KOSA LANGU NINI NI VANNESSA
SEHEMU YA 10 FINAL...
.
MWISHO USIACHE KUNIAMBIA LABDA KUNA SEHEMU NILIKOSEA ALAFU MIMI SIJASHTUKA
Tuendelee
Mahusiano yetu yaliendelea mara kadhaa tukiishi wote mpaka alivyomaliza diploma ila kabla hajamaliza . alianza kubadilika na kuwa mtu wa huzuni . Sio yule Vannesa niliyemzoea baadae nilijagundua ni mjamzito nilishtuka sana . Maana sikutarajia kwa ujanja alionao angezembea abebe mimba . Akawa mtu wa kulia sana . Nilimbembeleza nikimwaminisha hakuna kitakachobadilika lakini hakuna jibu nililopewaga na mpaka leo sijui na siamini kama ni mimba kuwa inamliza
mwezi mzima nilipewa mara mbili na Nilipewa kinyonge sana nakuondoka . Nilijiuliza sana sana tatizo nini ila nilikuwa nauchosha ubongo bure sikupata majibu. Mimi mwenyewe nilipoteza furaha kabisa. Nikawa kama nimeganda hivi sio kwa sababu ya mimba hapana kwa sababu ya kupoteza kabisa utani tabasamu mazoea na uchangamfu aliokuwa ananiletea Vanne... hapa tu tayari nilianza kuonja maumivu ya kumpoteza kipenzi changu.
Sasa baada ya kama mwezi siku moja akiwa ashamaliza diploma ( nilisahau kuwaambia mrembo alikuwa anaitafuta diploma )alikuja ghafla getto . Alikuja analia mfululizo alivyofika tu akanirukia na kulala kifuani kwangu nikafunga mlango kwa mguu nikasogea nae mpaka kwenye sofa na kujaribu kumbembeleza huku nikimwomba aniambie kinacho msibu akawa ananiangalia usoni tu na kuongeza kulia .
Nilijikuta nikilia pia


tena machozi yakitoka kwa kasi ajabu nikihisi labda mimi ndio sababu ya yeye kuwa kwenye hali ile akawa ananifuta machozi nikamuuliza kosa langu nini ni Vannesa hakunijibu. Nilimkumbatia nikizidi kumuuliza lakini wapi mpaka leo sijawahi kujua kwanini alibadilika vile . Nikajaribu kumtajia ni mimba akatikisa kichwa kuashiria hapana na kuongeza kulia kwa kweli nilijikuta nalia pia kama nimefiwa .
Baada ya muda aliinuka ghafla . Akiwa amenyamaza akataka kutoka kufika mlangoni . Akaanza kuniambia nakupenda sana . Wewe ni mwanaume wapekee niliyekupenda kwenye maisha yangu. Akanikumbatia . Akaniambia najua unanipenda sana pia ila hakuna namna .
Moyo wangu ulihisi jambo baya machozi yalianza kutoka mpaka leo hii sijawahi tokwa na machozi hivyo. Akajitoa kwenye kukumbatiana akanipiga kibao cha wastani tu akiwa ashafuta machozi yake na nikawaida yake akitaka umakini. nilikuwa nishamzoea akarudia kingine kikali cha kuuma kabisa akaniambia unaweza kuishi bila mimi jitahidi kujipenda na kujilinda usiwe malaya sawa . Hapo tayari machozi yalianza kumlenga nataka kumkumbatia ili nimuulize tena shida nini akarudi nyuma na kuanza kukimbia nilimfuata mpaka nje ya geti nikilia sana . Akanigeukia tu uso wake ukiwa umefunikwa na machozi huwezi kuamini kama ni yeye . mimi nilikuwa nimemzoea usoni mda mwingi ni kutabasamu tu ila leo sura yake ili funikwa kwa machozi na huzuni tele alibadilika rangi na kuwa mwekundu . Hata mwili wake ulikuwa umepungua sana ndani ya mwezi ambao kuwa simwelewi.
Basi ndio sura iliyobaki kwenye akili yangu mwishoni akilia machozi yakishuka kinoma akanipungia mkono wa kwaheri na kusepa. sikuweza kumfuata zaidi kwani nilitoka peku sikufunga mlango na ile hali ya kulia ilibidi nilirudi tu ndani nisionekane na kadamnasi. Nilibaki Nikiumia na kuwaza mengi sana nikaanza kuwaza labda amepima ukimwi nini kakutwa nao na kaona nitamlaumu yeye au. Nilijiuliza sana nikaamua kwenda kupima . Majibu yakawa hakuna. Na angekuwa nao ningepata tu kama kuwa hatumii dawa na match za kibabe zisizo na fair play lazima ingekuwa balaa . Siku hiyo nilikosa usingizi kabisa kuwa sielewi nini kinaendelea
Sasa asubuhi na mapema kesho yake . Nilikuta meseji imetumwa saa nane usiku. Alituma Vanne. Inasema " Nitakuwa mbali ,mbali sana naomba usijitese kabisa endelea na maisha jiamini hakuna mwanamke wa kukukataa wewe naomba naomba sana uendelee na maisha. Jana nilitaka ulie ili nikiondoka usilie tena naomba iwe hivyo usilie wala kuwa na huzuni "
Daah sijui aliwaza nini meseji ndio kwanza ilinipa kilio acha nikiri tu nililia sana
Hiyo ndio meseji ilikuwa ya mwisho kabisa laini aliitelekeza mpaka ikafungiwa na account zake za social media alifuta zote mpaka email.
Na meseji yangu ya mwisho kwake ilikuwa kosa langu nini ni Vannesa?. Kwanini unataka kuniacha mwenyewe. Kosa langu nini?.
Mpaka leo hii sijibiwi?.
Akaniacha mpweke zaidi ya mpweke mkiwa zaidi ya mkiwa nilichanganyikiwa balaa .
Chuo nilienda kinyonge sana kila nikipitaga hiyo njia kumbukumbu zinanijia nilivyokuwa natembea nipo nae. Nikawa na mwona kwa mawenge niliyokuwa nayo nilipoenda jengo tulilokutana sana mgahawa tuliokuwa tunakula ulikuwa ni mtihani sana .
Kila siku najiuliza kosa langu nini ?
Nimiaka miezi siku kibao zimepita hata kunitafuta mara moja tu hanitafuti . Hata nijue tu kosa langu haniambii.
Naumia sana .
Kwanini basi ulinifundisha kupenda ?
Kwanini ulinionjesha penzi nikiwa kwenye kilele cha furaha ukanitelekeza ?
Kiukweli nilichelewa sana kununua nguo kwani wakati wote tulikuwa pamoja karibu miaka miwili sikununua nguo bila yeye na yeye ndio alikuwa ananichagulia kila nilipotakaga kununua nguo nilishindwa kabisa kujiamini kama hiyo nguo itanipendeza . Mwaka na miezi nane ilipita bila mimi kunua nguo mpya zaidi ya kudandia za wadogo zangu wawili ambao tunalingana kabisa kimo na unene ukituona utadhani mapacha nilitaka kujirudisha alikonitoa kuvaa ovyo . Au kiheshima sana kujaribu kumsahau lakini wapi ikawa kama kukimbia kivuli changu mwenyewe.
Kiukweli baada yake nilishalazimisha mahusiano kadhaa lakini wa kumfikia hata robo Vannesa wangu hakuna .
Miaka inaenda naogopa kuoa mwanamke ambaye moyo wangu haumpendi licha ya kuwa anatabia njema na sura nzuri. Na kadata sana kwangu. Na kumwacha a move on namwonea huruma na sioni mbadala wake yupo vizuri tu
Hebu nishaurini kwa hili la kuoa huyu mrembo ambaye anaingia kwenye maisha yangu ila moyo wangu katoweka nao mrembo Vannesa . Nimwoe hivyo hivyo au niendelee kumsubiri Vannesa
Swali la pili . Ile mimba naamini ni yangu je atakuwa alienda kutoa au mtoto yupo? Na kama yupo kwanini hamleti ?
Swali la mwisho kwa ulivyosoma
KOSA LANGU NINI?



