Kosa la Tundu Lissu ni nini?

Kosa la Tundu Lissu ni nini?

Tundu Lisu anaweza kujipigania achana naye na wala hahitaji msaada wako, nina uhakika una ndugu na jamaa wengi ambao hawajiwezi na wangehitaji msaada wako zaidi, unapoteza muda kumpigania mtu anayetibiwa Ulaya tena yuko huko na Familia yake na siajabu hata jina lako halijui?
Mhe Barbarosa yaelekea Lisu humpendi kabisaaa. Daily nikipitia thread kumuhusu, wewe humpinga. Nilitegemea kwa hiii busara na hekima ya kiubinadam ingekuongoza kupitia tu na kutocomment ili usiwatoe kwenye mstari waliao kwa ajili yake, kwa kuwa NAO watahamia kwako na kuharibu mtiririko.
 
Kosa la Tundu Lissu ni nini?

Nilikuwa miongoni mwa waandishi wa kwanza kabisa kufanya mahojiano na Tundu Lissu(Mbunge),toka nimeanza kazi ya uandishi wa habari nimefanya mahojiano na viongozi wengi wakubwa nchini Tanzania na hata kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.

Mahojiano yote niliyafurahia sana kwani ilikuwa ni ndoto yangu kuhakikisha nawafikia viongozi wakuu na kuzungumza nao,lakini mahojiano na Tundu Lissu akiwa Kitandani Katika hospital ya Nairobi Nchini Kenya ndiyo mahojiano magumu niliyowahi yafanya.

Kwa nini basi?

Kwa sababu nilifanya mahojiano na mtu ambaye alikuwa mgonjwa na hajapona majeraha yake,alikuwa amedhoofu na kutia huruma,kuzipata dakika 47 za mahojiano ilikuwa kazi ngumu kwani kuna wakati nilihisi namsababishia maumivu.

Lissu aliumia sana,Lissu ni Mtanzania,Lissu ni kiongozi,tangu nifanye nae mahojiano nikiwa mwandishi wa kwanza kutoka Tanzania kuzungumza nae baada ya majeraha,Lissu amekuwa akilalamika kuwa Serikali ya Tanzania haijawahi msaidia hata senti,inastusha,inashangaza na inatia huruma.

Lissu ni Mtanzania,Raia,ni kosa gani ambalo Lissu kafanya huwa najiuliza mpaka linasababisha Bunge na serikali ya Tanzania ziweke ngumu kumsaidia katika matibabu yake pamoja na kilio cha muda mrefu kutoka kwake na familia yake?

Lissu amefanya kosa gani lisilo sameheka?maana nimemsikia zaidi ya mara mbili Spika Job Ndugai akisema Lissu hakufuata utaratibu ndiyo maana Bunge halikumsaidia,kweli yaweza kuwa sababu ya kumuacha Lissu bila msaada?

Najiuliza ni Kosa gani alilofanya Lissu mpaka linasababisha anakosa msaada wa matibabu kama anavyolia mwenyewe?

Hili kosa la Lissu lisilohitaji msamaha na kuambiwa hatasaidiwa matibabu mpaka afuate utaratibu ni lipi?ni kweli kosa la Lissu ni kutofuata utaratibu wa matibabu?

Je huo utaatibu ni msahafu usiyohitaji kuongezewa wala kupunguziwa kitu?katika hali kama ile aliyokuwa nayo Lissu kweli tubaki na msimamo ule ule kuwa Lissu hakufuata utaratibu?

Tumtazame Lissu kwa jicho la binadamu na Raia wa Tanzania anayehitahi msaada,tusimtazame Lissu kwa jicho la Mbunge anayetakiwa kufuata utaratibu kama Spika Job Ndugai alivyosema.

Serikali imsaidie Lissu kwa upendo ule ule ambao tumekuwa tunaona serikali ikiuonesha kwa watanzania ambao wanauhitaji wa msaada wa ghamara za matibabu.

Tuliuona Upendo wa serikali yetu kuhakikisha Raia wake wanapata matibabu kwa Raia wengi,tunakumbuka upendo wa hali ya juu kwa Marehemu King Majuto,Marehemu Sajuki,na jana tumesikia na kuona upendo wa hali ya juu wa serikali yetu kusaidia matibabu ya Kaka Ruge Mutahaba.

Binafsi najiuliza kwa nini Bunge na Serikali kwa Lissu upendo huu wa Serikali kwa watu wake unaondoka?Tundu,mwana wa Mugwai kafanya dhambi ipi inayomfanya asipate msaada wa Bunge na serikali?

Lissu anateseka,Lissu anaumia,Mke wake anateseka,familia na ndugu wanalia,Bunge na serikali zirejeshe moyo nyuma zimsaidie Lissu katika matibabu yake.

Mwenyezi Mungu alituwekea amri nyingi sana,lakini Amri kuu ni Upendo na Upendo huanza kwa kuwa na moyo wa kusamehe na kusahau kama unaamini au ni kweli umekosea.

Kama Kosa alilofanya Lissu lilikuwa ni kutokufuata utaratibu,siamini kama kosa hili adhabu yake ni kutokusamehewa.

Mwenyezi Mungu alituumba kwa sura na mfano wake,mfano wa mkuu ambao ni ishara ya kuwa tumeumbwa na Mungu ni kuwa na moyo wa Upendo.

Bunge na serikali kosa la Lissu la kutokufuata utaratibu wa matitabu kweli halisameheki?Bunge na Serikali,sikieni kilio cha Lissu,sikieni Kilio cha familia yake.

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.

Anaandika

Dotto Bullendu....
kosa la Lissu ni kuwa sahihi wakati serikali haipo sahihi........
 
Risasi 38; zimevunja vunja mifupa tu lakini hazikugusa mshipa mkubwa wowote wa damu ili ivuje kwa kasi na Lissu apoteze maisha instantly hata kabla ya kufika General Hosp.

Risasi 38 zikapenya lakini cha ajabu hakuna hata moja iliyopitia mishipa ya fahamu (nerves) ili hata kama akipona baadhi ya viongo vyake visifanye kazi. ( vipaparize). Moja ikapenya na imetulia kwenye uti wa mgongo... Sasa jiulize uti wa mgongo una nerves ngapi? Lakini risasi imepenya na ipo humo bila madhara.

Hayo yote hayakuwezekana; Tumesoma unabii uliofanyika miaka mingi sana katika vitabu vitakatifu wakati ule mwenyezi Mungu alipokuwa karibu mno na wanadamu - huu pia ni unabii; Mungu alitaka kusema nasi kupitia shambulio hili. Kwa akili ya kawaida kabisa Lissu alikuwa haponi.

Hapo ndipo unafikia hatua ya kusema hapa duniani hatujajileta na hii dunia haijajiumba!!

Mtoa mada wala usiwe na wasiwasi na fedha za matibabu; aliyemponya lazima atamsimamia; na so far anamsimamia kweli.
mkuu kuna watu mpk leo hawaamini kama shedraka,meshaka na abednego walitupwa kwenye tanuru ya moto lkn hawakuungua hata unywele..............

Biblia inasema kwa ukali wa ule moto, watu waliokua wamewashika kina shedraka na wenzake ili kuwatupa kwenye tanuru inayowaka walikufa!

lkn ajabu shedraka na wenzake hata unywele wake haukuunguzwa!

nina amini mpk leo wale vijana waliommiminia risasi Lissu baadhi yao wamefariki, lkn Lissu bado yupo!

hio ni kazi ya Yehovah Mungu Muumba wa vyote vilivyopo,vitakavyokuepo,vinavyoonekana na visivyoonekana
 
.....wako viongoza,kwa kuwatazama tu, unawagundua ni wazalendo, wana maono, hawatetereki, wana akili, ni sauti ya kweli ya wanyonge, wana mvuto wa kiuongozi. Mh Lissu, ndiye mwenye hizo traits. Sisemi wengine hawapo. Bali, yeye amejitokeza kama front liner. Mtu huyu ana heshima ya pekee kwa taifa hili. Mtu huyu hakupaswa kuchabangwa risasi kama simba aliyeingilia makazi ya watu. Mtu huyu, alipaswa kutumiwa kama zawadi pamoja na kwamba ana weakness zake. Lissu ni ZAWADI, na ndio Maana Mungu amemponya. Mungu amemponya ili ku reveal kuwa binadamu mwenye mipango ovu, kwake si kitu. Ona maajabu mtu anakufa kwa kupigwa na punje ya mhindi, sembuse risasi 38?. Huyu mtu naamini hayuko upande wa shetani insuch....amebeba maono. Ni muda muafaka wa wale waliomfanyia umafia. Kutubu na kuvipiga vifua vyao. Ni kosa kusema eti, alikuwa hash ktk kuwasilisha hojazake. Ujinga!. Hata yesu alipindua pindua meza pale hekaluni kwa hasira baada ya kuchukizwa, hii haimaanishi kuwa yesu hakuwa mtu safi. Sometimes ni lazima ukere ili ueleweke, ila usikere ili usieleweke.
 
Una matatizo wewe siyo bure, unapoteza muda wako kumpigania snitch ambaye kila Mwisho wa mwezi zaidi ya milioni 10 inaingia kwenye akaunti yake, hapo hapo 2020 atalipwa zaidi milioni 200 za kumalizia Ubunge, achilia mbali mshahara wa chadema kama mwajiriwa wa Chama na marupurupu mengine ktk law firms za kifisadi na tena amelazwa Hospitalini Ulaya, hata Mungu hawezi kuwasamehe na laana nyingine ni za kujitakia, embu funga safari nenda Mwananyamala hosp. uone mateso wagonjwa wanayopata halafu ujitafakari mara mbili, kati ya Tundu Lisu na hao wagonjwa yupi anahitaji msaada?

Nina uhakika una ndugu zako wengi ambao hata wangehitaji msaada wa Serikali klk Tundu Lisu, acha ujinga!
ficha upumbavu wako!
 
Hata mimi nimejibu kuhusu snitch Tundu Lisu labda haujaelewa tu!
Wewe utakuwa ulifeli kidato cha nne kwasababu hukuzingatia kusoma instructions kabla ya kuanza kujibu maswali, zero on the paper justifies zero on the brain.
 
Sio kosa, sema makosa, Tundu Lisu amekuwa akifanya yanayoitwa makosa kila mara tena kwa kujirudiarudia pasipo woga nje na ndani ya bunge, hadharani ktk vyombo mbalimbali vya habari na hata ktk mitandao ya kijamii pasipo kujali, ni makosa sana tena sana kuwa MKOSOAJI MSEMA KWELI DHIDI YA UTAWALA NA WATAWALA HASA WA NCHI ZA KIAFRIKA HUSUSANI INJI YETU.
 
Unajua kuna wengine uwa hawaoni mbali. Hivi miaka 10 ijayo Lisu kawa rais hawa wanaomkatalia kumpa pesa za matibabu watakuwa wapi?? Unajua mungu huwa anayo maksudi yake, Miaka 50 mbele mtoto wa Lisu kawa rais unategemea familia ya Magufuli au Ndugai watakuwa wapi?? Halafu ukute wanaroho ya kulipiza visasi kama roho ya Magufuli. Leo Magufuli anatoa pesa kwa Ruge mara kwa mcheza filamu wakati Lisu yupo Kitandani mwaka na. Na alietaka kumuua ni Magufuli. Ni mtanzania mbumbu tu ambaye aamini kuwa alietaka kumuua LISU NI MAGUFULI. MAGUFULI NI MUUAJI NA YEYE MWISHO WAKE ATAUWAWA KWA RISASI HAKUNA ALIEKUWA NA ULINZI KAMA SADDAM NA GADAFFI LKN WALIUWAWA. MAGUFULI HATA AKILINDWA NA JESHI ZIMA ILA SIKU YAKE IPO INAKUJA
Tulisha zoea porojo zenu.
 
Rais wangu ziangalie na issues za jamii yako ni kweli tumechelewa sana ila nchi sio miundo mbinu peke yake angalia watu wako wanahali ngumu sana ongeza mishahara weka kodi rafiki maisha ya wananchi masikini na wanyonge yaboreshe utaacha alama na kukumbukwa kwa mazuri
 
Doto Bulendu bro. huwa pale ninapopata muda nafuatilia na napenda sana unapoongoza vipindi au mijadala pale Startv! Hongera sana. Umeongea kwa uchungu sana kama mtanzania mwingine mwenye mapenzi na Lissu..

Ninachojua mimi kama mtanzania, ilikuwani mihemko ya kisiasa ndiyo imezaa haya leo hii na kuanza kuonekana kwamba Tundu ametelekezwa na bunge ama serikali. Watanzania tumekengeuka, hatuelimishani mambo mema siku hizi.

Kuna ngazi za matibabu na utaratibu wake, kwa.mfano ukitibiwa ngazi ya zahanati na tatizo likawa chini ya uwezo wa kituo, basi mgonjwa anapewa refferal leter kwenda ngazi ya juu kama Hospital level. Pia na ngazi hiyo ikishindwa kutoa huduma kwa manufaa ya mgonjwa pia hupelekwa ngazi ya juu yake mpaka inafika ngazi ya hospitali ya taifa. Na kama hapo itaonekana kama tatizo bado lipo nje yao ndipo hao hutoa kibali cha kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Ombi langu na mimi pia labda tuungane watanzani wot kumwomba mh. Rais maana ndiye yeye mwenye mamlaka zaidi, afanye msaada kama anavyofanya kwa watanzania wengine.
Keshapona ndo atoe msaada wanini sasa, watanzania hatuhitaji Tena msaada wa watawala, aendelee kuwasaidia wasanii hao hao....
 
Una matatizo wewe siyo bure, unapoteza muda wako kumpigania snitch ambaye kila Mwisho wa mwezi zaidi ya milioni 10 inaingia kwenye akaunti yake, hapo hapo 2020 atalipwa zaidi milioni 200 za kumalizia Ubunge, achilia mbali mshahara wa chadema kama mwajiriwa wa Chama na marupurupu mengine ktk law firms za kifisadi na tena amelazwa Hospitalini Ulaya, hata Mungu hawezi kuwasamehe na laana nyingine ni za kujitakia, embu funga safari nenda Mwananyamala hosp. uone mateso wagonjwa wanayopata halafu ujitafakari mara mbili, kati ya Tundu Lisu na hao wagonjwa yupi anahitaji msaada?

Nina uhakika una ndugu zako wengi ambao hata wangehitaji msaada wa Serikali klk Tundu Lisu, acha ujinga!

Mwacheni Tundu Lissu ajiuguze huku akisubiri hayo mafao yake....

Hata hivyo, Kwanini sasa msi - concentrate kuwahudumia hao wa Mwananyamala Hospital wanaoteseka?

Au tukuulize swali hilo hilo la...

Hivi wagonjwa wa hospitali ya Mwananyamala na zingine zote za umma wamekosea nini hata watelekezwe na serikali na kuendelea kuteseka kwa kukosa huduma bora za matibabu???
 
Una matatizo wewe siyo bure, unapoteza muda wako kumpigania snitch ambaye kila Mwisho wa mwezi zaidi ya milioni 10 inaingia kwenye akaunti yake, hapo hapo 2020 atalipwa zaidi milioni 200 za kumalizia Ubunge, achilia mbali mshahara wa chadema kama mwajiriwa wa Chama na marupurupu mengine ktk law firms za kifisadi na tena amelazwa Hospitalini Ulaya, hata Mungu hawezi kuwasamehe na laana nyingine ni za kujitakia, embu funga safari nenda Mwananyamala hosp. uone mateso wagonjwa wanayopata halafu ujitafakari mara mbili, kati ya Tundu Lisu na hao wagonjwa yupi anahitaji msaada?

Nina uhakika una ndugu zako wengi ambao hata wangehitaji msaada wa Serikali klk Tundu Lisu, acha ujinga!
Hili ni povu la chuki iliyokujaa moyoni bwege wewe
 
who is Lisssu by the way?
1. Mlijinasibu kuwa kwa gharama yoyote mtasimamia matibabu.

2. Sheria sio kitu, Bali taratibu zinazosimamiwa na sheria ndio zinazoipa sheria maana. Kuna wakati MTU unapoteza haki zako za msingi unaposhindwa kufuata taratibu. Hili litabaki kuwa hivi tu, haliitaji mjadala.

3. ungeonekana great thinker kama ungekuja na hoja ya nini kifanyike. Ukizingatia huyu MTU amesha poteza haki kwa kushindwa kufuata taratibu.
Uhai wa Lissu unawasumbua kichwa wauwaji wakubwa nyinyi, na Hafi kwa taarifa yenu...
 
Kosa la lissu ni kuisema bombaladiya ya mkuu
Ila jk hakua anampenda kabisa lissu na hakuwahi kumpenda ila mwisho wa siku hakuwahi hata kumteka kwa miaka yote iyo kaja mzee hata miaka mi3 haijaisha akataka kumrestisha in peace aseee
 
Kosa la Lisu ni kupinga juhudi badala ya kuunga mkono kama kina Mwita.
 
Back
Top Bottom