Kuacha na kuachwa kwenye mapenzi limekuwa jambo la kujisifu

Meshacky Allyson

Senior Member
Oct 29, 2020
126
250
Habari wana JF, natumaini mu wazima wa afya. Binafsi nimekuwa nikitafakari sana jambo hili, nimekuwa nikisikiliza friend zangu walioko kwenye mahusiano na wapenzi wao, wakiongea kwa kujisifu kabisa sijui akizingua namwacha. Wadada nao siku hizi hivyo hivyo, kama sijui huna hela unaachwa. Yaani jambo la kuachana achana limekuwa kama sifa flani hivii.

Najiuliza ni kwamba ni utandawazi au nini shida unayofanya watu waone huu mchezo wa kuacha sijui kuachwa ni sifa flani hivi?

Uzi nawasilisha
Nipeni mwongozo juu ya jambo hili tupeane mawazo...
 
Ni majisifu ya mtu kujiona bora, hata kile atakachopewa ataona siyo bora na hakina hadhi

Jitunze mtunze, mthamini akuthamini, pendaneni, shirikianeni
 
Back
Top Bottom