Kozi ya Ufamasia

Inategeme kama kuna nafasi au ikitokea mtu anataka kuhamia pharmacy mnaweza kuexchange

Ila kiujumla ni rahisi kuhama kutoka MD kwenda course zingine kuliko kutoka hizo kozi kwenda MD
Nmesikia kuhama kozi hapo MUHAS mpaka umpate mtu wa ku exchange je n kweli?
 
Habari zenu wakuu,samahani mm nlikuwa natamani nisome pharmacy certificate.,alaf katika ufaulu wang masomo ya sayansi nimefeli chemistry tu.,je, naweza kupata chuooo?
 
Hivi mtu aliyesoma CBA (Chemistry, Biology, Agriculture) anaweza kuchaguliwa huko?
 
....pharmacy msuli wake n hatar ..utafika mda utataman kuhamia md...utaona wenzako wanakula bata afu we ndo unateseka ...na hyo c muhas tu bal n vyuo vyote imrad n bpharm....bt ukijua ulichofuata hutakimbia bali utaipenda sana...karibu pharmacy jpo m cio wa muhas...
Nashukuru mkuu... lakini ningependa kujua pharmac unakua una deal na masomo yapi hasa
 
Msuli wake ni mkubwa kuliko wa medicine.Kazi unafanya hospitali,viwanda vya kutengeneza dawa,regulatory authorities kama Pharmacy Council na TFDA...Karibu Muhas upate stress

Unaweza pia ufanya kazi kwenye maduka ya dawa (Community pharmacies) na mashirika mbalimbali yasiyo ya serikali (NGOs)
 
Nashukuru mkuu... lakini ningependa kujua pharmac unakua una deal na masomo yapi hasa

Wewe nenda shule tu utayakuta.Lazima uwe na basic knowledge ya Anatomy,Physiology na Biochemistry..Hii ni bila kusahau somo muhimu la ethics and professionalism

Then utazama na yako haya
Medicinal Chemistry ambayo kimsingi ni organic chemistry
Pharmaceutics ambapo utajua maujanja ya akuformulate dosage forms..Hapa utajua kidonge kinatengenezwaje kuanzia mwanzo kabisa

Pharmacology...huyu ndio mama yao.Utajifunza dawa mbalimbali na namna zinavyofanya kazi mwilini,muingiliano wake na dawa nyingine,matumizi yake kimatibabu,na madhara yake kama yapo

Pharmacognosy utajifunza mimea na vitu vyote asilia vinavyoweza kutumika kama dawa.Utasoma botany hapa na mwisho wa mwaka mtaenda Tanga na Arusha kuishuhudia hii mimea

Na kadhalika
 
acha upotoshaji kaka, kozi yoyote ya afya(yoyote) msingi mkuu ni somo la biology, kama huna bios sahau.(Pcb)

Sasa wewe unasema anapotosha wakati anakwambia ukweli.Nenda pale Sekou Toure kuna intern pharmacist graduate wa CUHAS na amesoma PCM Ilboru.Hivi unaijua kozi ya pharmacy?Ni kweli kama huna biology utasumbuka hususani kwenye basic knowledge kama anatomy,physiology na biochemistry ambavyo hata hivyo ukiwa mwanafunzi smart unazimaster vizuri tu.Huko mbeleni ni kemia na mambo mengine ambayo hayategemei sana hiyo Advanced Biology unayoisemea wewe
 
...ahsante ndugu, hata m mwenyewe nmesoma pcm na npo cuhas pharmacy mwaka wa pili...so sibahatishi ninachosema...pharmacy is ol about chemistry and a very manute biology...
 
Back
Top Bottom