Kova kuanza kusaka mtandao wa vipeperushi

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
POLISI nchini wamepanga kusambaratisha mtandao unaodhamini na kuchapisha vipeperushi vinavyohamasisha kufanyika kwa maandamano, kutaka kutolewa kwa Katibu wa Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake.
Hatua hiyo imekuja baada ya waumini hao kupanga kufanya maandamano Novemba Mosi, ambayo yatahamasisha mahakama hiyo kutoa dhamana kwa kiongozi wa taasisi hiyo na wenzake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova alisema wataanza kufanya msako wa wote wanaohamasisha, wanaochapisha na wanaotoa vipeperushi ili kuwakamata.
“Tunafuatilia wadhamini na wachapishaji wa vipeperushi kwani ni chanzo cha uchochezi na upotevu wa amani nchini,” alisema Kova.
Kova alisema maandamano hayo ambayo yamepangwa na waumini hao yanatishia amani , wananchi watashindwa kwenda kazini na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
 
Unasaka vipi wanaosambaza vipeperushi wakati aliyeandaa amejiandika jina in full pale chini!
 
Hawataki kuwakamata!
Kama kweli wana nia ya kweli kuwasaka na kuwakamata, wajitahidi wamkamate m2 mwenye hicho kipeperushi, awambie nani kampatia, hivyo hivyo chain itaenda hadi kwa mchapishaji. Ila mchapishaji hana kosa; kosa ni mfadhili wa hivyo vipeperushi. Kuchapisha ni kazi yenye leseni halali.
 
Unasaka vipi wanaosambaza vipeperushi wakati aliyeandaa amejiandika jina in full pale chini!
Kova nampendea jambo moja tu, kupenda kuuza sura kwe TV,
mi nafikiri akistaafu ajiunge na Bongo movie tuendeleze tasnia
ya filamu...
 
Back
Top Bottom