Kosa la wabunge 10 - Wajifunze toka kwa Mandela na mgomo wa kula kifungoni

N

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2009
Messages
1,315
Likes
113
Points
160
N

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2009
1,315 113 160
Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela aliandika kitabu chake cha kwanza akielezea maisha yake tangu akiwa wakili hadi alipotoka gerezani kiitwacho “A long walk to freedom”. Waliokisoma watakubaliana na hoja yangu ninayoijenga hapa.

Mandela anaeleza kwamba alipokuwa gerezani kisiwani Robin vuguvugu mle jela lilikuwa likiendelea na ilifika mahala wafungwa walikuwa wakikubaliana ni aina gani ya mgomo wataufanya.

Mara nyingi walikuwa wanaishia kugoma kula (hunger strike). Lakini Mandela anaeleza kuwa binafsi hakuwa anaipenda migomo ya kula. Hivyo kila lilipoletwa wazo la kugoma kula Mandela alikuwa kwenye upande wa waliopinga wazo lile na mara zote ilibidi wafikie muafaka kwa kupiga kura. Kwamba tugome kula au tusigome.

Mandela anaeleza kuwa siku zote wenye wazo la kugoma kula walishinda kwa wingi wa kura.

Hadi hapa hakuna tofauti na CHADEMA kupiga kura kugomea hotuba ya Rais Kikwete yaani “Walkout”. Pia hakuna tofauti ya Zitto Kabwe na Mandela hadi hapa. Mandela hakupenda “hunger strike” wakati Zitto hakupenda “Walkout”. Kina Mandela walishindwa maoni yao kwa kura kama Zitto na wenzake walivyoshindwa juzijuzi.

Sasa tuone utekelezaje wa maamuzi ya upigaji kura kati ya Zitto Kabwe na Nelson Mandela.

Mandela anaeleza kwamba japo hakuunga mkono wazo la “hunger strike” lakini baada ya matokeo ya kura yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kusimamia kugoma.
Na anaeleza kuwa kama msimamizi mgomo unapofika siku ya tatu alitegemea kuona ndoo za vinyeshi ziwe kavu lakini anashangaa kuona zikiwa na vinyesi vya hapa na pale kwa maana ya kwamba kuna watu walikuwa wanachomoka kimyakimya na kujificha na kwenda kula kwa kushindwa kuvuilia njaa.

Anaieleza hii kama kichekekesho lakini Mandela anaeleza jinsi ambavyo wagomaji walitakiwa kuonyesha umoja mara tu baada ya matokea ya kura. Kwamba hata kama bado kuna watu walitoroka kwenda kura lakini walifanya kwa siri sana na hadi anaandika kitabu hakuwajua.

Mandela anatufundisha nini? Anatufundisha kwamba haia haja ya kupiga kura kama wote mna wazo moja mnalotaka litumike. Ila kama kila mmoja ana wazo lake kinachofuta ni kujadiliana na kupima sababu na hasara za kila wazo.

Yakishindikana yote basi hamuwezi kupoteza muda mkijadiliana wakati uamuzi unatakiwa ufikiwe. Ndipo hapo mnaposema hoja zenu wote ni safi lakini kwa vile tumeshindwa kutoa uamuzi kwa njia ya ushawishi na maoni basi kura ndiyo iwe uamuzi utakaoheshimiwa.

Hata kwenye soka tena ya watoto wadogo tunaelewa kuwa inawezekana timu ikapenda kuanzia mechi kwenye goli la kusini labda kwa sababu siku hiyo upepo unawasaidia kutokea kusini. Kama timu pinzani haioni shinda kuanzia kaskazini basi hakuna sababu ya kupiga kura kwa kurusha shilingi.

Lakini kama wote Timu A na Timu B wanagombania golila kuanzia basi wanaweka rehani maamuzi yao kwenye matokeo ya kura. Kwamba watafuata matokeo ya kura ili kuamua cha kufanya yaani kuannzia wapi. Ndipo hapo kura inapigwa kwa kurusha shilingi. Hapa hakuna cha kur kulingana. Lazima shilingi itatoa maamuzi. Ama Timu A itashinda kwa kuanzia kusini ama Timu B.

Baada ya kupigwa kura kama walivyofanya kina Mandela au kurushwa shilingi zilivyofanya zile timu hakuna majadiliano mapya tena. Kugomea uamuzi wa kura ni sawa na kugomea maamuzi yaliyokubaliwa.

Ndiyo maana Mandela analifafanua hili kwamba japo yeye siku zote amepinga kwa hoja na kura kwamba hapendi hunger strike lakini pamoja na kushindwa amekuwa akiwa kinara wa kusimamia mgomo. Mandela anaonyesha nidhamu ya maamuzi. Alishindwa kupinga mgomo kwa ushawishi wa hoja, kisha akashindwa kwa kura hakuwa na jinsi kuukata uamuzi wa walio wengi.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Nelson Mandela, shujaa anayeheshimika duniani kote. Je, ndivyo ilivyokuwa kwa Zitto Kabwe? Wote tumejua sivyo.

Kwanza bila Zitto tusingejua maamuzi yale yalifikiwa vipi. Hivyo Zitto katusaidia kujua kuwa yalifikiwa kwa kupiga kura. Kumbe demokrasi waliyotumia kina Mandela mle gerezani ndiyo demokrasia waliyotumia CHADEMA.

Siungani na wanaolaumu Zitto kwa kutoa siri ya kilichofanyika kwani kwa katufunulia walipiga kura katuonyesha kwamba CHADEMA ni chama makini kinachoheshimu maoni ya watu na si kuendeshwa na udikteta.

Sasa baada ya kupiga kura ilitakiwa kufanya nini? Hapa Zitto anatofautiana na Mandela. Mwenzake Mandela aliamua kuwa kiongozi wa mgomo lakini Zitto hafanyi kama Mandela. Zitto alipiga kura lakini hafanyi kulingana na matokeo ya kura. Zitto anasahau kuwa kama kundi lake lingeshinda CHADEMA wangefanya kama alivyotaka yeye. Sijui napo angeenda BBC na kusema kuwa CHADEMA haikugoma kwa sababu waliokataa mgomo walikuwa wengi?

Mandela anawafundisha watu kama Zitto kwamba maamuzi yoyote yaheshimiwe maadamu hayajafikiwa kwa njia ya udikteta.

Zitto hata kama tunampenda vipi lakini mbele ya kadamnasi katuonyesha kuwa ana utovu wa nidhamu ya maamuzi. Kukataa maamuzi ni utovu wa nidhamu. Utovu ambao Mandela hautaka kuushiriki hata kama hakupenda la walio wengi.

Zitto angesema kwamba hakupiga kura kabisa, mimi nigekuwa wa kwanza kumuelewa na kumtetea. Hata mtoto wa darasa la tatu anajua nini cha kufanya baada ya matokeo ya kura. TUmecheza michezo mingi utotoni inayohusisha kupiga kura. Leo umepiga kura, wenzako wengi wamesema wanataka kugoma. Matokeo yanatoka badala ya kuyaheshimu wewe unafanya unavyotaka na unanung’unika. Hivi neno utovu wa nidhamu litumike kwa vitendo gani kama si hivi!

Kama CHADEMA au Zitto mwenyewe wana mpango wa kuuwajibisha utovu huu wa nidhamu basi huu ndiyo wakati muafaka ikiwa bado mapema na wengi wakiwa nalo kichwani. Ni kweli kunaweza kuwa na mgawanyiko lakini kazi ya kuelewesha itakuchukua muda na watu wataelewa polepole wale wasiotaka kuelewa mapema. Mkisubiri utovu huu muushughulikie zaidi ya 2012 au 2013 wakati uchaguzi wa 2015 umekaribia basi mgawanyiko unaweza kuingia hadi wakati wa uchaguzi na ikala kwenu.

Linalowezekana leo lisingoje kesho.
 
G

Gaza

Senior Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
104
Likes
5
Points
35
G

Gaza

Senior Member
Joined Nov 3, 2010
104 5 35
Zito heshima yake kisiasa imeshuka sana mbele ya jamii ya wa Tanzania wakati vijana tuna kataa msemo wa vijana ni taifa la kesho Zito ana thibitisha ukigeugeu wetu na tamaa za kitoto ,tulisha mstukia yuko Chadema kimaslahi zaidi na kule kupayuka bungeni alikua ana tafuta umaarufu sasa anaona kaupata,mlango alio ingilia ndio atakao tokea
 
nsimba

nsimba

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2010
Messages
785
Likes
0
Points
33
nsimba

nsimba

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2010
785 0 33
Nikupateje hoja na ufafanuzi wako ni murua,HITIMISHO LAKO si SAHIHI SANA! hatujengi umoja kwa kuadhibu kosa moja. Mhusika alishajieleza humu ndani vema, na yeye ni mtu mwenye akili TIMAMU, "HILI KALIELEWA VEMA". Haja ipo kwa viongozi wote kuwa na umoja wa maamuzi hasa pale wanapokuwa na mitazamo tofauti, ili kulindaumoja wa CDM. Hili ni kwa viongozi wa juu wote,na si ZITO pekee! Hoja hii ilishajadiliwa sana, na sioni haja ya kuiendeleza! CDM juuuuuuuuuuuuuuuuuu, peoples...............................umoja ni nguvu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
S

superfisadi

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2009
Messages
553
Likes
3
Points
35
S

superfisadi

JF-Expert Member
Joined May 22, 2009
553 3 35
mnamzidishia umaarufu kama anawaudhi shikeni vichwa mumpigien uwiiiiiiiiiiiiii kama wanavyofaniwa wanaccm wakipita na sare zao mitaani
 
VoiceOfReason

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
5,234
Likes
59
Points
0
VoiceOfReason

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
5,234 59 0
This guy has been critised enough now..... Enough is enough, now lets wait and see if he has changed, Am sure he said what he did kiliwauzi wengi na anaomba msamaha.... What else can he say nadhani sasa tugange yajayo... lets see zitto of 2011
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,499
Likes
4,875
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,499 4,875 280
[
Siungani na wanaolaumu Zitto kwa kutoa siri ya kilichofanyika kwani kwa katufunulia walipiga kura katuonyesha kwamba CHADEMA ni chama makini kinachoheshimu maoni ya watu na si kuendeshwa na udikteta.

Sasa baada ya kupiga kura ilitakiwa kufanya nini? Hapa Zitto anatofautiana na Mandela. Mwenzake Mandela aliamua kuwa kiongozi wa mgomo lakini Zitto hafanyi kama Mandela. Zitto alipiga kura lakini hafanyi kulingana na matokeo ya kura. Zitto anasahau kuwa kama kundi lake lingeshinda CHADEMA wangefanya kama alivyotaka yeye. Sijui napo angeenda BBC na kusema kuwa CHADEMA haikugoma kwa sababu waliokataa mgomo walikuwa wengi?

Mandela anawafundisha watu kama Zitto kwamba maamuzi yoyote yaheshimiwe maadamu hayajafikiwa kwa njia ya udikteta.

Zitto hata kama tunampenda vipi lakini mbele ya kadamnasi katuonyesha kuwa ana utovu wa nidhamu ya maamuzi. Kukataa maamuzi ni utovu wa nidhamu. Utovu ambao Mandela hautaka kuushiriki hata kama hakupenda la walio wengi.

Zitto angesema kwamba hakupiga kura kabisa, mimi nigekuwa wa kwanza kumuelewa na kumtetea. Hata mtoto wa darasa la tatu anajua nini cha kufanya baada ya matokeo ya kura. TUmecheza michezo mingi utotoni inayohusisha kupiga kura. Leo umepiga kura, wenzako wengi wamesema wanataka kugoma. Matokeo yanatoka badala ya kuyaheshimu wewe unafanya unavyotaka na unanung'unika. Hivi neno utovu wa nidhamu litumike kwa vitendo gani kama si hivi!

Kama CHADEMA au Zitto mwenyewe wana mpango wa kuuwajibisha utovu huu wa nidhamu basi huu ndiyo wakati muafaka ikiwa bado mapema na wengi wakiwa nalo kichwani. Ni kweli kunaweza kuwa na mgawanyiko lakini kazi ya kuelewesha itakuchukua muda na watu wataelewa polepole wale wasiotaka kuelewa mapema. Mkisubiri utovu huu muushughulikie zaidi ya 2012 au 2013 wakati uchaguzi wa 2015 umekaribia basi mgawanyiko unaweza kuingia hadi wakati wa uchaguzi na ikala kwenu.

Linalowezekana leo lisingoje kesho.
Kwani si viongozi wa chama wapo? wamuadhibu basi! tuone mwenye nguvu!
 
D

dotto

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2010
Messages
1,722
Likes
21
Points
135
D

dotto

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2010
1,722 21 135
This guy has been critised enough now..... Enough is enough, now lets wait and see if he has changed, Am sure he said what he did kiliwauzi wengi na anaomba msamaha.... What else can he say nadhani sasa tugange yajayo... lets see zitto of 2011

Jamaa huyu Zito anadharau na sio mtu makini katika maamuzi ya pamoja. Lakini alishasema katika kampeni kuwa atagombea urais 2015. Hivyo anavyofanya ni vijisababu vya kujiunga na mwenzake Kafulila. Ni vema tu akaondoka kwa maamuzi ya kikubwa tu na sio ya kitoto na akagombee NCCR urais.
 
VoiceOfReason

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
5,234
Likes
59
Points
0
VoiceOfReason

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
5,234 59 0
Jamaa huyu Zito anadharau na sio mtu makini katika maamuzi ya pamoja. Lakini alishasema katika kampeni kuwa atagombea urais 2015. Hivyo anavyofanya ni vijisababu vya kujiunga na mwenzake Kafulila. Ni vema tu akaondoka kwa maamuzi ya kikubwa tu na sio ya kitoto na akagombee NCCR urais.
Kikatiba Zitto atakuwa na miaka 39 hawezi kugombea.... Lets give a guy a chance and see what he will do from now onwards
 
Gobegobe

Gobegobe

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Messages
245
Likes
1
Points
35
Gobegobe

Gobegobe

JF-Expert Member
Joined Nov 23, 2010
245 1 35
Zito heshima yake kisiasa imeshuka sana mbele ya jamii ya wa Tanzania wakati vijana tuna kataa msemo wa vijana ni taifa la kesho Zito ana thibitisha ukigeugeu wetu na tamaa za kitoto ,tulisha mstukia yuko Chadema kimaslahi zaidi na kule kupayuka bungeni alikua ana tafuta umaarufu sasa anaona kaupata,mlango alio ingilia ndio atakao tokea
Alaaa, mkuu upo ee!
 
Nyange

Nyange

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Messages
3,055
Likes
987
Points
280
Nyange

Nyange

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2010
3,055 987 280
Huyu bwana mdogo anapaswa kupewa onyo, mi binafsi huyu kijana namuona mwenye majivuno sana sana pale alipoteuliwa na kikwete kwenye tume ya madini. Huyu kijana ame-loose track mpaka leo.

Bwana zito, 1+1>2. Hii ndiyo nguvu ya chama. Tunajua sasa hivi mafisadi wamekubadilisha kwa fedha. Inabidi uheshimu maamuzi ya wengi make siasa inaweza kukujenga leo, na kesho ikakubomoa.
 
Makene

Makene

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
1,478
Likes
11
Points
135
Makene

Makene

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
1,478 11 135
zitto ni aibu kwa mapinduzi ya kweli, muelekeo wake kisiasa umechakachuliwa
 
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Messages
11,550
Likes
642
Points
280
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2008
11,550 642 280
Maelezo mazuri sana na yametulia.

Hivi kuna watu bado wanasema Zitto atagombea mwaka 2015? Hawa wakumbuke maneno aliyoyasema Nyerere kwa Waandishi wa habari wa Kenya walipomsema kuwa anataka kupindua serikali ya Kenya. Akili za kuambiwa changanyeni na za kwenu washiriki.

Kuhusu kumuadhibu, mhhhh!!!! Sidhani kama ni uamuzi mzuri sana. Tawi lisilozaa hukatwa na kutupwa ila mkono mchafu huoshwa na kukaushwa na tayari kutumika sehemu nyingine. Zitto si mtu wa kutupa pamoja na mapungufu yake ila Zitto ni kama GLASS za wine yaani ameandikwa kabisa "HANDLE WITH CARE." Sidhani kuna chama watakuwa tayari kumchukua na sanasana atachukuliwa na kuingizwa kwenye taasisi za Serikali ili asiwasumbue sana Serikali ya CCM. Ila kwa sasa sidhani CCM wanahofu tena na Zitto. Hofu yao kubwa iko kwa Mnyika na Tundu Lissu. Hivyo nina imani kuwa Zitto umaarufu wake utakuwa unapungua wenyewe kwa yeye mwenyewe kujimaliza na maamuzi au maneno yake yasiyokubalika na PIPOOO PAWAAA!!!!

Kuhusu kuomba Msamaha, mie sinunui. Mtu anaposema "kama nimewaudhi wengi......, samahani" hapa ndiyo kizizi cha fitina kipo. Mtu anayeomba kweli msahama, lazima kwanza aone kosa lake na akiri kuwa amekosea na ndipo hata bila ya kuomba msamaha, sisi tutasema kuwa "yamepita hayo BURAZA K. na sasa tuendelee na mengine....." Hii samahani yake ni kama kumaliza tu mjadala ili yaishe ila sidhani kweli anajutia kweli kosa lake. Na sisi tunabaki kusema "tutakuangalia kila hatua unayopiga Mkuu...."

Tuliona akina Masha wakitishia hadi watu kama akina Mengi, sasa wamefulia hadi wanaiba Vitasa na Mazulia ya offisi ya Mbunge wa Nyamagana. Aibu aibu hiyo. Kweli cheo ni dhamana.
 
N

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2009
Messages
1,315
Likes
113
Points
160
N

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2009
1,315 113 160
Nikupateje hoja na ufafanuzi wako ni murua,HITIMISHO LAKO si SAHIHI SANA! hatujengi umoja kwa kuadhibu kosa moja. Mhusika alishajieleza humu ndani vema, na yeye ni mtu mwenye akili TIMAMU, "HILI KALIELEWA VEMA". Haja ipo kwa viongozi wote kuwa na umoja wa maamuzi hasa pale wanapokuwa na mitazamo tofauti, ili kulindaumoja wa CDM. Hili ni kwa viongozi wa juu wote,na si ZITO pekee! Hoja hii ilishajadiliwa sana, na sioni haja ya kuiendeleza! CDM juuuuuuuuuuuuuuuuuu, peoples...............................umoja ni nguvu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mkuu, najua kwamba imejadiliwa sana si humu tu bali kwenye vichochoro vyote hapa nchini.

Kilichonisukuma kuingia jamvini ni pale niliposoma leo gazeti TAZAMA TANZANIA linalotoa picha kwamba Zitto anasukiwa zengwe la kuonewa.

Ninaiheshimu JF kwamba tunavyotoa comments zetu kama hivi waandishi wa habari waliomo humu wanahezishimu na sioni ubaya wakizitumia magazetini mwao kueleimisha umma ili kupingana na upuuzi unaonenezwa na wanahabari kama hawa wa TAZAMA TANZANIA ambao hadi leo hii wanaleta upotofu huu.

Kwa habari ya leo ni dhahiri mjadala wa Zitto haujatulia na juhudi ya kuelimisha ukweli lazima itumike kama hivi iwapo juhudi ya kueneza upotofu itaendelea hata kama ni baada ya miaka kadhaa.

Kuhusu adhabu nimekuwa makini kutumia neno uwajibikaji. Ukinisoma vizuri nimesema uwajibikaji ambao hata Zitto anaweza kuisaidia CHADEMA kwa kuwajibika.

Kuwajibika si lazima kupewa au kujipa adhabu ambayo sisi lazima tuijue. Najua katika hili CHADEMA wana njia nyingi za kulitimiza.
 
W

watarime

Senior Member
Joined
Oct 21, 2010
Messages
105
Likes
0
Points
0
W

watarime

Senior Member
Joined Oct 21, 2010
105 0 0

Salute kwa mchango mzuri,
Sisi watu wa mara tulikuwa tunampa heshima zito kama mzalendo lakini honestly speaking tangu alipo jiingiza kwny kamati ya ya JK chini ya Jaji Bomani huyu jamaa tumemuondoa akilini na kila cku tunampa chance ya kujirudi lakini inaonekana amepewa vinono na Mafisadi.

Anyway nasikia anajengewa Gorofa huko maeneo ya mbezi tangi bovu yawezekana jamaa katusaliti maana haiwezekani kila cku zitto anafanya usaliti usio na tija kwa taifa.

Huyu sio Zito wa Buzwagi labda yule alistafu siasa tukaletewa Jitu jingine!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Sn2139

Sn2139

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2010
Messages
828
Likes
9
Points
35
Sn2139

Sn2139

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2010
828 9 35
This guy has been critised enough now..... Enough is enough, now lets wait and see if he has changed, Am sure he said what he did kiliwauzi wengi na anaomba msamaha.... What else can he say nadhani sasa tugange yajayo... lets see zitto of 2011
It is not enough mama VOR, tunahitaji kujiridhisha juu ya viongozi wetu. Tumechoka kuahidiwa uongo, maisha bora..kumbe ni ya mke na watoto wake.

Mimi bado nina reservation na mtiririko wa matendo na maneno ya Mh Zito. Tuachane na hulka ya Wa-Tz ya kusamehe haraka na kusahau bila kupembua. Tunaweza kumsamehe kama yeye lakini siyo kama kiongozi. Uongozi ni jukumu linalobeba maisha ya watu na ustawi wa nchi. Kiongozi lazima ahukumiwe kwa matendo, maneno na kauli zake. Kumbuka Musa, kiongozi wa kwanza wa taifa la Israel alipokosa kama kiongozi akaadhibiwa kwa kuambiwa kuwa "Wewe hutaigia katika nchi ya ahadi, utakufa!"

Ni kweli Mh Zito, alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya wana JF, aliomba msamaha. Lakini kuna baadhi ya maswali yaliyokuwa critical aliulizwa na baadhi ya watu hakuyajibu. Maswali hayo yangeweza kutuonesha kama kweli ana toba ya kweli yenye utambuzi wa kweli juu ya kosa lake na madhara ya kosa hilo kwa jamii. Mimi nilifuatilia vizuri sana discussion yote hadi page ya 39, Mheshimiwa aliteleza kama samaki.

Huenda Mh Zito ana siri kubwa na lengo mahsusi lisilo na maslahi kwa chama na nchi. Mambo mengi amekuwa akiyafanya hayaoneshi kama ni mtu mwenye utambuzi, hekima ya kiongozi na msomi kama wengi wanavyodai. Naomba dada VOR usitulazimishe kutoa msamaha wa kijinga bila nafasi ya kutafakari vyema juu ya huyu mtu na wengine wanaoomba kupewa nafasi ya kutuongoza.
 
MartinDavid

MartinDavid

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2009
Messages
876
Likes
46
Points
45
MartinDavid

MartinDavid

JF-Expert Member
Joined May 22, 2009
876 46 45
Ni vema tu akaondoka muda huu bado mapema.. jamaa hana msimamo hata kidogo huyu...
 
S

Sheka

Senior Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
116
Likes
4
Points
35
S

Sheka

Senior Member
Joined Oct 4, 2010
116 4 35
It is not enough mama VOR, tunahitaji kujiridhisha juu ya viongozi wetu. Tumechoka kuahidiwa uongo, maisha bora..kumbe ni ya mke na watoto wake.

Mimi bado nina reservation na mtiririko wa matendo na maneno ya Mh Zito. Tuachane na hulka ya Wa-Tz ya kusamehe haraka na kusahau bila kupembua. Tunaweza kumsamehe kama yeye lakini siyo kama kiongozi. Uongozi ni jukumu linalobeba maisha ya watu na ustawi wa nchi. Kiongozi lazima ahukumiwe kwa matendo, maneno na kauli zake. Kumbuka Musa, kiongozi wa kwanza wa taifa la Israel alipokosa kama kiongozi akaadhibiwa kwa kuambiwa kuwa "Wewe hutaigia katika nchi ya ahadi, utakufa!"

Ni kweli Mh Zito, alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya wana JF, aliomba msamaha. Lakini kuna baadhi ya maswali yaliyokuwa critical aliulizwa na baadhi ya watu hakuyajibu. Maswali hayo yangeweza kutuonesha kama kweli ana toba ya kweli yenye utambuzi wa kweli juu ya kosa lake na madhara ya kosa hilo kwa jamii. Mimi nilifuatilia vizuri sana discussion yote hadi page ya 39, Mheshimiwa aliteleza kama samaki.

Huenda Mh Zito ana siri kubwa na lengo mahsusi lisilo na maslahi kwa chama na nchi. Mambo mengi amekuwa akiyafanya hayaoneshi kama ni mtu mwenye utambuzi, hekima ya kiongozi na msomi kama wengi wanavyodai. Naomba dada VOR usitulazimishe kutoa msamaha wa kijinga bila nafasi ya kutafakari vyema juu ya huyu mtu na wengine wanaoomba kupewa nafasi ya kutuongoza.
Dogo Zito tafadhali uonyesha kweli kujutia makosa, hebu tubu kutoka moyoni mwako uone km kweli utasakamwa, kimsingi km ww zito tumekusamehe ila kama kiongozi inabidi na wewe ujibu critical kama wana JF wanavyo critisise utetezi wako kama kiongozi.
 
Plato

Plato

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Messages
421
Likes
5
Points
33
Plato

Plato

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2010
421 5 33
asamehewe nini? Hii ni mara ya ngapi anafanya huu upuuzi? Haya mleeni,atakuja kuwa mkubwa kuliko chama kama jk.
 
lm317

lm317

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Messages
452
Likes
1
Points
0
lm317

lm317

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2009
452 1 0
Akae pembeni!
Atuonyeshe kujutia makosa akiwa nje kabisa ya CDM labda tutamfikiria!
 
Forum statistics

Threads 1,235,846
Members 474,742
Posts 29,238,336