Kuacha kuongeza mshahara ni kosa kubwa

Kuacha kuongeza mshahara ni kosa kubwa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,208
Reaction score
16,871
Jamii huwa inapata fedha zao kwenye mzunguko kupitia wenzao wenye ajira, kwakuwa wao hawana njia yoyote ya kupata hela kutoka hazina moja kwa moja. Serikali inatoa fedha hazina kuwalipa watumishi, makandarasi na watoa huduma. Baada ya makundi haya kulipwa ndio wanazipeleka hela hizo kwa wananchi kwa kufanya manunuzi, kutoa michango Kama ya harusi na kuwatumia ndugu zao hela za matumizi na kuufanya mzunguuko wa hela uwepo kwenye jamii.

Ukubwa wa mzunguuko wa pesa unategemea pia ukubwa wa manunuzi ya waliopewa pesa hizo kutoka hazina, yaani wafanyakazi na ukubwa wa manunuzi utakaofanywa na wafanyakazi utategemea pia ukubwa wa malipo waliopewa kutoka hazina, yaani na mwajiri.

Idadi ya watu kwenye ngazi ya familia, mitaa, Kijiji, kata, wilaya, mkoa na taifa inayohitaji pesa huwa inaongezeka kila mwaka, Hivyo, usipowaongezea hela watumishi kwa miaka mitano maana yake watu wote wakioongezeka kwa kipindi hicho Cha miaka 5 watanyang'anya hela hiyo hiyo ya watu waliokuwepo miaka 5 iliyopita na kuufanya mzunguko wa hela uwe mdogo na maisha kuonekana kuwa magumu.

Ili mzunguko wa pesa uwe mzuri na maisha kuwa nafuu ni lazima yafuatayo yafanyike kila mwaka:

1. Ajira ziongezeke kila mwaka pia kama vile jamii inavyoongekeza pia.
2. Mishahara iongezwe kila mwaka pia Kama jamii inavyoongekeza pia.
3. Watoa huduma serikalini walipwe kwa wakati na waongezeke pia kila mwaka.
4. Juhudi za kuzuia uongezeko la watu lipewe kipaumbele.
6. Uzalishaji kwenye ngazi ya kata, Kijiji, kata, wilaya na taifa lazima uongezeke.
7. Masoko ya uhakika ya bidhaa lazima yawepo na yaongezeke.

Kama mambo haya yasipofanyika usije ukatafuta mchawi, maana mtoto anapolia njaa huwezi kumwambia subiri flyovers zinajengwa, mzazi anapokosa ada ya mtoto hawezi kusubiri ndege zinunuliwe kwanza. Gari yako inapokosa mafuta huwezi kusubiri barabara iishe. Na hii ndiyo maana kila mtumishi bila kuangalia anafanya kazi gani huwa anafurahia sherehe za May day kila mwaka ikiwa na matarajio kuwa huenda kutakuwa na nyongeza.

Kama ukiona mfanyakazi hata awe housegirl ambae hajalipwa au hajaongezewa mshahara anakuchekea ujuwe wazi kuwa anakudanganya.
 
Kuondoa FAO la kujitoa ni kosa kubwa.

Hasa Sekta binafsi, FAO la kujitoa ni haki na muhimu.

Watu wanafanya kazi kwa malengo, mkataba ikiisha alipwe Pesa yake yote na akajiajiri na kuajiri wengine.

Magufuli ulikosea sana na bado Magufuli husikilizi.

Jiwe anajiamini ataiba kura
 
Kuondoa FAO la kujitoa ni kosa kubwaa.

Hasa Sekta binafsi, FAO la kujitoa ni haki na muhimu...
Shida yetu tunawaandaa watoto wetu kwaajili ya kuajiriwa, ndio maana wakaondoa fao la kujitoa wakiamini kuwa ukiachishwa kazi ya kuajiriwa muda si mrefu utapata kazi ya kuajiriwa Tena.

Hawataki kuamini kuwa hizo hela zinaweza kugeuka mtaji Kama atapewa hela yake. Mbona 80% ya watu wamejiajiri wenyewe kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi?

Kwanini fao la kujitoa asipewe huyu mtumishi aliyekosa kazi aende akaungane mapema na wale wakulima, wafugaji, wavuvi na wafanya biashara ambao hawana NSSF lakini wanadunda?
 
Hela hazimwagwi tu katika uchumi bali zinategemea ukuaji wa uchumi husika . Kama ukuaji wa pesa katika mzunguko ni mkubwa kuliko ukuaji wa uchumi kutatokea ongezeko kubwa la bei za bidhaa na huduma hivyo ongezeko halitakuwa na faida yeyote kwa mfanyakazi na wananchi na utarudi hapa kulialia kuwa bei ziko juu. Pili thamani ya shilingi kulinganisha na Dola au Euro na pesa zingine za nje itashuka na kuchochea zaidi uporomokaji wa shilingi.

Tatu, hizo flyover, miundombinu na ndege unazoona hazifai kwa uelewa wako wa uchumi sio sahihi; kwani iujenzi wa miundombinu (public works) unachochea ongezeko la ajira na pesa mtaani hivyo kuongeza demand ya vitu mbalimbali na hivyo kufanya uzalishaji wa bidhaa na huduma uongezeke na kupelekea kipato mtaani kuongezeka.

Hayo unayoita naendeleo ya vitu kiuhalisia ndiyo maendeleo ya watu. Sasa hivi DSM tunakula matikiti yanayotoka Sumbawanga kwa sababu ya miundombinu ya barabara na masoko iliyojengwa hivyo kufanya pesa ya wanadsm kutiririka mpaka ndani kabisa remote area; kama barabara za kuunganisha mikoa na wilaya zisingejengwa mazao toka remote areas ya Tanzania yasingefika sokoni Dar au kuuzwa nchi za nje. Leo hii nyama inachinjwa Dodoma na kupelekwa uarabuni ni kwa sababu barabara, viwanja ya ndege vimejengwa hivyo kuchochea ukuaji wa demand ambao unapelekea ukuaji wa uzalishaji katika sekta husika moja kwa moja na pia indirectly katika sekta zingine zinazosapoti sekta husika mfano kama nyumba za wageni, baa za pombe, ukahaba, saluni za urembo, sekta za vifungashio, uchukuzi, dizeli na petroli nk.

Kama unalinganisha pesa za wizi na ufisadi zilizokuwa zinaibwa na wafanyakazi wa serikali na kuja kumwagwa mitaani kupitia matanuzi na maendeleo binafsi hizo kwa sasa hazipo na hazitarudi kamwe. Pesa hizo hizo sasa ndizo serikali inazielekeza katika ujenzi wa miundombinu, zahanati, hospitali, na huduma zingine za kijamii. Mambo ya misheni tawni hayataruhusiwa tena kwa sababu wizi unaumiza wengi na kufaidisha wachache. Hivyo kama ulikuwa unafaidika na mnyororo wa wizi, jipange katika shughuli halali iwe kujiajiri au kuajiriwa.

Tarehe 28 Oktoba tukampigie kura Magufuli na wabunge na madiwani wa CCM ili aendelee kuipaisha Tanzania. Kwa kasi yake nina hakika hadi kufikia 2025 tutakuwa tumeingia higher middle income country status.
 
Kuondoa FAO la kujitoa ni kosa kubwaa.

Hasa Sekta binafsi, FAO la kujitoa ni haki na muhimu.

Watu wanafanya kazi kwa malengo, mkataba ikiisha alipwe Pesa yake yote na akajiajiri na kuajiri wengine.

Magufuli ulikosea sana na bado Magufuli husikilizi.

Jiwe anajiamini ataiba kura
Point sn mkuu
 
Hela hazimwagwi tu katika uchumi bali zinategemea ukuaji wa uchumi husika . Kama ukuaji wa pesa katika mzunguko ni mkubwa kuliko ukuaji wa uchumi kutatokea ongezeko kubwa la bei za bidhaa na huduma hivyo ongezeko halitakuwa na faida yeyote kwa mfanyakazi na wananchi na utarudi hapa kulialia kuwa bei ziko juu. Pili thamani ya shilingi kulinganisha na Dola au Euro na pesa zingine za nje itashuka na kuchochea zaidi uporomokaji wa shilingi.

Tatu, hizo flyover, miundombinu na ndege unazoona hazifai kwa uelewa wako wa uchumi sio sahihi; kwani iujenzi wa miundombinu (public works) unachochea ongezeko la ajira na pesa mtaani hivyo kuongeza demand ya vitu mbalimbali na hivyo kufanya uzalishaji wa bidhaa na huduma uongezeke na kupelekea kipato mtaani kuongezeka.

Hayo unayoita naendeleo ya vitu kiuhalisia ndiyo maendeleo ya watu. Sasa hivi DSM tunakula matikiti yanayotoka Sumbawanga kwa sababu ya miundombinu ya barabara na masoko iliyojengwa hivyo kufanya pesa ya wanadsm kutiririka mpaka ndani kabisa remote area; kama barabara za kuunganisha mikoa na wilaya zisingejengwa mazao toka remote areas ya Tanzania yasingefika sokoni Dar au kuuzwa nchi za nje. Leo hii nyama inachinjwa Dodoma na kupelekwa uarabuni ni kwa sababu barabara, viwanja ya ndege vimejengwa hivyo kuchochea ukuaji wa demand ambao unapelekea ukuaji wa uzalishaji katika sekta husika moja kwa moja na pia indirectly katika sekta zingine zinazosapoti sekta husika mfano kama nyumba za wageni, baa za pombe, ukahaba, saluni za urembo, sekta za vifungashio, uchukuzi, dizeli na petroli nk.

Kama unalinganisha pesa za wizi na ufisadi zilizokuwa zinaibwa na wafanyakazi wa serikali na kuja kumwagwa mitaani kupitia matanuzi na maendeleo binafsi hizo kwa sasa hazipo na hazitarudi kamwe. Pesa hizo hizo sasa ndizo serikali inazielekeza katika ujenzi wa miundombinu, zahanati, hospitali, na huduma zingine za kijamii. Mambo ya misheni tawni hayataruhusiwa tena kwa sababu wizi unaumiza wengi na kufaidisha wachache. Hivyo kama ulikuwa unafaidika na mnyororo wa wizi, jipange katika shughuli halali iwe kujiajiri au kuajiriwa.

Tarehe 28 Oktoba tukampigie kura Magufuli na wabunge na madiwani wa CCM ili aendelee kuipaisha Tanzania. Kwa kasi yake nina hakika hadi kufikia 2025 tutakuwa tumeingia higher middle income country status.
Hakuna anayesema flyovers na reli sio muhimu, anayesema hivyo hajijui, lakini hakuna anaepaswa kuacha kulipa Karo za watoto leo ili ajenge nyumba tatu za biashara itakayoleta faida miaka 20 pale utakapozeeka na kupungua kipato. Wewe unadhani Ni kwanini hata baba wa taifa mwenyewe alishindwa kuhamishia Dodoma serikali yake? Maendeleo ya watu lazima yatangulie maendeleo ya vitu.

Tunapenda muuguzi leo atabasabu mbele ya mgonjwa Kama sehemu ya tiba, je, asubiri flyovers ziishe ndipo apandishwe daraja lake?
 
Hawaongezi mshahara lakini wameweka riba ya 6% kwenye makato ya bodi ya mikopo kila mwaka wao wanaita retention fee. Ukiwauliza hiyo riba ya nini, wanakwambia hiyo ni muhimu kwa sababu fedha inashuka thamani kila mwaka, kwamba hiyo sh 100 uliyokopa mwaka juzi siyo sawa na sh 100 ya leo.

Ukiwaambia kuwa kama hivyo ndivyo kwa nini basi hamuongezi mishahara kila mwaka ili kulinda thamani ya mshahara husika kutokana na gharama za maisha kupanda na pesa kushuka thamani?, Hawana majibu ya kueleweka!
 
Mwaka 2015 Chadema iliibiwa kura nyingi.

Kuna uwezekano mawakala wa Chadema waliuza mechi

Nashangaa bado kwa Nini 2015 Chadema haikupata wabunge wengi

Tusibweteke na nyomi
 
Jamii huwa inapata fedha zao kwenye mzunguko kupitia wenzao wenye ajira, kwakuwa wao hawana njia yoyote ya kupata hela kutoka hazina moja kwa moja. Serikali inatoa fedha hazina kuwalipa watumishi, makandarasi na watoa huduma. Baada ya makundi haya kulipwa ndio wanazipeleka hela hizo kwa wananchi kwa kufanya manunuzi, kutoa michango Kama ya harusi na kuwatumia ndugu zao hela za matumizi na kuufanya mzunguuko wa hela uwepo kwenye jamii.

Ukubwa wa mzunguuko wa pesa unategemea pia ukubwa wa manunuzi ya waliopewa pesa hizo kutoka hazina, yaani wafanyakazi na ukubwa wa manunuzi utakaofanywa na wafanyakazi utategemea pia ukubwa wa malipo waliopewa kutoka hazina, yaani na mwajiri.

Idadi ya watu kwenye ngazi ya familia, mitaa, Kijiji, kata, wilaya, mkoa na taifa inayohitaji pesa huwa inaongezeka kila mwaka, Hivyo, usipowaongezea hela watumishi kwa miaka mitano maana yake watu wote wakioongezeka kwa kipindi hicho Cha miaka 5 watanyang'anya hela hiyo hiyo ya watu waliokuwepo miaka 5 iliyopita na kuufanya mzunguko wa hela uwe mdogo na maisha kuonekana kuwa magumu.

Ili mzunguko wa pesa uwe mzuri na maisha kuwa nafuu ni lazima yafuatayo yafanyike kila mwaka:

1. Ajira ziongezeke kila mwaka pia kama vile jamii inavyoongekeza pia.
2. Mishahara iongezwe kila mwaka pia Kama jamii inavyoongekeza pia.
3. Watoa huduma serikalini walipwe kwa wakati na waongezeke pia kila mwaka.
4. Juhudi za kuzuia uongezeko la watu lipewe kipaumbele.
6. Uzalishaji kwenye ngazi ya kata, Kijiji, kata, wilaya na taifa lazima uongezeke.
7. Masoko ya uhakika ya bidhaa lazima yawepo na yaongezeke.

Kama mambo haya yasipofanyika usije ukatafuta mchawi, maana mtoto anapolia njaa huwezi kumwambia subiri flyovers zinajengwa, mzazi anapokosa ada ya mtoto hawezi kusubiri ndege zinunuliwe kwanza. Gari yako inapokosa mafuta huwezi kusubiri barabara iishe. Na hii ndiyo maana kila mtumishi bila kuangalia anafanya kazi gani huwa anafurahia sherehe za May day kila mwaka ikiwa na matarajio kuwa huenda kutakuwa na nyongeza.

Kama ukiona mfanyakazi hata awe housegirl ambae hajalipwa au hajaongezewa mshahara anakuchekea ujuwe wazi kuwa anakudanganya.
Wakati mnaongezwa mishahara sisi wa vijijini tusioajiriwa na serikali tunaongezwa nini!?

Kukaa karibu na waridi mnaanza kunukia... Kudhani nyie tu ndio muhimu.. muongezwe mishahara..

Sisi huku kijijini tunataka dawa, barabara, huduma za elimu na masoko. Hatujawahi kuongezwa mishahara tangu uhuru.. nyie kunyimwa miaka hii michache imekuwa nongwa!?

Plus ni sisi ambao huwa hatuongezwi kitu tinaichangia serikali hiyo hiyo ili iwaongeze mishahara... This has been blown out of proportions...

Kama hali ni hivi kweli iko siku watanzania watajitolea kufanya kazi bila malipo? (Volunteering)

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Daa! Kaka hebu fanya utafiti mdogo Kati ya Kijiji ambacho kina shule ya msingi na sekondari, zahanati, na kituo Cha polisi na Kijiji ambacho hakina vitu hivyo kwenye mzunguuko wa fedha. Kijiji chenye watu walioajiriwa wengi hata wakulima wananufaika kwa kuuza mazao yao ya shambani na mifugo, nyumba za kupangisha na hata biashara zinapata wanunuzi kwa wingi kuliko Kijiji ambacho hakina watumishi. Baada ya watumishi kulipwa mwisho wa mwezi au kupata mikopo ya benk hufanya matumizi ambayo hata wasioajiriwa wananufaika na mishahara hiyo kwa njia moja au nyingine.
Walioajiriwa wakipata mshahara wanawatumia wazazi wao kijijini, wanalimiwa, wanajenga, wananunua nyama, wanahonga, nk
 
Hela hazimwagwi tu katika uchumi bali zinategemea ukuaji wa uchumi husika . Kama ukuaji wa pesa katika mzunguko ni mkubwa kuliko ukuaji wa uchumi kutatokea ongezeko kubwa la bei za bidhaa na huduma hivyo ongezeko halitakuwa na faida yeyote kwa mfanyakazi na wananchi na utarudi hapa kulialia kuwa bei ziko juu. Pili thamani ya shilingi kulinganisha na Dola au Euro na pesa zingine za nje itashuka na kuchochea zaidi uporomokaji wa shilingi.

Tatu, hizo flyover, miundombinu na ndege unazoona hazifai kwa uelewa wako wa uchumi sio sahihi; kwani iujenzi wa miundombinu (public works) unachochea ongezeko la ajira na pesa mtaani hivyo kuongeza demand ya vitu mbalimbali na hivyo kufanya uzalishaji wa bidhaa na huduma uongezeke na kupelekea kipato mtaani kuongezeka.

Hayo unayoita naendeleo ya vitu kiuhalisia ndiyo maendeleo ya watu. Sasa hivi DSM tunakula matikiti yanayotoka Sumbawanga kwa sababu ya miundombinu ya barabara na masoko iliyojengwa hivyo kufanya pesa ya wanadsm kutiririka mpaka ndani kabisa remote area; kama barabara za kuunganisha mikoa na wilaya zisingejengwa mazao toka remote areas ya Tanzania yasingefika sokoni Dar au kuuzwa nchi za nje. Leo hii nyama inachinjwa Dodoma na kupelekwa uarabuni ni kwa sababu barabara, viwanja ya ndege vimejengwa hivyo kuchochea ukuaji wa demand ambao unapelekea ukuaji wa uzalishaji katika sekta husika moja kwa moja na pia indirectly katika sekta zingine zinazosapoti sekta husika mfano kama nyumba za wageni, baa za pombe, ukahaba, saluni za urembo, sekta za vifungashio, uchukuzi, dizeli na petroli nk.

Kama unalinganisha pesa za wizi na ufisadi zilizokuwa zinaibwa na wafanyakazi wa serikali na kuja kumwagwa mitaani kupitia matanuzi na maendeleo binafsi hizo kwa sasa hazipo na hazitarudi kamwe. Pesa hizo hizo sasa ndizo serikali inazielekeza katika ujenzi wa miundombinu, zahanati, hospitali, na huduma zingine za kijamii. Mambo ya misheni tawni hayataruhusiwa tena kwa sababu wizi unaumiza wengi na kufaidisha wachache. Hivyo kama ulikuwa unafaidika na mnyororo wa wizi, jipange katika shughuli halali iwe kujiajiri au kuajiriwa.

Tarehe 28 Oktoba tukampigie kura Magufuli na wabunge na madiwani wa CCM ili aendelee kuipaisha Tanzania. Kwa kasi yake nina hakika hadi kufikia 2025 tutakuwa tumeingia higher middle income country status.
Ubinafsi tu umekujaa. Huna lolote. Mtoa mada kaongelea Watumishi wa umma kutopandishiwa mishahara na pia madaraja yao kwa miaka zaidi ya mitano sasa kinyume na utaratibu!

Wewe unawaza kula tu matikiti. Hovyo kabisa. Na nakuhakikishia huyo mgombea wako asingetegemea nguvu ya polisi na tume kumbeba, mwaka huu angeangukia pua.

Na hayupo Mtumishi wa umma mwenye akili timamu! Awe ccm, chadema au hata asiye na chama kama mimi atakua na ujasiri wa kumchagua mtu kama magufuli asiye na msaada wowote kwake.

Bora hata nimpigie kura Hashimu Rungwe aliyeahidi kugawa ubwabwa! Kuliko mtu anayedhani kujenga flyovers na kununua ndege ndiyo maendeleo! Huku akiwadhulimu wafanyakazi haki zao za msingi.
 
Wakati mnaongezwa mishahara sisi wa vijijini tusioajiriwa na serikali tunaongezwa nini!?

Kukaa karibu na waridi mnaanza kunukia... Kudhani nyie tu ndio muhimu.. muongezwe mishahara..

Sisi huku kijijini tunataka dawa, barabara, huduma za elimu na masoko. Hatujawahi kuongezwa mishahara tangu uhuru.. nyie kunyimwa miaka hii michache imekuwa nongwa!?

Plus ni sisi ambao huwa hatuongezwi kitu tinaichangia serikali hiyo hiyo ili iwaongeze mishahara... This has been blown out of proportions...

Kama hali ni hivi kweli iko siku watanzania watajitolea kufanya kazi bila malipo? (Volunteering)

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Unazijua taratibu za kazi au unalalamika tu na kuwaonea wivu walioajiriwa? Kuna mtu alikuzuia na wewe kuajiriwa? Halafu aliyekuambia huo mchango wako ndiyo unaomlipa mfanyakazi ni nani?

Na unachangia kodi kiasi gani walau kwa mwezi tu? Au ndiyo kile kitambulisho ulichopewa na magufuli na kukilipia kwa elfu 20 kwa mwaka? Unaifahamu kodi wanayolipishwa wafanyakazi kila mwezi kulingana na madaraja yao ya kiutumishi?
 
Hawaongezi mshahara lakini wameweka riba ya 6% kwenye makato ya bodi ya mikopo kila mwaka wao wanaita retention fee. Ukiwauliza hiyo riba ya nini, wanakwambia hiyo ni muhimu kwa sababu fedha inashuka thamani kila mwaka, kwamba hiyo sh 100 uliyokopa mwaka juzi siyo sawa na sh 100 ya leo.

Ukiwaambia kuwa kama hivyo ndivyo kwa nini basi hamuongezi mishahara kila mwaka ili kulinda thamani ya mshahara husika kutokana na gharama za maisha kupanda na pesa kushuka thamani?, Hawana majibu ya kueleweka!
Hawa watu wamejawa tu na ubinafsi. Hawana lolote. Wao na familia zao maisha yao yanazidi tu kuneemeka! Na ndiyo maana leo hii wamejaza mabango na mapicha yao nchi nzima! Ila kujali maisha ya wengine, hawako tayari.

Halafu eti wanataka wachaguliwe. Labda na hao wanyonge wao. Ila mimi na akili zangu timamu, siwezi kumchagua asiye na faida kwangu! Ili aniumize zaidi? Big NO.
 
Hakuna anayesema flyovers na reli sio muhimu, anayesema hivyo hajijui, lakini hakuna anaepaswa kuacha kulipa Karo za watoto leo ili ajenge nyumba tatu za biashara itakayoleta faida miaka 20 pale utakapozeeka na kupungua kipato. Wewe unadhani Ni kwanini hata baba wa taifa mwenyewe alishindwa kuhamishia Dodoma serikali yake? Maendeleo ya watu lazima yatangulie maendeleo ya vitu.

Tunapenda muuguzi leo atabasabu mbele ya mgonjwa Kama sehemu ya tiba, je, asubiri flyovers ziishe ndipo apandishwe daraja lake?
Well said
 
Ubinafsi tu umekujaa. Huna lolote. Mtoa mada kaongelea Watumishi wa umma kutopandishiwa mishahara na pia madaraja yao kwa miaka zaidi ya mitano sasa kinyume na utaratibu!

Wewe unawaza kula tu matikiti. Hovyo kabisa. Na nakuhakikishia huyo mgombea wako asingetegemea nguvu ya polisi na tume kumbeba, mwaka huu angeangukia pua.

Na hayupo Mtumishi wa umma mwenye akili timamu! Awe ccm, chadema au hata asiye na chama kama mimi atakua na ujasiri wa kumchagua mtu kama magufuli asiye na msaada wowote kwake.

Bora hata nimpigie kura Hashimu Rungwe aliyeahidi kugawa ubwabwa! Kuliko mtu anayedhani kujenga flyovers na kununua ndege ndiyo maendeleo! Huku akiwadhulimu wafanyakazi haki zao za msingi.

Ubinafsi tu umekujaa. Huna lolote. Mtoa mada kaongelea Watumishi wa umma kutopandishiwa mishahara na pia madaraja yao kwa miaka zaidi ya mitano sasa kinyume na utaratibu!

Wewe unawaza kula tu matikiti. Hovyo kabisa. Na nakuhakikishia huyo mgombea wako asingetegemea nguvu ya polisi na tume kumbeba, mwaka huu angeangukia pua.

Na hayupo Mtumishi wa umma mwenye akili timamu! Awe ccm, chadema au hata asiye na chama kama mimi atakua na ujasiri wa kumchagua mtu kama magufuli asiye na msaada wowote kwake.

Bora hata nimpigie kura Hashimu Rungwe aliyeahidi kugawa ubwabwa! Kuliko mtu anayedhani kujenga flyovers na kununua ndege ndiyo maendeleo! Huku akiwadhulimu wafanyakazi haki zao za msingi.
Watumishi wengi tu wa umma ttutamchagua Magufuli; labda wale wezi wa fedha za umma ambao wamebanwa ndio hawatamchagua.

Wewe kwanza nina mashaka kama ni mtumishi, mtumishi gani anapinga ujenzi wa barabara? Yaani faida za barabara huzioni hata hilo la kuwahi kwenda na kurudi nyumbani kwa sababu ya flyoover na barabara kuwa zimejengwa hivyo kupunguza foleni.
 
Aisee!! Yaani nikiwa kama mfanyakazi badala ya kudai nyongeza ya mshahara, kupandishwa daraja kwa wakati, mazingira bora ya kufanyia kazi, kurudishwa fao la kujitoa,kulipwa pensheni kwa wakati, nk. Nipiganie ujenzi wa barabara!!

Hilo ni jukumu la serikali yoyote ile iliyopo madarakani. Mfanyakazi analipa kodi kila mwezi, mfanyabiashara naye analipa kodi hiyo hiyo kwa utaratibu aliowekeana na serikali! Mkulima naye analipa kodi baada ya kuuza mazao yake!

Kodi hiyo ndiyo inayotakiwa sasa kuendeshea serikali iliyopo madarakani, pamoja na kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo hizo barabara! Hili somo umfikishie MZEE! Sawa? By the way, foleni iko nchi nzima au ni huko Dar tu mnakong'ang'ania wote kuishi?
 
Back
Top Bottom