Kuacha kazi ya ualimu kusomea kodi

Kuacha kazi ya ualimu kusomea kodi

makenze

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
356
Reaction score
217
habarini Ndugu zangu,kiukweli ninalitoa hili kutoka moyoni.mshahara haukutani mwisho wa mwezi japo nina degree ya ualimu wa sayansi ila hela ni ndogo.
sikufuru kuna wengi hawana kazi kwa sasa ila nawaambieni ualimu wanavyosema ni wito wanamaanisha usitegemee kupata pesa ya kufanya lolote.nimejitahidi kukusanya masalia ya mshahara ili nipate walau ela ya mtaji wa kufanya biashara yoyote ila haukusanyiki aisee.
nimewaza mengi ila kubwa nimeona kupata mtaji kwa sasa ni mtihani mzito.
nimeona ni chepuke kodogo japo nikasomee mambo ya kodi japo cheti tu kwanza.nicheki na ajira upande huo wandugu
Naomba Godfather pande hizo wakuu such as mentor and something like that.
msaada wakuu mawazo na hitaji hilo hapo juu
 
Wewe unataka pesa yanini kuzungukazunguka usiende direct kwenye taaluma ya kudeal na hizo pesa. Kama wewe ni mwalimu wa sayansi lazima hesabu zitakuwa sio mama mkwe kwako hivyo soma uhasibu professional ambayo haijawahi kumwangusha mtu smart.
 
Mkuu, Kuacha kazi kunahitaji moyo sana. Pia inahitaji uwe na hakika ya 10000% ya kitu kipya ambacho unahitaji kufanya.

Nashukuru ume declare kwamba kazi zimekuwa ngumu sana na pesa hakuna. Ni vema kama umelitambua hilo mapema.

So kabla hujaacha kazi weka Options zako kwenye mizani ili usije jutia maamuzi.

Kama kuna fursa umeiona kwenye TAX na unaweza itoa sadaka ajira yako kwa manufaa makubwa ya mbeleni basi nakuunga mkono.

Ila uwe tayari kupokea mabadiliko yoyote yatakayo jitokeza
 
Mkuu kwanza pole kwa majukumu ya kitaifa yabkutuondolea ujinga watoto wetu .. Kuna msemo huku mtaani Upo unasema hivi USIACHE KAZ BILA KUPATA KAZ NYINGINE.. Nasema hivi mm nikiwa muhanga wa uamuz ambao unataka kuufanya wewe mkuu .. Binafs nilikuwa mwalimu mkoa fulan baada ya miaka 2 nkaona mambo hayaend nikimaanisha salary nilikuwa ndogo hvyo bas nkaamua kuacha ualimu nkaenda kusoma koz za mifugo upande wa maabara I mean veterinary laboratory technology kwa wakat huo uhitaj ulikuwa mkubwa sana kabla ya mzee baba mh Maguful hajaingia madarakan niliowakuta chuoni walikuwa wanaajiriwa mwaka wa mwisho miez 2 kabla ya kumaliza masomo bahat mbaya kwangu jamaa anaingia madarakani akasitisha ajira na ndio mwaka wa mwisho mm namaliza hebu fikiria n magumu kias gan nimepitia kwa wakat huo Huu nimekupa tu mfano halisi wa mm kwa maamuz Yangu niliyochukua kipind hicho japo kwa sasa nimejiajir kupitia fani Yangu ila kiukwel hali n tete na unapo Fanya maamuz chief angalia faida na hasara kwa ushaur zaid waweza kunipm nikakupa msaada wa kimawazo zaidi
 
Ila usiache kazi, kwa maana ajira zenyewe siku hizi hazieleweki.
Unaweza kuhamia kwenye kusoma kodi, ukaishia mtaani.

Viginevyo, nakushauri kusomea ujasiriamali.
 
UMEFANYA TAFITI YA ENEO UNALOTAKA KUSOMA? UMEANGALI AKIDOGO MITANDAO YA VYUO WANAOFUNDISHA KODI AKUANGALIA NI ASILIMIA NGAPI YA WANACHUO AMBAO WANAMALIZA NA AJIRA ZAO KWA KADA HIYO? NADHANI KWA HAPO UTAJUA NINI CHA KUPANGA NA NINI CHA KUCHAGUA.

USHAURI WANGU KWAKO KWA MASOMO YA KODI NI TAASISI CHACHE SANA AMBAZO ZINA UHITAJI WA WATAALAMU WA HII KADA ILA UNAWEZA UKAANZA KUSOMA KADA AMBAYO HATA OFISI IKIWA NA WATU WATANO BASI NAWE NI MMOJAWAPO KAMA UHASIBU, PROCUREMENT NA HATA MARKETING PIA SIO MBAYA SANA KWA WAKATI HUU KWANI UNAWEZA UKAFANYA JAPO ONLINE MARKETING MAISHA YAKAENDA ILA KWA KODI HAPANA SIKUSHAURI LABDA KAMA UNA MCHONGO TRA AMBAO UNA UHAKIKA 100% UTAFANIKIWA . UTAKUJA JUTA TENA KWA MARA YA PILI KAMA AMBAVYO UNAICHUKIA HIYO DEGREE YAKO YA UALIMU KWA SASA

FANYIA KAZI HUU UPEMBUZI YAKINIFU KISHA CHUKUA YALE YALOYO MAZURI KWAKO
 
habarini Ndugu zangu,kiukweli ninalitoa hili kutoka moyoni.mshahara haukutani mwisho wa mwezi japo nina degree ya ualimu wa sayansi ila hela ni ndogo.
sikufuru kuna wengi hawana kazi kwa sasa ila nawaambieni ualimu wanavyosema ni wito wanamaanisha usitegemee kupata pesa ya kufanya lolote.nimejitahidi kukusanya masalia ya mshahara ili nipate walau ela ya mtaji wa kufanya biashara yoyote ila haukusanyiki aisee.
nimewaza mengi ila kubwa nimeona kupata mtaji kwa sasa ni mtihani mzito.
nimeona ni chepuke kodogo japo nikasomee mambo ya kodi japo cheti tu kwanza.nicheki na ajira upande huo wandugu
Naomba Godfather pande hizo wakuu such as mentor and something like that.
msaada wakuu mawazo na hitaji hilo hapo juu
Mwalimu, nakushauli ubaki hapo kwanza mpaka uwe na uhakika sehemu unayoenda , cheti cha kodi hakita kusaidia kwa maana ya mshahara! Hata kupata ajira ni ïssue! Anza kufuga au kilimo cha busitani.
 
Ww nenda kasome kitu unachokipenda tu ila usiache kazi ukirudi endelea na ualimu huwa nafasi zinatoka walimu wanapandishwa vyeo ,Mm nimesoma na na walimu ila sasa wameajiriwa kwenye professional zingine kabisa (walipandishwa vyeo)
 
Degree ya science unakosa vichwa vya mitahani kujiongezea kipato??? Hii likizo nina vichwa mpaka nashindwa kuviatend vyote.maths and science sio mtu wa kulia lia shida za elfu 20 au 30.
Elfu 30 unaipata kwa kichwa kimoja tu kwa saa 1 pande za kinondoni wakati elfu 50 ni kichwa kimoja tu masaki then unarud zako mtaani bila pressure
 
Ni rahis kusema hivyo mkuu si wote wameajiliwa DSM wengne wapo nanjilinji huko shule nzima ina wanafunz 90 na mwamko wa elimu hakuna mwanafunz wa kijjn umwambie akupe 20k kwa ajil ya tuition n ngumu kwa hapa DSM n sawa hilo linawezekana sometimes mazingira pia yanachangia nasema hivi sababu mm n muhanga wa haya tena n MWL wa sayans
 
UMEFANYA TAFITI YA ENEO UNALOTAKA KUSOMA? UMEANGALI AKIDOGO MITANDAO YA VYUO WANAOFUNDISHA KODI AKUANGALIA NI ASILIMIA NGAPI YA WANACHUO AMBAO WANAMALIZA NA AJIRA ZAO KWA KADA HIYO? NADHANI KWA HAPO UTAJUA NINI CHA KUPANGA NA NINI CHA KUCHAGUA.

USHAURI WANGU KWAKO KWA MASOMO YA KODI NI TAASISI CHACHE SANA AMBAZO ZINA UHITAJI WA WATAALAMU WA HII KADA ILA UNAWEZA UKAANZA KUSOMA KADA AMBAYO HATA OFISI IKIWA NA WATU WATANO BASI NAWE NI MMOJAWAPO KAMA UHASIBU, PROCUREMENT NA HATA MARKETING PIA SIO MBAYA SANA KWA WAKATI HUU KWANI UNAWEZA UKAFANYA JAPO ONLINE MARKETING MAISHA YAKAENDA ILA KWA KODI HAPANA SIKUSHAURI LABDA KAMA UNA MCHONGO TRA AMBAO UNA UHAKIKA 100% UTAFANIKIWA . UTAKUJA JUTA TENA KWA MARA YA PILI KAMA AMBAVYO UNAICHUKIA HIYO DEGREE YAKO YA UALIMU KWA SASA

FANYIA KAZI HUU UPEMBUZI YAKINIFU KISHA CHUKUA YALE YALOYO MAZURI KWAKO
Aiseee haya maherufi makubwa yanasumbua kusoma. Tumia herufi ndogo
 
Hakuna ajira ya serikali ambayo mshahara hukutana,Hapo usische kazi jiongeze kitaaa.Nipm nikupe michapo tunafanyaje kumake life kitaa huku ukiwa mtumishi wa umma!
 
tuanzie hapa ndugu , kwani take home unapokea bei gan
 
weka mambo hadharani, huko pm usije kumgeuza mwenzio fursa
Nataka kumfundisha kuwa awe mwizi wa muda wa serikali afanye mambo yake ataenjoy sana,Wewe kopa hadi mwisho kwa wewe mwl wa degree kopa crdb 11 mil kwa miaka 7, Then jichanganye kitaaa kazini unaenda siku 2 kwa wiki kazini hata wakikusepesha unatambaaa kiulaini.Hata ungeenda kusoma utapoteza muda bure!!
 
habarini Ndugu zangu,kiukweli ninalitoa hili kutoka moyoni.mshahara haukutani mwisho wa mwezi japo nina degree ya ualimu wa sayansi ila hela ni ndogo.
sikufuru kuna wengi hawana kazi kwa sasa ila nawaambieni ualimu wanavyosema ni wito wanamaanisha usitegemee kupata pesa ya kufanya lolote.nimejitahidi kukusanya masalia ya mshahara ili nipate walau ela ya mtaji wa kufanya biashara yoyote ila haukusanyiki aisee.
nimewaza mengi ila kubwa nimeona kupata mtaji kwa sasa ni mtihani mzito.
nimeona ni chepuke kodogo japo nikasomee mambo ya kodi japo cheti tu kwanza.nicheki na ajira upande huo wandugu
Naomba Godfather pande hizo wakuu such as mentor and something like that.
msaada wakuu mawazo na hitaji hilo hapo juu
Kama ni bsc phy& math. Jiongeze katika tecnical skill au engineering UDSM kuna post graduate ktk engineering, civil, mechanics, electronics İT nk. Hizi fani wewe mwrnyewe ni ofisi tofauti na kodi lazima uajiliwe ili uishi.Kwa mfano ukisoma civil huta kosa kazi hata za chini kabisa.Jambo lingine ni ufundi wa kawaida. Jifunze kufanya repair and mantainance ya vitu vifuatavyo
1.Smart phone (Hardware and software )
2.Computer maintainance (Hardware and soft ware) baadhi ya mambo umeishayasoma ktk digital & analogue circuits.Hapa unahitaji practical tu.
3.Office machinery ie.photocopy, printer nk
4.Fridge
5.car electrification( kumbuka magari yanaongezeka kila kukicha tena sminapesa
) ambayo hayahitaji wababsishaji!
6.Air condition hii principle ipo sawa na fridge na baadhi ya mambo umeisha yasoma kwenye thermodynamics
7 .Home decoration.Hii fani sijui inapotolewa ila kuna jamaa zangu(La 7) Walikuw wakifanya sijui hata walikojifunza ila inapesa

Kuwa multipurpose .
Kuwa focused.
İvue degree na ujivae wew mwenyewe.
Shirikiana na watu wa maeneo ulipo, watakufungua zaidi.
Mwisho soma kidogo kuhusu ujasiliamali bsc huwa hwafundishwi hiyo kozi na ndio maana huelewi kuwa degree ya bsc ni tofauti na nyingine .
 
Mkuu kwanza pole kwa majukumu ya kitaifa yabkutuondolea ujinga watoto wetu .. Kuna msemo huku mtaani Upo unasema hivi USIACHE KAZ BILA KUPATA KAZ NYINGINE.. Nasema hivi mm nikiwa muhanga wa uamuz ambao unataka kuufanya wewe mkuu .. Binafs nilikuwa mwalimu mkoa fulan baada ya miaka 2 nkaona mambo hayaend nikimaanisha salary nilikuwa ndogo hvyo bas nkaamua kuacha ualimu nkaenda kusoma koz za mifugo upande wa maabara I mean veterinary laboratory technology kwa wakat huo uhitaj ulikuwa mkubwa sana kabla ya mzee baba mh Maguful hajaingia madarakan niliowakuta chuoni walikuwa wanaajiriwa mwaka wa mwisho miez 2 kabla ya kumaliza masomo bahat mbaya kwangu jamaa anaingia madarakani akasitisha ajira na ndio mwaka wa mwisho mm namaliza hebu fikiria n magumu kias gan nimepitia kwa wakat huo Huu nimekupa tu mfano halisi wa mm kwa maamuz Yangu niliyochukua kipind hicho japo kwa sasa nimejiajir kupitia fani Yangu ila kiukwel hali n tete na unapo Fanya maamuz chief angalia faida na hasara kwa ushaur zaid waweza kunipm nikakupa msaada wa kimawazo zaidi
pole mkuu.ila zikufichi hamna kitu kabisa.ni upate ela ya ugali mpaka tarehe 15.uanze kukopa tena kwa mangi.uje mshahara ulipe na mzunguko wa madeni uendelee
 
Wewe unataka pesa yanini kuzungukazunguka usiende direct kwenye taaluma ya kudeal na hizo pesa. Kama wewe ni mwalimu wa sayansi lazima hesabu zitakuwa sio mama mkwe kwako hivyo soma uhasibu professional ambayo haijawahi kumwangusha mtu smart.
uhasibu?
mkuu sijawahi kuliwaza hilo nikupm kwa mawazo zaidi?
 
Mkuu, Kuacha kazi kunahitaji moyo sana. Pia inahitaji uwe na hakika ya 10000% ya kitu kipya ambacho unahitaji kufanya.

Nashukuru ume declare kwamba kazi zimekuwa ngumu sana na pesa hakuna. Ni vema kama umelitambua hilo mapema.

So kabla hujaacha kazi weka Options zako kwenye mizani ili usije jutia maamuzi.

Kama kuna fursa umeiona kwenye TAX na unaweza itoa sadaka ajira yako kwa manufaa makubwa ya mbeleni basi nakuunga mkono.

Ila uwe tayari kupokea mabadiliko yoyote yatakayo jitokeza
mkuu sijaona fursa direct ila kwa sasa mambo yalivyo naona ukiwa na ujuzi wa kodi unaweza kupata ajira nzuri
ndo maana nikaomba Muongozo zaidi mkuu
 
Back
Top Bottom