivu mtoto uliyemuasili ambaye anakula good time.

Kama alivodokeza komredi, hii ishu kiafrika inahitaji tathmini, ujasiri na uthubutu uliotukuka.

Mawaidha kuntu sana hayo Komredi.

Shukran jazilan!
 
Amewahi jinadi hapa ana mtoto wa kike...
Sasa anataka nini???
Kiongozi kuasili mtoto hakuna uhusiano wowote na kukosa uzazi. JK kama sikosei ameasili mtoto pamoja na kuwa ana watoto kadhaa kwa wanawake kadhaa...
 
In the end, we only regret the chances we didn't
take, relationships we were afraid to have, and the
decisions we waited too long to make.....

Mark my Words

I like those words.
 
Yeah, process ni ndefu kiasi kwamba, unatakiwa uwepo Tanzania kipindi kirefu kuyashughulikia hayo mambo; hii ni kama uko nje ya nchi, ili uweze kulifanikisha suala zima!. Nyani Ngabu!.

I see.

Labda sasa serema serema ya Ngosha watu watachapa kazi na mizungusho itaisha.

Tutaona.
 
Utakuja kuasili mla vumbi huku mavumbini?
Mavumbini baby[emoji12] [emoji626]

Hahahaaa. That's yet to be determined.

USA baby
upload_2016-7-24_13-44-28.png
upload_2016-7-24_13-44-33.png
upload_2016-7-24_13-44-34.png
 
Nimejifunza nenojipya la Kiswahili leo, nilikuwa sijui kama kuasili ndiyo kuadopt. Ni jambo jema sana unalotaka kulifanya. Naamini umeamua kufanya hivyo kwa kuona unaweza kumpa malezi mazuri na bora mtoto huo ili naye aje kuwa raia mwema kwenye siku za usoni.

Bila shaka utakuwa umeamua pia ni umri upi ambao ungependelea mtoto huyo awe nao. Wataalamu wengi wa mambo ya watoto na saikolojia wanadai kwamba mapenzi ya baba na mama ni muhimu sana katika malezi ya mtoto ili kufanikisha malezi hayo kuja kutoa raia mwema, lakini kuna mifano chungu nzima ya watoto ambao wamelelewa na baba /mama tu kwa sababu mbali mbali ikiwemo vifo, kutengana na maisha ya siku hizi baba anafanya kazi mji/nchi nyingine n.k.

Hivyo kila la heri na baraka natumai ukiamua kuitimiza hii adhma yako mtoto utakayemchagua atakuwa ni mtoto wa Kitanzania.
 
Back
Top Bottom