kuagiza gari

mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
559
nataka kuagiza gari japan, ni toyota super custom van 8 seaters ya mwaka 1994. mwenye ufahamu na mambo ya kodi pale bandarini dar tafadhali aning'ate sikio namna itakavyokuwa taxed niangalie mfuko wangu vzuri kabla cjalipia. cif yake imesimama usd 7000.
 
Andaa Tshs21,124,950 Nime asume US$1= Tshs1,550.

Hili gari lina umri zaidi ya miaka10

Us$7,000 rate Us$/Tshs1550

CIF 10,850,000
IMPORT DUTY 2,712,500
ANT DUMPING 2,712,500
EXISE DUTY 1,627,500
VAT 3,222,450
TOTAL 21,124,950

Tax rates

Import duty ni 25% ya CIF

ANT DUMPING ni 20% ya (CIF+Import duty)
EXISE DUTY 10% ya (CIF+Import duty+ANT DUMPING)
VAT ni 18% ya (CIF+Import duty+ANT DUMPING+EXISE DUTY)
 
nafikiri ezan kashamaliza , yaaaani ndio maana hatundelei gari la dola 7000 unalipa ushuru mil 21 wapi na wapi , mkuu ka unaweza unavyotuma hela huko japana , fnya transfer mara 2 , yaaani dola 3500 alafu dola 3500 , ili wakupe risiti 2 , so unaweza kuwaambia watu wa tra/bandarini umenunua kwa dola 3500 ingawa na wao wata uplift kidogo inaweza kusaidia ni mtazamo tu .......
 
Bado. Utalipia port charges kama dola 400. Motor vehicle registration tsh 300000. Agency fee tsh 150000. Uongo kidogo tsh 100000
 
nashukuruni sana kwa mchanganuo, i real was un aware zaidi tu ya kujua nitatakiwa kukamuliwa damping charges, idea ya kufinya cif ktk receipt naiona nzuri. tatizo langu napendelea sana super custom na manual na kwa sasa magari ya hivo huyapati mpaka ya zamani sana over 10 yrs. bwana congo when am ready hasa baada ya kurudi bongo April mwanzoni nitaomba uniunganishe na clearing agent nisuke naye mpango mzima
 
Nakushauri masuala ya kutuma 3500 kwa risiti mbili inaweza kukugharimu sana. Wanauwezo wa ku-trace hiyo gari na kuona bei yake kirahisi sana. Jamaa yangu alijaribu huo mchezo ukamgarimu kuliko alivyo tarajia. Huwezi kumdanya mtu hiyo gari umeipata kwa usd3,5000 bei za magari zinajulikana huwezi kudanganya kirahisi.
 
Ilikuwaje? alitakiwa kufidia?
Nakushauri masuala ya kutuma 3500 kwa risiti mbili inaweza kukugharimu sana. Wanauwezo wa ku-trace hiyo gari na kuona bei yake kirahisi sana. Jamaa yangu alijaribu huo mchezo ukamgarimu kuliko alivyo tarajia. Huwezi kumdanya mtu hiyo gari umeipata kwa usd3,5000 bei za magari zinajulikana huwezi kudanganya kirahisi.
 
nafikiri ezan kashamaliza , yaaaani ndio maana hatundelei gari la dola 7000 unalipa ushuru mil 21 wapi na wapi , mkuu ka unaweza unavyotuma hela huko japana , fnya transfer mara 2 , yaaani dola 3500 alafu dola 3500 , ili wakupe risiti 2 , so unaweza kuwaambia watu wa tra/bandarini umenunua kwa dola 3500 ingawa na wao wata uplift kidogo inaweza kusaidia ni mtazamo tu .......

Nadhani hiyo milioni 21 amejumlisha pamoja na bei ya manunuzi(ie usd 7,000) kodi pekee itakuwa Tsh. 10,274,950
 
Ezan ametoa maelezo mazuri.Mara nyingi hesabu za haraka haraka mpaka unalitoa gari inakuwa kama mara 2 ya CIF.Kwa mfano hilo gari lako la USD 7000 maana yake andaa USD 7000 nyingine kukombolea.
 
Back
Top Bottom