Kuahirishwa kwa Safari ya Mwanza......

Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,306
2,000
Kwa heshima na taadhima.........naomba nisogee mbele yenu.....(kwa niaba ya Arusha Wing).......kwa masikitiko......kuwaeleza wale wote waliokuwa wanatutarajia wageni wao kutoka Arusha kuelekea Mwanza.......kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu........(majukumu kuzidi)......tutashindwa kuhitimisha safari yetu hii kwa sasa hadi hapo tutakapoweza kujipanga tena.

Shukrani zetu zimwendee kila mmoja wenu......ambao mlikuwa mmejitolea kutupokea na tuwaombe samahani sana.......kama binadamu huwa tunapanga.....lakini mpangaji mkuu huwa ni Mungu.....

Mpendwa wetu charminglady.......tunaomba radhi kwa kutokuweza kufika.......umejitahidi sana kutuwekea mambo sawa lakini ndio kama hivyo tena........tunaomba uwafikishie na wengine uliokuwa nao kwenye team yako salam zetu hizi za masikitiko.......tutakuja siku nyingine........

Tunawashukuru wote mlioonyesha moyo wa kuungana na sisi.......Mungu atajalia tutafanikisha hili.........siku zijazo.......

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/547912-jf-mwanza-wing-mpo-arusha-wing-tunakuja-kuwashikaaa.html..

Asanteni Sana.........

cc: Filipo.. marejesho.... Arushaone.... Valentina.... Tonykp.... Lily Flower..... PakaJimmy..... Dark City.... Mwanyasi..... SnowBall.... IGWE... LiverpoolFC.... Madame B.... Mzee wa Rula... Kaizer.... watu8... KOKUTONA.... Cantalisia.... Blaki Womani......

Last edited by a moderator:

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
58,491
2,000
Ayaaaahh...

Dr unajua nilishaaga hapa mtaani kuwa naenda kukutana na Preta wa jeiefu...sura yangu sijui nitaificha wapi mimi!!!

Hata hivyo kama ulivyotangulia kuandika, Mola ndiye mpangaji wa zetu ratiba.

Atatujumuisha tu tena panapo majaaliwa yake!
 
Last edited by a moderator:

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,183
2,000
Kwa heshima na taadhima.........naomba nisogee mbele yenu.....(kwa niaba ya Arusha Wing).......kwa masikitiko......kuwaeleza wale wote waliokuwa wanatutarajia wageni wao kutoka Arusha kuelekea Mwanza.......kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu........(majukumu kuzidi)......tutashindwa kuhitimisha safari yetu hii kwa sasa hadi hapo tutakapoweza kujipanga tena.

Shukrani zetu zimwendee kila mmoja wenu......ambao mlikuwa mmejitolea kutupokea na tuwaombe samahani sana.......kama binadamu huwa tunapanga.....lakini mpangaji mkuu huwa ni Mungu.....

Mpendwa wetu charminglady.......tunaomba radhi kwa kutokuweza kufika.......umejitahidi sana kutuwekea mambo sawa lakini ndio kama hivyo tena........tunaomba uwafikishie na wengine uliokuwa nao kwenye team yako salam zetu hizi za masikitiko.......tutakuja siku nyingine........

Tunawashukuru wote mlioonyesha moyo wa kuungana na sisi.......Mungu atajalia tutafanikisha hili.........siku zijazo.......

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/547912-jf-mwanza-wing-mpo-arusha-wing-tunakuja-kuwashikaaa.html..

Asanteni Sana.........

cc: Filipo.. marejesho.... Arushaone.... Valentina.... Tonykp.... Lily Flower..... PakaJimmy..... Dark City.... Mwanyasi..... SnowBall.... IGWE... LiverpoolFC.... Madame B.... Mzee wa Rula... Kaizer.... watu8... KOKUTONA.... Cantalisia.... Blaki Womani......

images
 
Last edited by a moderator:

Mwanyasi

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
7,926
2,000
mpendwa pole sana......kama alivyotangulia kusema mwenzetu majukumu yamezidi tuombe mungu atujalie uzima na afya atujalie kipindi kijacho wasalimie Mwanza wing wote

Imewahi kunikuta naandaa mapokezi ya wageni nikafanya booking ya hotel kwa makubaliano kuwa wageni watalala hapo. Si wakakimbia baada ya kuona lodge za bei rahisi bana. charminglady please we are sorry!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,255
2,000
Tumekuelewa Preta, na tunafahamu jinsi haya mambo yalivyo magumu....

Ila hatuwezi kuacha kuhuzunika na kuugua mioyoni kwa sababu "Hamu ni tamu sana".....sasa naona hata hiyo hamu imetoweka..... Tu wageni wa nani sasa?

Mubarikiwe sana ili next time tuwe na mipango inayopangika!!

babu DC!!
 
babu mpaka dakika ya mwisho kila kitu kilikuwa kama kilivyopangwa............sasa kufika nchani ndipo palipokuja kuvurugika.......
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom