Krismas hii Ngina amenitoa jasho kweli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Krismas hii Ngina amenitoa jasho kweli!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Dec 26, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kule kwetu kijijini enzi zetu tulikuwa tunajua sikukuu tatu tu kwa mwaka, kulikuwa na sikukuu ya idi, Krismas na kuzaliwa kwa chama cha TANU, kwa hiyo wazazi walikuwa hawaumizi kichwa sana kuhusu nguo za sikukuu, kwani ni sikukuu moja tu tulikuwa tunapata nguo mpya. Kwa wakiristo walikuwa wanapata nguo mpya wakati wa Krismas na waislamu walikuwa wanapata nguo mpya wakati wa Idi.

  Hata hivyo nikisema nguo mpya sina maana ya baba kwenda dukani na kununua nguo mpya kwa ajili yako, hapana. Nguo mpya ilikuwa na maana baba kuchukua suruali yake ya zamani, kuikata kwa wembe vizuri bila hata kukupima. Halafu angeipinda chini kwa umahiri mkubwa. Shughuli ingekuja kwenye ukubwa wa kiuno. Kwa sababu hakuwa na ujuzi wa kupunguza kiuno, angetafuta mkwiji, yaani tambara kama mkanda. Angekuita na kuanza kukupa semina kwanza kabla hajakupa hiyo nguo mpya. Angekwambia, yeye kama baba wa familia anajitahidi sana kuona familia yake inafurahiya sikukuu. Angesema, kuwa amejitolea hata kutoa nguo yake ya pekee kwa ajili yako. Halafu angekupa hilo suruali ambalo alikuwa analivaa siku akienda kuwasalimia wakwe zake tu.

  Angekwambia ujaribu sulupwete hilo na angekupa pamoja na ule mkwiji ili sulupwete hilo lisidondoke. Angekusaidia kufunga mkwiji na kukuambia, 'hebu tembea.' Halafu angesema, ‘umependeza kwelikweli.' Kwa sababu ya utoto na ushamba wa wakati ule usingejua kwamba, sulupwete hilo linakufanya ufanane kama kifurushi cha viazi vitamu. Lakini, kwa sababu kule kwetu wakati ule, kila mmoja alikuwa anakatiwa kipande cha suruali na baba yake na kuhesabiwa kuwa amepata nguo mpya, hakuna aliyejali. Nawasifu sana wale wazee wa enzi za utoto wetu. Ni kweli kabisa, nguo mpya maana yake ni nguo ambayo hujawahi kuivaa. Kama baba yako aliivaa na kukupatia wewe, kwako ni lazima iwe mpya.

  Lakini huku mjini na kwa watoto wa sasa, mambo ni kinyume kabisa. Krismas hii wanangu hawa watatu wamenitoa jasho kwelikweli, hususan huyu binti yangu Ngina, Binti huyu ananipa ugonjwa wa moyo kila uchao. Wiki moja kabla ya ujio wa sikukuu hii ya Krismas wanangu walitaka kujua nitawanunulia nguo za aina gani. Niliwambia hali ya uchumi hairidhishi na nikaona ni wazo zuri kusingizia umeme. Niliwaambia, kiwanda cha kutengeneza fedha kimesimama kuzalisha kwa sababu ya umeme. Huyu mwanangu Ngina mwenye kiherehere kama bibi yake mzaa mama, alinikata kalma na kusema, ‘baba fedha zinatengenezwa Ulaya siyo hapa nchini. Tuna orodha ya nguo tunazotaka tunataka kwenda na fasheni safari hii, mie bila skin jinzi hapatatosha hapa.'

  Nikajua walimu wa siku hizi ni wataalamu hasa, yaani mtoto wa darasa la nne ameshafundishwa kuwa fedha zinatengenezwa Ulaya! Ikabidi nijifanye sikusikia maelezo ya huyu binti yangu ambaye kwa kawaida ndiye anayeongoza migomo kwenye familia yangu. Nikawaambia kama wanataka, nitajitahidi kila mmoja apate gauni, shati na suruali ya mtumba. Kusikia hivyo, watoto wakasema, itakuwa ngumu wao kukubali kuvishwea mitumba. Ngina alikuja na wazo mbadala, alisema, kama sina hela ni afadhali tuuze TV yetu. Lakini wenzake walipinga lile wazo wakidai watakosa kuona Ze Comedy. Ngina hakukubali kushindwa akaja na wazo lingine akitaka niuze Music System yangu ili wapate nguo za sikukuu. Nilipinga wazo hilo na kumfokea kwa kuwa na mawazo mufilisi. Lakini wapi, Ngina hakubali kushindwa, alinijia juu akidai ni jukumu langu kuhakikisha wao wanapata nguo za sikukuu, kwa hiyo nipunguze jazba tuweze kujadili hadi kufikia muafaka. Nilimuonya achunge kauli zake za maudhi.

  Hata hivyo alikuja na wazo lingine, alinitaka nikakope. Alinishauri nikakope kwa jirani yetu mmoja ambaye aliwahi kunituhumu kwamba ninamilki mtandao wa wezi wa magari baada ya kuniona nikija na magari tofauti hapo nyumbani karibu kila siku. Magari ambayo yalikuwa ni ya kazini kwangu. Huyu jirani alinichongea Polisi nikaja kusachiwa na kupelekwa kituoni kutoa maelezo. Nilikuja kugundua kwamba ni nuyu jirani yangu ndiye aliyenichongea, kwani baada ya kukamatwa na kupelekwa Polisi huku nyuma alitamba kwamba mwaka huo lazima nifungwe.

  Ilibidi nigeukie Dini na kuwaambia kwamba, hata bwana wetu Yesu Kristo katika kueneza Injili wakati huo alikuwa na nguo moja tu na hakuwahi kwenda na fasheni. Wote walinijia juu wakidai nimemkashifu Bwana Yesu Kristo na watamwambia mchungaji. Nikaona ule mjadala utakuwa hauishi kama nisipokuwa makini. Niliwaomba waandike mahitaji yao, kisha nitaangalia uwezekano wa kuomba mkopo kibaruani kwangu. Nikawa nimeufunga ule mjadala.Ama kweli watoto wa kizazi hiki, hawana maadili kabisa.
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Watoto wa siku hizi wananifurahisha jinsi wanavyotambua haki zao mapema, hizi siyo enzi za ndiyo mzee tena, lol,.
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sio hawana maadili bali baadhi yao wana akili zinazojitegemea, unatakiwa ufurahi badala ya kumsema hana maadili.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Nadhani ni muhimu kuwafundisha watoto wetu negotiation skills. Na watambue kuwa sio kila wanachotaka maishani watapata 100%. Wanangu watajua one principle: tutakopa kwa ajili ya vital (sio hata basic needs tu! I mean food and shelter) na hatuko desperate for anything! Dingi, utatengeneza kizazi tunachoona maofisini, nina coaligue huwa wakija wale machinga wenye magari wanaotoka china na belgium kusanya, anakopa nguo zake na za wanae worth tshs 2M! Anakopa hadi miwani ya jua! Sijui anaishije huko mtaani kwake!
   
 5. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Duh! Nimeipenda na imenikumbusha zamani.hilo sulubwete.kwa watoto wengine ambao tulikuwa tukichimbwa biti na wazazi basi tulikuwa tunafanya maandalizi ya mda mrefu sana ili siku ikifika basi tayari tunakuwa na kianzio.
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  My dear Lizzy, kusema kweli ni kukosa maadili, yaani mwanangu mwenyewe wa kumzaa, ajibishane na mimi kama vile anajibishana na mtoto mwenzie! hiyo haikubaliki, wakati mwingine natamani kukatandika, sema tu kaliugua sana utotoni mwake!
   
 7. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280

  King umeongea jambo la maana sana. Watoto wa siku hizi, kwa vile baadhi yao huwa wanaona kila siku wanakula, wanavaa, wanaenda shulenzuri, basi huwa wanajisahau kuwa kuna kukosa na sio kila kitu wanachotaka wanakipata. Matokeo yake wanakuwa na matarajio makubwa sana hasa wanapokuwa wanahitaji kitu, hawaachi kukuganda. Nadhani kuwafundisha negotiations skill is the way.....
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwanangu,uliyoyasema ni ya kweli kabisa, kuna watu wanashindwa kutofautisha kati ya uhitaji na utashi na hao wako kila mahali duniani kote. mimi najitahidi sana kununua kulingana na uhitaji na siyo utashi................kama mulivyosema kitu muhimu ni uhakika wa kuwa na chakula, malazi na mavazi................Nikisema chakula sina maana ya Pilau, kuku, nyama, mayai, maini nk, na nikisema malazi sio kulala kitanda cha sita kwa sita, godoro la springi sijui la milioni ngapi na mito lukuki kitandani na midoli isiyo na idadi, na nikisema Mavasi sina maana ya Suti, skin jinzi, magauni ya Boutique, vipodozi vya gharama na kila aina ya ghasia................
   
 9. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,110
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  hao wanao kiboko. nimecheka kwelis
   
 10. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kikazi kipya iko............... yan watoto wa siku iz wana mahitaj balaa. sijui kwa kwel 2nakwenda wap maana wamekuwa balaa.
  umenichekesha bila skin jeans hapatoshi lol.
   
 11. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  ndio wanaohitajika kwa mabadiliko. Sisi tuliokua enzi za ndio mzee tunaibiwa na tunakaa kimya.
   
 12. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #12
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Wala hawana makosa Mtambuzi kwa kuwa hivyo ndivyo walivyolelewa, mbona sisi tulikuwa na bado tuna maadili mazuri? kwanini wao wasiwe nayo? whats wrong with them? Kosa ni kwa walezi wala si mwingine au mtoto.
   
 13. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Hii mbona kama busasa za mlevi katika Mwananchi J'mosi?
   
 14. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #14
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,452
  Likes Received: 4,736
  Trophy Points: 280
  Lakini huyo Ngina si kubisha tu alikua na HOJA nadhani
   
 15. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #15
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha mengi hasa huo utaratibu wa nguo za sikukuu...baba yangu alipenda sana kunirushia makaptura yaliyokatwa kukoka katika suruali zake za zamani. Hakuwa maskini sana wakati ule,hebu fikiria meneja wa duka la kijiji,duka ambalo halikuwa na mshindani...kununua redio ya mbao lazima ujaze fomu maalum. RIP dad! Hata hivyo adhabu niliyompa ni kutotumia jina lake...majina ya ubin situmii jina lake...jamaa alikuwa mpuuzi sana,
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  mfundishe Ngina kuwa si kika atakacho atapata. Halafu usiwazoeshe watoto nguo mpya sikukuu. Mie wazazi wangu walikuwa wananipa nguo mpya miezi ya kawaida. Sikukuu hakuna nguo mpya
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Dec 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Basi inabidi ujilaumu kwa kiasi kikubwa maana wewe ndie uliyetakiwa kumfunza maadili unayotamani/taka angekuwa nayo. Anza sasa ili mwakani aombe tu na ukisema haiwezekani atulie.
   
 18. F

  Fofader JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Mtambuzi pole sana. Namfagilia mwanao Ngina. Angeomba ndege au gari ningeshangaa lakini nguo!!! Hiyo kawaida fanya kazi inayolipa bana. Ongeza uwezo wako wa kupata pesa. Watoto wana imani na baba zao.
   
 19. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #19
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Kiongozi wa migomo kwenye familia!!!!!
  teh!teh!teh!
  nimeipenda hiyo
   
Loading...