Kuasili mtoto

Kuasili mtoto

Nimejifunza nenojipya la Kiswahili leo, nilikuwa sijui kama kuasili ndiyo kuadopt.

Naam, Kiswahili kinajitosheleza sana tu na ni kitamu kweli kweli.

Ni jambo jema sana unalotaka kulifanya. Naamini umeamua kufanya hivyo kwa kuona unaweza kumpa maelezi mazuri na bora mtoto huo ili naye aje kuwa raia mwema kwenye siku za usoni.

Kabisa. Ningekuwa sina uwezo hata hilo wazo lisingenijia. Huwa napenda sana kusaidia watu wasio na bahati ya maisha mazuri hususan watoto.

Bila shaka utakuwa umeamua pia ni umri upi ambao ungependelea mtoto huyo awe nao. Wataalamu wengi wa mambo ya watoto na saikolojia wanadai kwamba mapenzi ya baba na mama ni muhimu sana katika malezi ya mtoto ili kufanikisha malezi hayo kuja kutoa raia mwema, lakini kuna mifano chungu nzima ya watoto ambao wamelelewa na baba /mama tu kwa sababu mbali mbali ikiwemo vifo, kutengana na maisha ya siku hizi baba anafanya kazi mji/nchi nyingine n.k.

Suala la umri ni moja ya mambo ya juu kabisa ya kuzingatia katika orodha ya mambo yanayohitajika katika jambo kama hilo.

Hivyo kila la heri na Baraka natumai ukiamua kuitimiza hii adhma yako mtoto utakayemchagua atakuwa ni mtoto wa Kitanzania

Shukran sana rafiki.
 
Kiongozi kuasili mtoto hakuna uhusiano wowote na kukosa uzazi. JK kama sikosei ameasili mtoto pamoja na kuwa ana watoto kadhaa kwa wanawake kadhaa...
He aint a MEENN....
 
Hahaaa sina bana.

Natia huruma eeh?

Mkuu frankly speaking wewe ni mwanachama wa muda mrefu ambaye kwa namna moja ama nyingine umeinspire bila kujua vijana wengi waliozaliwa utawala wa Mkapa na kuendelea...mara nyingi umekuwa ukitoa shauri zenye harufu ya beberu ukimaanisha wewe ni dume, si la mbegu tu bali la kutotolesha..sasa mkuu bila kuathiri wazo lako la kuasili huoni kwamba uamuzi wako wa kupanda vyeo vyote kutoka Boyfriend msaidizi hadi Senior Assistant Commissioner wa haya mambo ya mahusiano bila kuweka mtu ndani utapelekea uzazi kuwa stagnant?
 
Hivi kwani kila anayeasili ni kwamba hana mtoto/ watoto? Ni kwamba hana uwezo wa kuzaa?

Mbona watu mna mawazo fungwa hivyo!

Tatizo ni ujinga au upumbavu au vyote kwa pamoja?

Come on now man...
 
Hayo uliyoyasema yanawatia hofu wengi sana wanaotaka kulifanya hili jambo zuri. Na kweli hutokea mtoto anapogundua kwamba wewe/nyinyi si wazazi wake basi anakasirika sana na kutaka kufahamua kuhusu wazazi wake na kwanini walimtelekeza na huweza hata kusababisha chuki kubwa kwenu.

Ni jambo ambalo linahitaji moyo wa uvumilivu mkubwa sana, lakini kuna wengi wanafanikiwa na watoto huwaona hao ni kama wazazi wao kabisa kwa malezi mazuri waliyowapa ikiwemo elimu na hivyo kuja kuwa watu bora ambao wanaweza kusimama kwa miguu yao miwili bila kuwa tegemezi kwa yeyote yule.

Kwakweli,Hilo wazo hata mimi nimekuwa nalo kwa muda mrefu sana ila nilikatishwa tamaa sana na partner wangu... Kwanza aliniambia kuna tabia za kurithi anaweza akawa na tabia mbaya ambayo inaweza ikaleta athari katika mahusiano yetu. Pili,mtoto huyo akishajielewa na kufahamu kuwa sisi sio wazazi wake mtazamo wake juu yetu pia unaweza ukabadilika pengine akaona he/she has nothin loose coz sisi sio ndugu zake wala wazazi wake...
Personally,nilipinga sana kwasababu naona hayo ni matokeo tu. So long as atakuwa treated kama wenzie tulionao tusiwaze sana negative outcome but mwenzangu hakulipenda sana hilo wazo.

But @ Nyani Ngabu kama hiki wazo unalo endelea nalo ..Mimi nataman mpaka kesho.
 
Hivi kwani kila anayeasili ni kwamba hana mtoto/ watoto? Ni kwamba hana uwezo wa kuzaa?

Mbona watu mna mawazo fungwa hivyo!

Tatizo ni ujinga au upumbavu au vyote kwa pamoja?

Come on now man...

Nimetanguliza 'bila kuathiri wazo lako' tafuta hata kabinti kamoja kaliko occupied kabadili status kawe 'singo' kisha mdouble ili uweze kumlea huyo mtoto vizuri mkuu...kulea kuna changamoto zake mkuu esp kwenye early stages!
 
Ngoja kwanza, maana sijakuelewa na nadhani hata wewe hujaelewa kabisa.

Ina maana ulichoking'amua hapa ni kwamba mimi sina mtoto au?

Manake naona kama vile kuna tatizo la kusoma na kuelewa ulichokisoma.

Tuanzie hapo kwanza...
 
Nimekuelewa... suala la kuasili mtoto si jambo baya..yumkini una m/watoto ila kwa nature ya binadamu tumezaliwa tukiwa wabinafsi tokea siku ya kwanza...umejiandaaje na changamoto za makuzi ya mtoto unayemwasili pale atakapokua na kugundua kwamba wewe si mzazi Biological na kwamba hata ndugu aliodhani ni wake(wanoa wengine) kwamba siyo?
 
Why unamkejeli mwenzio lakini?

Mkuu heshima yako...binadamu tumeumbwa tofauti na wenye mahitaji tofauti ili turekebishane na kusaidiana kuelekezana ili dunia iwe sehemu bora ya kuishi! Asamehewe bure tu huwezi jua stress za maisha na uhakiki wa vyeti unaoendelea ukawa changizo!
 
Nimejiandaa kwa kuomba ushauri na kuongea na watu mbalimbali ambao tayari wameshaipita hiyo njia.

Tajiriba yao pamoja na hekima na busara zangu ndo zitakuwa mwongozo wangu.

Halafu ndugu na wazazi si lazima mchangie damu. Na undugu wa damu si kila kitu. Ingekuwa ni kila kitu basi kusingekuwepo na mifarakano ya ndugu ambayo hupelekea hadi watu kupoteza maisha.

Mimi kwangu ndugu ni yeyote yule anayenithamini, kuniheshimu, na kunijali kwa nyakati zote, iwe shida au raha.

Na maishani kuna watu wengi tu wenye mioyo mizuri ambao wamewahi kuwasaidia watu baki kuliko hata ndugu za hao watu baki.

Cha muhimu hapa ni ubinadamu. Na hayo ndo maadili ninayomfunza binti wangu na namfunza kwa matendo pia. Siyo maneno tu.

Na hili suala la kuasili ni mojawapo ya funzo la matendo.
 
Mkuu heshima yako...binadamu tumeumbwa tofauti na wenye mahitaji tofauti ili turekebishane na kusaidiana kuelekezana ili dunia iwe sehemu bora ya kuishi! Asamehewe bure tu huwezi jua stress za maisha na uhakiki wa vyeti unaoendelea ukawa changizo!
Ha haa na kweli,tatizo la vyeti ni shida nyingine
 
Ni nzuri hii idea ht mimi mambo yakiwa sawa nitafanya hivyo sema watafutie mama yao mkuu utalea matom boys lol..
 
Back
Top Bottom