mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,726
- 11,942
AiseeeKosa la Lissu ni KUTOKUFA!!!
AiseeeKosa la Lissu ni KUTOKUFA!!!
Hata ulimboka aliribiwa na ndio maana hata haikuwa na chuki kama sasaAngalia hizi kauli zako, ivi leo ukiitwa uthibishe haya utaleta ushahidi? Na kama ni kweli Jpm ndiye na serikali yake ndiyo walio mshambulia Lisu kwann leo watu mnataka jpm agalamie matibabu yake? Wakati shutuma mnaziweka wazi hivyo!
Ni mwendawazimu tu anayeweza kusema mtu aliyepigwa risasi 38 afuate taratibu za matibabu wakati yeye risasi moja tu hawezi kuihimili. What a Great Thinker! Risasi si peremende au korosho za kusema utakuwa unatafuna taratibu huku akifuata taratibu za tiba.who is Lisssu by the way?
1. Mlijinasibu kuwa kwa gharama yoyote mtasimamia matibabu.
2. Sheria sio kitu, Bali taratibu zinazosimamiwa na sheria ndio zinazoipa sheria maana. Kuna wakati MTU unapoteza haki zako za msingi unaposhindwa kufuata taratibu. Hili litabaki kuwa hivi tu, haliitaji mjadala.
3. ungeonekana great thinker kama ungekuja na hoja ya nini kifanyike. Ukizingatia huyu MTU amesha poteza haki kwa kushindwa kufuata taratibu.
Tuko pamoja mkuuExactly; nilitaka kuandika hivi hivi!
Ndo hivyo chifu!Aiseee
Ni mwendawazimu tu anayeweza kusema mtu aliyepigwa risasi 38 afuate taratibu za matibabu wakati yeye risasi moja tu hawezi kuihimili. What a Great Thinker! Risasi si peremende au korosho za kusema utakuwa unatafuna taratibu huku akifuata taratibu za tiba.
Nyie watu aliewaroga kafaLissu ni Mtanzania,Raia,ni kosa gani ambalo Lissu kafanya huwa najiuliza mpaka linasababisha Bunge na serikali ya Tanzania ziweke ngumu kumsaidia katika matibabu yake pamoja na kilio cha muda mrefu kutoka kwake na familia yake?
Lissu amefanya kosa ga
Kwakweli hata mimi naona hasira ya Mungu dhidi ya watesi na wauaji wa raia wasiokuwa na hatia kama Akwilina na David Mwangosi inachelewa sana. Ee Mungu wewe uketiye mahali palipo juu palipoinuka na miguu yako kukanyaga hulu chimi kwanini usiwaangamize watesi hawa kama ulivyofanya kwa Sodoma na Gomora. Tena Mungu wale walikuwa wanajinywea tu pombe zao, kula, kunywa, kusaza, kuoa na kuolewa lakini ulikasirika ukawaangamiza. Sasa hawa wanaotesa watu kwa kuwapiga risasi raia, kuua na kupoteza watu unawaacha wa nini?! Mungu waangamize hao tena kwa mateso makuu kama kuwatupa kwenye tanuru la moyo kama Shedrack na Abernago. Nimeomba hayo kwa jina lako kuu, Ameni!Wakati mwingine unawaza, kisasi cha Mungu kwa watesi na wauaji huchukua muda gani, maana km anawachelesha sana.
Hii inanikumbusha ule wimbo: ".....ukiwaangalia usoni ni kama watu....."Nyie watu aliewaroga kafa
Mmesahau mlimkimbiza Nairobi kwa kusema akipelekwa muhimbili atakufa?
Pia serikali ilipoiomba familia imtibie lissu wakakataa na chadema kwa mbwembwe wakaanzisha michango
Michango imeliwa sasa mbatafuta mchawi
Andika tu mkuu usiogopeKosa lake linajulikana ila kwa sheria hii ya makosa ya mitandao kuliandika hapa labda uwe nje ya nchi. Lazima utasakwa tu.
Wewe naona roho iliyo ndani yako ni roho kama ya MCHAWI.Una matatizo wewe siyo bure, unapoteza muda wako kumpigania snitch ambaye kila Mwisho wa mwezi zaidi ya milioni 10 inaingia kwenye akaunti yake, hapo hapo 2020 atalipwa zaidi milioni 200 za kumalizia Ubunge, achilia mbali mshahara wa chadema kama mwajiriwa wa Chama na marupurupu mengine ktk law firms za kifisadi na tena amelazwa Hospitalini Ulaya, hata Mungu hawezi kuwasamehe na laana nyingine ni za kujitakia, embu funga safari nenda Mwananyamala hosp. uone mateso wagonjwa wanayopata halafu ujitafakari mara mbili, kati ya Tundu Lisu na hao wagonjwa yupi anahitaji msaada?
Nina uhakika una ndugu zako wengi ambao hata wangehitaji msaada wa Serikali klk Tundu Lisu, acha ujinga!
Tatizo kosa halijawahi kusemwa humu JF na naomba nisiwe wa kwanza. Maana hawatahitaji 7m au kifungo cha miaka 3, wataku Gwandalize tu.Andika tu mkuu usiogope
Ww
Wewe naona roho iliyo ndani yako ni roho kama ya MCHAWI.
SWALI NI KAKOSA NINI LISU, JIBU HILO!!!!
Msaada?'???!!!!Kosa la Tundu Lissu ni nini?
Nilikuwa miongoni mwa waandishi wa kwanza kabisa kufanya mahojiano na Tundu Lissu(Mbunge),toka nimeanza kazi ya uandishi wa habari nimefanya mahojiano na viongozi wengi wakubwa nchini Tanzania na hata kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.
Mahojiano yote niliyafurahia sana kwani ilikuwa ni ndoto yangu kuhakikisha nawafikia viongozi wakuu na kuzungumza nao,lakini mahojiano na Tundu Lissu akiwa Kitandani Katika hospital ya Nairobi Nchini Kenya ndiyo mahojiano magumu niliyowahi yafanya.
Kwa nini basi?
Kwa sababu nilifanya mahojiano na mtu ambaye alikuwa mgonjwa na hajapona majeraha yake,alikuwa amedhoofu na kutia huruma,kuzipata dakika 47 za mahojiano ilikuwa kazi ngumu kwani kuna wakati nilihisi namsababishia maumivu.
Lissu aliumia sana,Lissu ni Mtanzania,Lissu ni kiongozi,tangu nifanye nae mahojiano nikiwa mwandishi wa kwanza kutoka Tanzania kuzungumza nae baada ya majeraha,Lissu amekuwa akilalamika kuwa Serikali ya Tanzania haijawahi msaidia hata senti,inastusha,inashangaza na inatia huruma.
Lissu ni Mtanzania,Raia,ni kosa gani ambalo Lissu kafanya huwa najiuliza mpaka linasababisha Bunge na serikali ya Tanzania ziweke ngumu kumsaidia katika matibabu yake pamoja na kilio cha muda mrefu kutoka kwake na familia yake?
Lissu amefanya kosa gani lisilo sameheka?maana nimemsikia zaidi ya mara mbili Spika Job Ndugai akisema Lissu hakufuata utaratibu ndiyo maana Bunge halikumsaidia,kweli yaweza kuwa sababu ya kumuacha Lissu bila msaada?
Najiuliza ni Kosa gani alilofanya Lissu mpaka linasababisha anakosa msaada wa matibabu kama anavyolia mwenyewe?
Hili kosa la Lissu lisilohitaji msamaha na kuambiwa hatasaidiwa matibabu mpaka afuate utaratibu ni lipi?ni kweli kosa la Lissu ni kutofuata utaratibu wa matibabu?
Je huo utaatibu ni msahafu usiyohitaji kuongezewa wala kupunguziwa kitu?katika hali kama ile aliyokuwa nayo Lissu kweli tubaki na msimamo ule ule kuwa Lissu hakufuata utaratibu?
Tumtazame Lissu kwa jicho la binadamu na Raia wa Tanzania anayehitahi msaada,tusimtazame Lissu kwa jicho la Mbunge anayetakiwa kufuata utaratibu kama Spika Job Ndugai alivyosema.
Serikali imsaidie Lissu kwa upendo ule ule ambao tumekuwa tunaona serikali ikiuonesha kwa watanzania ambao wanauhitaji wa msaada wa ghamara za matibabu.
Tuliuona Upendo wa serikali yetu kuhakikisha Raia wake wanapata matibabu kwa Raia wengi,tunakumbuka upendo wa hali ya juu kwa Marehemu King Majuto,Marehemu Sajuki,na jana tumesikia na kuona upendo wa hali ya juu wa serikali yetu kusaidia matibabu ya Kaka Ruge Mutahaba.
Binafsi najiuliza kwa nini Bunge na Serikali kwa Lissu upendo huu wa Serikali kwa watu wake unaondoka?Tundu,mwana wa Mugwai kafanya dhambi ipi inayomfanya asipate msaada wa Bunge na serikali?
Lissu anateseka,Lissu anaumia,Mke wake anateseka,familia na ndugu wanalia,Bunge na serikali zirejeshe moyo nyuma zimsaidie Lissu katika matibabu yake.
Mwenyezi Mungu alituwekea amri nyingi sana,lakini Amri kuu ni Upendo na Upendo huanza kwa kuwa na moyo wa kusamehe na kusahau kama unaamini au ni kweli umekosea.
Kama Kosa alilofanya Lissu lilikuwa ni kutokufuata utaratibu,siamini kama kosa hili adhabu yake ni kutokusamehewa.
Mwenyezi Mungu alituumba kwa sura na mfano wake,mfano wa mkuu ambao ni ishara ya kuwa tumeumbwa na Mungu ni kuwa na moyo wa Upendo.
Bunge na serikali kosa la Lissu la kutokufuata utaratibu wa matitabu kweli halisameheki?Bunge na Serikali,sikieni kilio cha Lissu,sikieni Kilio cha familia yake.
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.
Anaandika
Dotto Bullendu....
Aombwe Mkulu wakati hiyo ni stahiki yake??Doto Bulendu bro. huwa pale ninapopata muda nafuatilia na napenda sana unapoongoza vipindi au mijadala pale Startv! Hongera sana. Umeongea kwa uchungu sana kama mtanzania mwingine mwenye mapenzi na Lissu..
Ninachojua mimi kama mtanzania, ilikuwani mihemko ya kisiasa ndiyo imezaa haya leo hii na kuanza kuonekana kwamba Tundu ametelekezwa na bunge ama serikali. Watanzania tumekengeuka, hatuelimishani mambo mema siku hizi.
Kuna ngazi za matibabu na utaratibu wake, kwa.mfano ukitibiwa ngazi ya zahanati na tatizo likawa chini ya uwezo wa kituo, basi mgonjwa anapewa refferal leter kwenda ngazi ya juu kama Hospital level. Pia na ngazi hiyo ikishindwa kutoa huduma kwa manufaa ya mgonjwa pia hupelekwa ngazi ya juu yake mpaka inafika ngazi ya hospitali ya taifa. Na kama hapo itaonekana kama tatizo bado lipo nje yao ndipo hao hutoa kibali cha kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Ombi langu na mimi pia labda tuungane watanzani wot kumwomba mh. Rais maana ndiye yeye mwenye mamlaka zaidi, afanye msaada kama anavyofanya kwa watanzania wengine.
tueleze na zile mil.50 alizotoa jiwe kumpa huyo mkurugenzi wa CMG kwa matibabu . ndio tuseme ruge hana huo uwezo au.....????Una matatizo wewe siyo bure, unapoteza muda wako kumpigania snitch ambaye kila Mwisho wa mwezi zaidi ya milioni 10 inaingia kwenye akaunti yake, hapo hapo 2020 atalipwa zaidi milioni 200 za kumalizia Ubunge, achilia mbali mshahara wa chadema kama mwajiriwa wa Chama na marupurupu mengine ktk law firms za kifisadi na tena amelazwa Hospitalini Ulaya, hata Mungu hawezi kuwasamehe na laana nyingine ni za kujitakia, embu funga safari nenda Mwananyamala hosp. uone mateso wagonjwa wanayopata halafu ujitafakari mara mbili, kati ya Tundu Lisu na hao wagonjwa yupi anahitaji msaada?
Nina uhakika una ndugu zako wengi ambao hata wangehitaji msaada wa Serikali klk Tundu Lisu, acha ujinga!