Kuanzia wiki ijayo sitokula sato wala sangara

Sasa uwezo wa kivuko ni kubeba watu 100, nataarifa za awali zinadai kilikuwa kimebeba watu 400, bado kuna mtu anakuja anadai eti kuna jamaa kaacha mkosi.
Kungekuwa na kivuko kikubwa au zaidi ya kimoja kilicho sawa na uwiano wa Idadi ya wasafiri haya yangetokea?
 
hapo ndipo ujinga wa baadhi ya watu unapoonekana!! hakuna cha mkosi wala nini!! Tufikie watanzania tuviheshimu vyombo vya usafiri Mzungu anapotengeneza uwezo wa chombo ni kubeba uzito kadhaa basi lizingatiwe!! kumbuka pia Mv Bukoba ilikua wame overload, hii nayo wameoverload!! hii ni shida
Siku zote binadamu ni mtu wa kuharakia na hapo anakuwa hajali hata usalama na ndo maana kunakwepo na sheria kanuni na taratibu...

Mule kuna wachache waliokuwa wakitambua hicho unachosema (kwamba tumezidi) lakini hawangekuwa tayari kupungua kwajili nao wapo katika kuharakia harakati za kimaisha...

Lakini kundi kubwa hawakujua hilo Jambo la kuzidi na hata wakijua hawangekubali pia vilevile kupungua kwa hiari yao mpaka kutumike sheria...

Katika sheria hizo kunakwepo na wasimamizi wa sheria hizo (viongozi )...

Swali ni kwamba je mpaka watu wanaoverload hao wasimamizi wa sheria walishindwa kusimamia sheria (kupunguza kilichozidi)?

Tusiwe tunatukana tu watu waliokufa na kuona kama wamekufa kizembe laa!
Hakuna anaependa kufa
 
Back
Top Bottom