Suluhisho la kuzima simu litatatua matatizo ya Watanzania na kutufikisha kwenye uchumi wa kati?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,493
2,000
Nimekuwa nikisikitishwa sana na mfumo unao tumiwa na Serikali hii ya awamu ya tano, katika kuwahudumia wananchi, katika ule msingi mkuu wa serikali,ni ustawi kwa wananchi wake.

Ukisoma Millennium Development Goals (MDGs) kama inavyo ainishwa hapo chini utaona nchi imekosa kuwa na taasisi imara, inategemea mawazo ya mtu mmoja akiamini ana akili kuliko wananchi zaidi ya milioni 50.

Tanzania Development Vision 2025 elucidates that Tanzania of 2025 should be a nation imbued with five
main attributes, namely, high quality livelihood; peace, stability and unity; good governance; a well-educated
and learning society; and a competitive economy capable of producing sustainable growth and shared benefits.

Maono ya maendeleo ya tanzania 2025 yanabainisha kuwa Tanzania ya 2025 inapaswa kuwa taifa lililojaa
sifa kuu kwenye mambo matano, ambayo ni, hali ya maisha kuwa nzuri; amani, utulivu na umoja; utawala bora; elimu bora na jamii ya kujifunzia; na uchumi wa ushindani wenye uwezo wa kukuza ukuaji endelevu na faida za pamoja.

Bila kuzingatia makubaliano ya mpango huu wa maendeleo, serikali kwa kukurupuka imeachana na mipango hiyo na kuhangaika kuzima line za wananchi wake kwa ajili ya kuzuia mawasiliano,kwa mikakati duni isiyo na maandalizi madhubuti.

Hapo ndipo ile dhana ya kufikia uchumi wa kati inapoonekana ni ndoto za mchana.

Imekuwa mara nyingi serikali zetu zikifanya maamuzi ya kizima moto bila tafiti za kina kwa mambo makubwa, kwa muachia mtu mmoja(rais) afikiri kwa niaba ya taifa, na kuifanya taasisi ya urais kuonekana dhaifu kwa kuwa imeacha mambo makubwa ya kitaifa kuamuliwa kwa utashi wa utu.

Kwanini nimeanza kuangalia malengo ya millennium,nikazungumzia na TCRA kwa maana ya wenye dhamana ya kufanya wayatakayo katika kuhakikisha line za simu zisizo sajiliwa kwa alama za vidole zitazimishwa.

Hii ni kwasababu tumewapa nguvu watu wachache kutekeleza utashi wa matakwa yao kwa kutumia dhamana tulizo wapa kwa maslahi ya taifa.

Matokeo yake ukikerwa na jambo kwa utashi wako unatumia nguvu kubwa ya kimamlaka tuliyolipa ili utekeleze, ndiyo maana kila kukicha utashi wa mtawala unakuwa na nguvu kuliko watawaliwa.

Huenda tunatekeleza mikakati ya millennium goals lakini ushirikishwaji wa wananchi ambao ndiyo wadau wa nchi hii wanashirikishwa!!!

Maamuzi magumu yanayo fanywa sasa yana baraka toka kwa wananchi!!!

Maana imekuwa desturi sasa mtu mmoja anaamua na kuweka ukomo wa maamuzi yake bila kuzingatia athari za kijamii,kiuchumi na kisayansi pia.

Hivi haya maendeleo tutayafikia kweli, ikiwa kila kivuli chenye dalili ya kukosoa kitashugulikiwa ipasavyo!!

Nasema hivi kutokana na maneno ya rais aliyowahi kuyasema anatamani sana kama mitandao ya kijamii ingezima angefurahi sana!!!

Unapokuwa na hamasa kama hiyo kisha ukaanza kudhibiti visababishi vya mitandao hiyo, huoni kuwa utashi binafsi unakuwa na nguvu kuliko wananchi walio kuweka usimamie matakwa yao!!!

Yaani serikali inaguswa na imepata sana maumivu kwenye line za simu kuliko katiba itakayo toa mwongozo utakaoendana na wakati tulionao!!!

Yaani mkakati wa dunia kufikia malengo ya millennium hayana nguvu kubwa japo yamewekewa utekelezaji wa maazimio kwa vipindi virefu visivyo vya kizimamoto, lakini hili la utashi wa mtu mmoja limefanyiwa utekelezaji wa haraka!!!

Kwa mwenendo huu wa kukurupuka bila kutazama athari zake kwanza tunairudisha nchi kwenye UJIMA.

Nini kifanyike,;

Kwa kuwa wadau wa line hizi ni wananchi, serikali iliapaswa kuwashirikisha kwa 100%,kwa kubainisha athari zake na faida zake.

Serikali itumie wataalamu wake kufanya tafiti za kina zenye malengo sawia kuliko kuzua mtanziko usio na tija kabla ya kutekeleza maazimio yake.

Serikali iache mara moja kuunganisha (link) matatizo ya sehemu mbili kuwa tatizo mmoja. Maanake nini;

Kuacha ubabaishaji wa maamuzi ya kizimamoto kwa kutafuta mchawi badala ya kutatua tatizo.

NIDA ina tatizo, suala la vitambulisho halikuanza leo toka awamu ya nne, utekelezaji wake umekuwa unasua sua, kuwaunganisha wananchi kwenye huduma yenye matatizo kwa kuwaongezea tatizo kisha ukatumia matatizo hayo kuwatupia wananchi lawama na maneno ya kejeli kama ya RC Makonda, ni kuwakosea wananchi.

Serikali iache mara moja kutafuta sifa kwa kutengeneza tatizo na kulitatua,hii inawafanya wananchi kukosa uaminifu na serikali yao.

Suala hili linahitaji muda zaidi ya huo mwaka mmoja tuliopewa,tuna implement kwa gharama za chini tukigetegemea matokeo chanya kwa muda mfupi, huko ni kuwahada wananchi.

Mwisho, Watanzania wana haki na nchi yao, tusiwaburuze ili kuwahofisha. Tuwe mifumo imara yenye tija kwa huduma za nchi na wananchi bila bugudha, kuzima kwa line kumeathiri watu wangapi kiuchumi na kijamii,tuamke maendeleo ni ushirikishwaji, mbona la mifuko ya plastic mlifanikiwa hii haraka ya kuzima line wakati hamjandaa mazingira wezeshi inatoka wapi!!!!
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
3,298
2,000
Kwa kweli lain lazima zizimwe hii itaforce watu kupata vitambulisho vya taifa mbali na hasara itakayojitokeza , zoezi hili haliwez fanikiwa kama et wataangalia hasara na hili ni zoez nyeti Sana Kwa mstakabal wa Taifa
 

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
2,419
2,000
Kwa kweli lain lazima zizimwe hii itaforce watu kupata vitambulisho vya taifa mbali na hasara itakayojitokeza , zoezi hili haliwez fanikiwa kama et wataangalia hasara na hili ni zoez nyeti Sana Kwa mstakabal wa Taifa
Unyeti wake uko wapi kwa mtu ambae hana simu, na wala haitaji passport?
 

t2t

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
329
500
Ndugu zangu wawili wamefungiwa laini zao za Airtel wakati wamesajili kwa Alama za vidole na wakihakiki wanaambiwa usajili wao umekamilika. TCRA tunaomba mtuambie hili linaweza vipi kutokea kama mamlaka inafanya kazi kwa ufanisi?
NOTE:Hii si habari ya kuhadithiwa, ninaishi nao hao ndugu zangu.
 

Avriel

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
3,773
2,000
sammosses, Buroo yaani umeongea jambo nimemaliza kulifanyia presentation sasa hivi hapa kuhusu Tanzania vision 2025 na millennium development goals, evaluation ya tunakoelekea na tulikotoka.

Tunahitaji alama toka mbinguni hii nchi tunachangamoto za kimaumbile na kiroho maana haiwezekani ikaendelea kuwa hivi despite of all natura endowed resources tumejaaliwa. Tumekosa leaders only.

We need signs to react on the same..


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
2,414
2,000
Japo kuna changamoto chache katika kutekeleza zoezi hili, haziwezi kuondoa umuhimu wa mchakato huu; hasa suala zima la usalama wa nchi na raia. Faida ni nyingi kuliko hasara, tutoeni ushirikiano. Sio kila kitu tunapinga.
 

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,493
2,000
Tatizo la vitambulisho vya NIDA ni sugu halina uhalisia japo bajeti ina tengwa kila mwaka, huenda kuna maslahi ya watu ndo maana ufanisi wake ni wa kikonokono zaidi.

Kuingiza usajili wa alama za vidole kupitia zoezi la vitambulisho hapo ndipo tatizo lilipoanzia.

Wangetofautisha mifumo ya usajili tukatumia vile vya mpiga kura isingekuwa taabu kama hii, wakaachana na mambo ya NIDA.

NIDA ingeshughulikiwa kipekee yake kuliko tatizo la NIDA ulifanye tatizo la usajili wa line
 

koyola

JF-Expert Member
May 20, 2015
2,384
2,000
Tatizo la vitambulisho vya NIDA ni sugu halina uhalisia japo bajeti ina tengwa kila mwaka, huenda kuna maslahi ya watu ndo maana ufanisi wake ni wa kikonokono zaidi.

Kuingiza usajili wa alama za vidole kupitia zoezi la vitambulisho hapo ndipo tatizo lilipoanzia.

Wangetofautisha mifumo ya usajili tukatumia vile vya mpiga kura isingekuwa taabu kama hii, wakaachana na mambo ya NIDA.

NIDA ingeshughulikiwa kipekee yake kuliko tatizo la NIDA ulifanye tatizo la usajili wa line
Ndg sammosse hili swala limefeli na litaendela kufeli kwa vigezo inavyohitajika na Nida, viongozi wengi wameangalia watu wa mijini na kuacha kuaangalia hali halisi ya watu wa vijijini, kimtazamo watu walozaliwa miaka ya 1970 hadi 1990 huko vijijini hawana vyeti vya kuzaliwa,wala hawana huduma za kisheria kuwathibitisha kuwa ni wazaliwa wa maeneo hayo vip leo uombe vyeti au uthibitisho wa kisheria kwa watu hao wa vijijini bila kuwasogezea hizo huduma, kwa maana hiyo hili zoezi bado ni mzigo mkubwa kulifanikisha vinginevyo waangalie utaratibu mapya, haya mambo kuona yanayofanyika mijini kwa kuwa wako karibu na huduma zote ulinganishe na vijijini ambapo huzifuta hizo huduma mijini kwa garama na huenda wasipate hata hicho walichofuta, kwamuangalizo swala litazamwe upya ili kufanikisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,493
2,000
Ndg sammosse hili swala limefeli na litaendela kufeli kwa vigezo inavyohitajika na Nida, viongozi wengi wameangalia watu wa mijini na kuacha kuaangalia hali halisi ya watu wa vijijini, kimtazamo watu walozaliwa miaka ya 1970 hadi 1990 huko vijijini hawana vyeti vya kuzaliwa,wala hawana huduma za kisheria kuwathibitisha kuwa ni wazaliwa wa maeneo hayo vip leo uombe vyeti au uthibitisho wa kisheria kwa watu hao wa vijijini bila kuwasogezea hizo huduma, kwa maana hiyo hili zoezi bado ni mzigo mkubwa kulifanikisha vinginevyo waangalie utaratibu mapya, haya mambo kuona yanayofanyika mijini kwa kuwa wako karibu na huduma zote ulinganishe na vijijini ambapo huzifuta hizo huduma mijini kwa garama na huenda wasipate hata hicho walichofuta, kwamuangalizo swala litazamwe upya ili kufanikisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Sahihi kaka, tuna kurupuka sana kila kukicha, mambo mengine ni ndoto yaani mtu anaota usiku mchana anatoa amri, namuona mfalme Nikabudreza ndani ya Tanzania Mpya ya wanyonge
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom