Kuachwa na mpenzi bila sababu

Kuachwa na mpenzi bila sababu

alichokisema kipi mkuu hakusema kitu ndo kinachoniuma miaka na miaka
Miaka na miaka? Why can't you let go? Ujana ni maji ya moto, hasa kama kijana hajaamua kwa dhati kabisa kutulia na mpenzi mmoja. Hakuna jinsi unaweza kumtuliza.

Na pia, kuna wakati unaona sio vizuri kumwambia ukweli wa tabia zake, labda mtu ana tabia fulani zinakera lakini hakukosei kiasi cha kupata sababu za kuachana.

Wewe jua tu kuwa ujana ni maji ya moto, akiondoka bila kusema kitu jua kuwa kuna "better choice" kwake au kakuchoka anataka mwingine.
 
Miaka na miaka? Why can't you let go? Ujana ni maji ya moto, hasa kama kijana hajaamua kwa dhati kabisa kutulia na mpenzi mmoja. Hakuna jinsi unaweza kumtuliza.

Na pia, kuna wakati unaona sio vizuri kumwambia ukweli wa tabia zake, labda mtu ana tabia fulani zinakera lakini hakukosei kiasi cha kupata sababu za kuachana.

Wewe jua tu kuwa ujana ni maji ya moto, akiondoka bila kusema kitu jua kuwa kuna "better choice" kwake au kakuchoka anataka mwingine.
Aisee pole sana dada.....Ila mnapokoseaga ni kuwaruhusu mapema kabisa kuwapa mlichonacho.........Ila pia ni changamoto ya kawaida....kaza moyo....Pia mjitahidi kuwa halisi....(kuwa real)...msiigize....wanaume sisi ni wajanja.
 
Anakuwa amekuchoka tu. Na hizo lawama ni sabb tu.
Km unampenda mpenz wako utamvumilia na kila anapokosea lzm umwambie tu.
Weny mapenz ya dhat watakuwa wameshanisoma, kupenda ni noma. Ni zaidi ya upofu.
 
hata kama
1. Tabia na akili za kitoto Toto.
2. Muonekano tofauti na aliokuwa anautarajia MF. Mavazi, usafi wa ndani ya mwili, na jinsi unavyojiweka.
3. Vipaumbele vyako MF. Unapenda sana hela, hata kama husemi akiiangalia akili yako anaona future ilivokaa, hulka yako such as uropokaji au vijitabia vya hovyohovyo ambavyo wewe unaona poa tu, hasira unazozificha au makucha yalofichika
4. Nafasi yake kwako..kujionyesha tu kuwa unabwana but deep down akichunguza we ndo walewale.

Na vingine vingi ambavyo mwanaume akipima anaona kabisa haviwezi kubadirika. So hata Mimi utaona manyoya tu, na ishatokea saana.
 
Pole sana kwa yaliyokupata. Usikate tamaa. Kila jambo lina sababu ya kutokea. Kwa kawaida, ni vizuri mtu akaeleza sababu inayomfanya afikie uamuzi huo. Lakini ikitokea hatoi sababu, basi usiruhusu hali hiyo ikutese. Jipe moyo, ukiamini kwamba kwa namna moja au nyingine Mungu amekuepusha na jambo fulani. Mimi ninaamini kabisa, ya kwamba wakati wako unakuja na furaha yako itakamilika.

Jambo la msingi, lipokee na usiendelee kulitafakari. Kwa sababu kadri unavyoendelea kutafakari sababu zilizomfanya afikie hayo maamuzi, ndivyo unavyojiweka kwenye hatari ya kuumia zaidi. Katika maisha, kuna wakati jambo moja ni lazima liharibike ili jipya lije. Kuna watu wanatakiwa kuondoka maishani mwako, ili wengine waingie. Hayo ni mapito, yanapita, na wewe utabaki ukiwa imara, na maisha yataendelea.

Mwisho kabisa, usijiwekee mpaka au ukuta wa kihisia au kimtazamo, wenye lengo la kukuzuia usisonge mbele kimaisha au kimahusiano. Jipe nafasi nyingine, pale utakapokuwa tayari kuingia kwenye uhusiano mpya. Binafsi, ninaamini, kwamba dunia hii ina watu wema na wazuri ambao wanafahamu nini maana ya upendo na jinsi ya kuuishi. Muombe Mungu, na siku moja atakukutanisha na mmoja wao, na kamwe hutokumbuka ulikotoka. Machozi yako yatageuka kuwa furaha, na amani itatawala moyoni mwako.

Ninaamini kabisa, unastahili kuwa na furaha. Nakutakia kila la heri, Mungu akupe furaha unayostahili kuipata maisha yako yote. Yaliyopita yamepita, ni saa ya kusonga mbele.

Asante, ninaamini kwa mchango huu, na michango ya wengine, utapata kitu cha kukusaidia.
 
Pole sana sana binti yangu, vijana wa siku hizi wanataka kula na kukimbia hawataki majukumu, kisha wanaamini kuwa kila mwanamke ana ladha nzuri Zaidi pas kujua kuwa bucha zote nyama ni ile ile tu. Hakuna kitu kizuri kama kuwa na mpenzi unayempenda aiseee, pole sana endelea na maisha. Uje PM

We mpiuuzi nawe mlaji tu
 
ahahaaa halafu unajua wadau wataanza kunishambulia kwa akili yako badili id bna
Mlinichanganya na id zenu!
Mimi mwenyewe nimepigwa kibuti bila hata sababu ya msingi au hata siijuw

Sababu inawezakana ipo
mfano umekua mnene kwa sasa,labda ulikua unampa mahaba mazuri sana na sasa umepunguza,au umekua na Maneno makali au dharau juu yake ,au inawezakana ukawa umepunguza usafi,kuna harufu unayoitoa inamkera,hizo hapo inawezakana kukawa na sababu pia jaribu kutafakari au yawezekana kuna ukweli haujauweka wazi hapa
 
Miss Natafuta,
Wewe wataka fairness tena kwenye mambo ya relatioship...haipogo hiyo always itakulaga kwa upande mmoja.
 
kimbia fasta aisee! nlishajifanyaga kuvumilia ligumegume linanuka vumbi, ana maneno yamatusi daily, yeye ndo perfect kila kitu anaponda yeye ndo mshika dini wengine shetani! hajielewi nkajua ni mapungufu yake tu kumbe yale yote ilikuwa ni maamuzi akaishia kama huyo
 
Migogoro ni kitu muhimu katika mapenzi, wakati mwengine anakuangalia utachukua hatua gani? Utaendelea kumpenda au utaona hana umuhimu, unahitajika kumuangalia ni mwanamke wa aina gani uliyekua naye, inawezekana anakuchallenge tu lakini pia wanawake ni watu wa kuchukua maamuzi yao, inawezekana pia kuna kitu amesikia kuhusu wewe na akaamua kukuacha
 
nahisi anakuwa kapata mwingine, na kwa sababu unakuwa hujamkosea, hawezi kukwambia sababu
 
Back
Top Bottom