Kwa waoulizia Kuhusu Muhimbili Nitaandika hapa kwa kifupi labda kuwe na swali
kwanza muhimbili huombi kupitia nacte kwa sababu chuo kipo chini ya wizara ya Afya hivyo utaratibu unaomba kupitia chuoni moja kwa moja na utaratibu ni kuwa application form huwa ziwekwa kwenye website ya chuo kuanzia mwezi wa nne mwanzoni na hutoa mwezi mmoja tu wa kufanya application na application form inalipiwa Elfu 20
Baada ya application kufungwa kama hukufanikiwa kufanya application mwezi wa Kumi huwa wanatoa tena second around application unaweza kufanya kwa utaratibu ule ule!
Kozi zote hapa Muhimbili lazima uwe umefaulu masomo Matano yaani Mathematics,Biology,physics,chemistry,na English kuna baadhi ya Kozi Biology ni major subject,chemistry ni major subject na physics ni major subject
Wakati unachukua Form kutoka kwenye website ya chuo uwe makini na ujue ni form gani unaichukua kuna Regular Programe na Excutive programm( evening)
Ukichukua Regular program (government sponsored) ambayo mara nyingi huwa ina ushindani sababu ni wengi wanao omba,ada ni laki 4.5 per year,utapewa hostel,hela ya field utajitegemea utasoma Asubuhi kuanzia sa mbili hadi sa saba kwa baadhi ya Kozi
Excutive program ( Evening) ada ni 1.5M,utajitegemea kila kitu sehemu ya kulala means hostel hutapewa labda ulipie laki 6 utapewa hostel,utajitegemea chakula,hela ya field na utasoma kuanzia sa nane kwa baadhi ya Kozi na mara nyingi hapa competition huwa ndogo!
wastani ni 50 ukishindwa kufikisha wastani huo kwa masomo matatu una disco.
Kama kuna swali labda