Kosa la wabunge 10 - Wajifunze toka kwa Mandela na mgomo wa kula kifungoni

Kwani si viongozi wa chama wapo? wamuadhibu basi! tuone mwenye nguvu!

Mwenye nguvu ni chama sio mtu binafsi! Zitto anatakiwa kuzingatia hilo na akiamua kuweka mbele maslahi binafsi ataendelea kuporomoka zaidi wakati huu ambapo vijana wengi na makini wameingia kwenye siasa!!
 
wasaliti adhabu yao ni kupigwa kiberit tu....aende uko CCM hatumwitaji
 
A very nice analysis Mkuu!!

Zitto ni kijana jeuri na anayejiona ana akili sana!! Asiogopwe kupewa adhabu, hana uwezo wa kukigawa chama. Kumbukeni chama si Zitto, mwacheni aende CCM!!
 
Kwani si viongozi wa chama wapo? wamuadhibu basi! tuone mwenye nguvu!
kesha adhibiwa na wananchi itamchukuwa muda mrefu kurekebisha damage aliyoifanya ukweli wenyewe uamuzi ule umemrejea kwa kiswahili cha kawaida imekula kwake he is no longer an icon as he used to be alifanya timing yake vibaya sana kiujumla hana nguvu yeyote
 
kaka Zito ametukatisha tamaa vijana, tunajua mawazo yake na hoja aliviona vya msingi ila sisi tutapigana kupitia nguvu ya umma ambayo haiangalii umaarufu au fedha bali uwajibikaji na ukweli.
 
Nikupateje hoja na ufafanuzi wako ni murua,HITIMISHO LAKO si SAHIHI SANA! hatujengi umoja kwa kuadhibu kosa moja. Mhusika alishajieleza humu ndani vema, na yeye ni mtu mwenye akili TIMAMU, "HILI KALIELEWA VEMA". Haja ipo kwa viongozi wote kuwa na umoja wa maamuzi hasa pale wanapokuwa na mitazamo tofauti, ili kulindaumoja wa CDM. Hili ni kwa viongozi wa juu wote,na si ZITO pekee! Hoja hii ilishajadiliwa sana, na sioni haja ya kuiendeleza! CDM juuuuuuuuuuuuuuuuuu, peoples...............................umoja ni nguvu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Sikuelewi kabisa.
Viongozi wana msimamo tofauti.
Kura inapigwa.
Kundi moja linashinda kwa uwingi wa kura.
Kundi moja linagoma kutekeleza matokeao ya kura.
Sasa umoja utapatikanaje?
Kwa nini kura imepigwa?
Mtu kuwajibishwa si lazima afungiwe au apewe adhabu. Hata kile kitendo cha kuitisha kikao kujadili maana ya matokeo ya kupiga kura, na namna kila kiongozi apasavyo kuwajibika baada ya matokeo ya kura na kuwekana sawa ni kuwajibishwa.

Mtu ana haki ya kupinga matokeo ya kura iwapo tu anadhani matokeo yamechakachuriwa.
 
Nikupataje,

This is very good analysis, I enjoy reading it. Zitto and many will learn from this example.
 
Kama mimi ningekuwa Zitto, ningekaa chini na kufikiri sana kwamba kwa nini jamii inanisema vibaya namna hii, nimekosea wapi mimi?.

Ila masikini unaweza kukuta katika fikra zake anawaza kwamba, labda hizi kelele zoote ni mashambulizi ya wapinzani wake wa kisiasa ndani na nje ya CDM, assumption ya namna hii itakuwa ni mistake kubwa.

Kuna thread moja, Zitto alichangia akasema kwamba tunamuonea sana, tutamuonea vipi wakati jamii imeweka matumaini kwake na wenzake ili angalau wapigane kufa na kupona kuisaidia dhidi ya matatizo lukuki ambayo chama tawala wameshindwa kuyafanyia kazi?.

Mtu makini hatafuti uongozi hasa katika nchi masikini kama ya kwetu kwa minajili ya ucelebrity, yaani kwa ajilil kupia ukitamba kwa vijana wa rika lako kwamba uko juu, bali unatafuta uongozi ili kutoa mchango wako makini, ili hata siku umeondoka duniani upate kukumbukwa kwa juhudi na mchango wako.

Kiongozi mwenye dhati, mwenye kujua matatizo ya nchi hii hawezi kuforge alliance za siri na watafuna nchi ili apatiwe vijisenti vichache na kuuza imani ambayo wananchi wameiweka juu yake(hapa simaanishi kwamba Zitto Kanunuliwa na mafisadi, nazungumzia kwa ujumla wa uongozi mzuri).

Hata Ukipewa Shilingi Billioni Moja, hicho ni kiasi gani?, bado zinazidiwa tu na fedha anazoweza kupata binti mdogo kama Rihanna pengine kwa kuuza single yake moja!!. sasa sembuse kuuza utu na imani ya Watanzania juu yako.

Inauma sana, na inasikitisha sana kuona watu ambao jamii inawaamini kwa wakati mmoja, baadae wanakwenda kusimama upande ambao si wa wananchi, kwa kisingizio cha fikra huru.

Tumpe benefit of doubt bwana Zitto labda kama kweli ni mtu mwenye kufikiria, ataelewa kwamba wananchi wana mitizamo gani katika ishu wanazozithamini sana.
 
Back
Top Bottom