Habari za asubuhi wana JF.
Nina somea computer science level ya degree, nahtaji kufahamu material,njia Na sehemu ambayo nitapractice hizi cozi vizuri kwa muda wangu wa ziada pia naomba guidance kutoka kwa expert, nahtaji kufahamu ipi inalipa zaidi katika upande wa technolojia hasa hapa nyumbani kati ya kazi za programming Na animation. Nina penda sana kufanya hizi kazi Na nahtaji kusoma ndani zaidi ndo maana nahitaji kufanya uchaguzi ili niwe vizuri saana. Maoni Na msaada wa wa ki-ushauri ni muhimu, karibuni.
Mimi nipo zaidi kwenye mambo Ya usanifu majengo (architecture) so, nitakushauri kwa uwelekeo fulani ambao sio 100% kwenye line yako Ya Computer science.
Nimeanza kufanya programming ambayo ni visual programming (building design with codes) kiukweli haya mambo ni machache sana kwa context Yetu lakini sio impossible...mara nyingi watu wengi kwenye ofisi zilizopo serious huwa wanakwama kufanya baadhi ya mambo bila programming na Ukipata chance inalipa sana, hasa foreign companies..cha msingi upate connections tu, ila kuna some very serious people in need hasa Dar es salaam, sema issue ni connections which needs time.
Nafanya Pia animations but architectural animations only, ambayo kibongo bongo ndio kwanza ni chipukizi...kwa sasa ni makampuni makubwa tu na real estate developers ndio wapo interested. Lakini kwa wewe nahisi upo kwenye "character animations" ambayo ina demand sana mpaka natamani niisome...cha msingi wewe jiwekee connections na media hasa "visual adds" I can assure you utafanikiwa in months kwa sababu kwa sasa tanzania inategemea sana social media ambazo ni sawa na matangazo.
Changamoto iliyopo Tanzania kwa mawazo yangu ni hivi;
1. Hakuna platform inayo-acknowledge teknolojia mpya zijazohusu visualization Kabisa.Huku mambo yanafanywa kimazoea sana na kujuana kwingi. Unaweza kuwa talented na kazi ukakosa au worse, ukalipwa chini Ya Kiwango sana, kazi Ya siku Tatu bila kulala ukaambulia laki 2 au ukadhulumiwa kabisa hasa baada Ya watu kujua kwamba, ili wakulipe ni lazima waone kwanza ulichofanya (na wachukue copy). It's complicated than you think kwenye hili tatizo!
Nafikiri hilo Pia linaongeza tatizo la kufanya watu wasielewe ugumu na gharama Ya hii kazi;
Mfano kuna mtu alikuja kwangu na mil1 anataka animation Ya mji mzima (Dar kwa mfano) ikiwa na magari yanatembea na watu!!
2. Hakuna shule za kujifunza au kujiendeleza au zenye ari Ya maendeleo..zaidi Ya vyuo, ni mara chache utakuta watu wanajifunza, so hii trend inahitaji passion sana zaidi ya Pesa mbele. Labda hapo baadae.
Cha msingi, fungua kampuni,tafuta watu wengine talented then anza kazi.Hii ita kufanya uonekane legit na utaweza kupanda tenda kubwa..mfano kama ni character animator, unahitaji story teller mzuri
Usiogope kuanza na free work kwanza ili kujenga jina.
Pia, usife moyo.
Pia, ukiona vipi, ajiriwa kwanza usome trend Ya soko na ukutane na watu muhimu...Goodluck!