Kodi ni pesa za watanzania wote hata kama mwenye dhamana ya kuzihifadhi ni mmoja. Hapaswi kupigiwa magoti kama vile anatoa pesa ya baba yake. Tunaaibishwa mbele ya jumuia ya kimataifa jinsi tulivyo na tabia za wanyama na kuwa hatujafikia hatua ya binadamu mwenye akili.Doto Bulendu bro. huwa pale ninapopata muda nafuatilia na napenda sana unapoongoza vipindi au mijadala pale Startv! Hongera sana. Umeongea kwa uchungu sana kama mtanzania mwingine mwenye mapenzi na Lissu..
Ninachojua mimi kama mtanzania, ilikuwani mihemko ya kisiasa ndiyo imezaa haya leo hii na kuanza kuonekana kwamba Tundu ametelekezwa na bunge ama serikali. Watanzania tumekengeuka, hatuelimishani mambo mema siku hizi.
Kuna ngazi za matibabu na utaratibu wake, kwa.mfano ukitibiwa ngazi ya zahanati na tatizo likawa chini ya uwezo wa kituo, basi mgonjwa anapewa refferal leter kwenda ngazi ya juu kama Hospital level. Pia na ngazi hiyo ikishindwa kutoa huduma kwa manufaa ya mgonjwa pia hupelekwa ngazi ya juu yake mpaka inafika ngazi ya hospitali ya taifa. Na kama hapo itaonekana kama tatizo bado lipo nje yao ndipo hao hutoa kibali cha kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Ombi langu na mimi pia labda tuungane watanzani wot kumwomba mh. Rais maana ndiye yeye mwenye mamlaka zaidi, afanye msaada kama anavyofanya kwa watanzania wengine.
Suala la kumnyima matibabu ni fedheha kubwa.
Sent using Jamii Forums mobile app