Ku-copy na ku-paste style za member wa JF

Ahsante mkuu, inauma sana hiyo Ukizingatia unandika kwa ghalama zako mwenyewe na hutrgemei kupata hata senti 1 in return. Tunachoingiza ni furaha unayopata baada ya mtu kupenda andiko lako kwa kujifunza kitu kipya. Still watu hawaoni hayo wananakiri. Mimi ukiniomba nakuachia hata ukaandike kitabu kabisa. Just kuomba tu muhusika mbona vyepesi mnoo
Pole sana
 
Bora wewe aisee mimi nilikuta mada nzima wameihamishia kwenye blog. Hafu kuna mtu kaiona huko kaipenda akaleta tena huku jf..
Ni sawa kunakili kitu cha mtu ila kuomba ridhaa kwa muhusika ni vizuri zaidi.

Watu wanadhani hua tunaamka tunaandika tu ila tunaingia ghalama sana hadi kitu kupostiwa hapa jf. Mfano mada hii ilinichukua 17,000/=Tsh na muda wangu wa kutosha maana nilitumia masaa 5kuandika.
Why? Sina kifaa cha kuandikia so kila nikitaka kuandika lazima niende Cafe.
Huko ni ghalama zatumiaka then mtu anakopi so easily bila taarifa. Sio Uungwana na Utu kabisa
View attachment 1564640
Nyinyi pia huwa mnakosea kitu kimoja, makala kama hizi muwe mnaandika na marejeo, ukiwa unafanya khiyana na nyinyi lazima mfanyiwe khiyana. Haya ndiyo malipo ya wizi.
 
Hamna banaaaaa fanyeni kazi Acheni porojo jamvini
Usiemjua usimdharau, najua mapito yangu, mvua yangu jua langu. Naumia na baridi kali na jua pia, niko mbali na nyumbani nahussle, then unaongea kirahisi tu fanyeni kazi. Mkuu, tuheshimiane budda! Nafanya kazi zaidi ya ujuavyo hizi porojo za humu jamvini ni sehemu ya kujifariji
Saint Anne its me Careem.
 
Kuna member mmoja kwenye twitter anajiita Kidukulilo leo nimeshuhudia kwa macho yangu amecopy na kupaste style yangu, najua sisi kama member wa hapa JF pia tuna account katika mitandao mbali mbali lakini kwanini?

1. Uchukue mambo ya JF uyapeleke Twitter?
2. Kwanini ucopy na kupaste hadi style ya mwenzio?

Kwa kweli alichokifanya huyu member anaejiita Kidukulilo huko kwenye twitter sijapendezwa nacho hata kidogo. Hatukatai kuigana kupo lakini sio mpaka style ya mwenzio.



Kwenye kila post nikionyesha kufurahi lazima utakuta hizo emoji kama zilivyo zikiwa zimefuatana katika style hiyo ya 3x3 na naitumia kwa muda mrefu sana, kwanini mtu acopy hadi style ya member mwenziwe?

Ushahidi upo chini kwenye picha.

View attachment 1564618
View attachment 1564619
Ingekuwa bora zaidi ugomvi huu ungeubakiza kwenye mtandao huo huo ulikotokea? Waliouona huko ndiyo wangenufaika kwa kusikia pamde zote mbili. Mimi siko huko. Naliona suala hili kwa mara ya kwanza hapa. Na sijui kama mgomvi wako yumo humu JF. Kama hayumo, maonyo yako yatakuwa hayakumfikia. Kama ungeyatoa kulekule yalikotokea bila shaka angepata rejesho lako.
 
Ile mbwa isiyojua kucopy hatimaye imeniblock
Screenshot_20200909-222436.jpg
 
Ingekuwa bora zaidi ugomvi huu ungeubakiza kwenye mtandao huo huo ulikotokea? Waliouona huko ndiyo wangenufaika kwa kusikia pamde zote mbili. Mimi siko huko. Naliona suala hili kwa mara ya kwanza hapa. Na sijui kama mgomvi wako yumo humu JF. Kama hayumo, maonyo yako yatakuwa hayakumfikia. Kama ungeyatoa kulekule yalikotokea bila shaka angepata rejesho lako.
Mkuu maonyo yamemfikia hatimaye kaniblock!!
 
Tumshauri mwenzetu hatua za kufanya, maana hili swala la kukopiwa limemletea msongo wa mawazo na kumwathiri kisaikolojia.
Haipendezi kuiba kitu Cha mtu bila ku acknowledge huo sio uungwana kwenye academic Hilo ni kosa, Ila JF watu wengi huiba taarifa na kupost mitandao mingine Kama wao, kuanzia thread's Hadi comments za watu
 
Haipendezi kuiba kitu Cha mtu bila ku acknowledge huo sio uungwana kwenye academic Hilo ni kosa, Ila JF watu wengi huiba taarifa na kupost mitandao mingine Kama wao, kuanzia thread's Hadi comments za watu

Kuna vitu vya kulalamikia kwamba umeibiwa, ila sioni kama emojis ni moja ya vitu hivyo.
 
Back
Top Bottom