Leo Nimeota CCM imeng'olewa madarakani na Umoja Wa Katiba Ya Wananchi (UKAWA).Wananchi walijitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura.Baada ya matokeo ya awali kuanza kuonyesha CCM ina hali mbaya na UKAWA kuonekana kuwa tishio,kama kawaida yao CCM wakaanza mbinu zao chafu za kutaka kutumia mabavu kuchakachua matokeo lakini mawakala wa UKAWA na wafuasi wao walisimama kidete kuhakikisha matokeo hayachakuchuliwi na CCM,baada ya kushindikana kwa hila hiyo ikabidi kwa shingo upande Tume ya Uchaguzi ianze kutangaza matokeo rasmi,lakini kadri matokeo yalivyozidi kutangazwa ndivyo CCM ilivyozidi kugaragazwa na UKAWA katika nafasi zote za Wagombea kuanzia Urais,Wabunge na Madiwani.Baada ya CCM kuona matokeo yamewaendea ndivyo sivyo,wakailazimisha Tume ya Uchaguzi kusitisha kuutangaza matokeo kwa kisingizio kwamba kuna baadhi ya maeneo yalikiuka kanuni na taratibu za uchaguzi hivyo matokeo yaliyotangazwa yatafutwa na kuhesabiwa upya.Wananchi kusikia hivyo nao hawakukubali,wakaiingia mitaani kuandamana na kuipinga serikali kwa hatua yake ya kubatilisha matokeo,serikali kuona wananchi wanaandamana ikawapeleka askari polisi mitaani kwenda kuwadhibiti wananchi,safari hii wananchi hawakukimbia kwani walijiandaa hasa kupambana na lolote lile litakalo kuja mbele yao.Mapambano kati ya wananchi na polisi yakaanza,polisi wakitumia silaha za moto na wananchi wakitumia kila aina za silaha za jadi,polisi wakazidiwa kwani wananchi walikuwa wakiongezeka makundi kwa makundi,likaitwa jeshi la wananchi kusaidia kudhibiti wananchi walioamua kulinda na kutetea haki yao inayotishiwa kuporwa na Watawala.Lakini wananchi hawakurudi nyuma,sasa ikawa vita kamili,wananchi wakaanza kuvamia vituo vya polisi na baadhi ya kambi na kupora silaha,hali ikawa mbaya sana,baadhi ya wanajeshi na polisi wakaanza kuasi na kuungana na wananchi,CCM na baadhi ya wanausalama wake watiifu wakazidiwa na kuamua kukimbia nchi.Hatimaye UKAWA wakaitwaa nchi. Na Ndoto yangu ikaishia hapo.