Kova: Ole wenu wafuasi wa Gwajima

Kova: Ole wenu wafuasi wa Gwajima

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,909
Reaction score
4,057
kamanda Kova amewaonya vikali wafuasi wa Gwajima kuandamana Leo kuelekea makao makuu ya polisi ambapo mch. Gwajima Leo atahojiwa.

Onyo hilo linakuja baada ya mchungaji Gwajima kuwaambia wafuasi wake wakati wa ibada ya pasaka kumsindikiza makao makuu atakapoenda kuhojiwa.

My take;
Gwajima bora uwazuie wafuasi wako kwani watakula kichapo kikali Kova huwa hatanii waulize wanabawacha waliojaa HP jf watakujuza.

Chanzo: Magazeti RFA
 
bawacha msikae kimya HP jf toeni some kwa wanagwajima
 
Bora uchangie mwenyewe upuuzi wako huu
 
Mwaka huu siyo mda wa kucheka na watu wahuni wenye lengo la kuvuruga amani na utulivu wa taifa letu kwahiyo polisi tunawaomba mkkomae nao kweli.
 
Kova awe macho na tahadhali ya ugaidi aachane na siasa ampazo zinapenyezwa kwenye dini.
 
mambo mengine tunayataka wenyewe sasa mtu anawaambia watu waje central kufanya nini kama sio kusababisha vurugu,tuacheni ushabiki watanzania tukipigwa mabomu ya machozi tutasema polisi wanachuki na kanisa letu,ok hao waumini elfu sabini tutaenea kwenye chumba cha mahojiano na polisi ili tusikie askofu wetu anachohojiwa na sidhani kama mahojiano na polisi huwa wanaruhusu na wapambe kusikiliza ni hayo tu mimi si muumini wa Gwajima wala pengo
 
kamanda Kova amewaonya vikali wafuasi wa Gwajima kuandamana Leo kuelekea makao makuu ya polisi ambapo mch. Gwajima Leo atahojiwa.

Nina taarifa kuwa kuna wachache wako mbele ya jengo la central polisi pale kuna wengine wana pistol.Polisi wawa ambush na kuwa seach haraka.

Mtu akiitwa kwa mahojiano anatakiwa yeye sio wapambe
 
Halafu tunalaumu Tanzania maskini mara oooh viongozi hawafai mara siujui Rais hafai, kweli kwa aina hii ya watanzania hata angekuwa washington ndo Rais tungekuwa tu kama tulivyo. Hakika mabadiliko yaanze na mmoja mmoja kwenye ubongo wake
 
Nashauri ndugu zangu msiende na maandamano yenu kwanza hamjazoea;na pia gwajima yupo na wakili wake na haendi kuchinjwa.mahojiano ni kitu cha kawaida tu
 
Busara ya Gwajima na wale waliomtetea humu na kote kwingineko imeishia hapo. Sasa mtamtambua Seleman, hanaga utani kwenye haya makitu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom