Kuanzia leo silali na smartphone, zijue sababu

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,188
3,367
Nakumbuka enzi za nokia ya tochi ikifika night kali karibu watu wote wamelala na hakuna wa kuchat nae wala wa kumpigia hivyo na wewe inabidi ulalae tu labda uwe na jambo la msingi la kufanya.
Hali hii ilianza kupotea baada ya kuletwa kwa smartphone ambazo kwa sasa zimepungua bei sana na kumilikiwa na watu wengi sana, Si ajabu hata team popo zilianza kutokana na hizi simu, Ndani ya simu kuna facebook, instagram, whatsapp, youtibe, kucheki movie, kucheza game N.k yani kiufupi hizi simu ukilala nazo kama huwezi kujicontroll unaweza kuingia kitandani saa nne ukaichezea simu hadi saa nane ndio ulale na sasa nimeamua pindi niingiapo kitandani simu naiaga mezani kwa sababu hizi.

Kutunza macho yangu:Nikiingia kulala nazima taa na nikitumia simu mwanga ule unavonipiga macho unaharibu macho yangu.

Kuepuka kero ya kuamka nimechoka: kuna hangover za pombe ila smartphone zimeleta hangover zake, Mwanadamu inabidi apate uaingizi masaa 8 kwa afya njema ila hizi smartphone zinaingilia sana ratiba yangu ya kulala na kufanya niamke na uchovu.

Kuepuka kupiga ngunga: Bado sijaoa ila nina mchumba na usiku nnalala peke yangu, Kuna yale matangazo unakuta yamejiminya Chura huyoooo anarukaruka, hapa kama siku hiyo siwezi kujocontroll sinaga budi kuurudia uanachama wa chaputa

Kujilinda na ugonjwa wa usahaulifu: Kadiri unavyojinyima usingizi unapunguza masaa ya kulala na kesgo yake sio mwili tu unakuwa umechoka bali hata akili, Hii tabia ikiendelea kwa muda mrefu unakuwa mtu ambae unasahau sahau
 
Tangu saa 3 nipo kitandani hadi sasa mkuu.....,nakumbuka Siemens a25
 
Back
Top Bottom