Kosa la kutobadilisha jina la African Barrick Gold na Acacia kama lipo faini yake ni elfu moja tu!

Mwenye makosa ni accasia au waliokuwa wakilamba kodi ya accasia huku wakiwa na wanajua wanashirikiana na kampuni isiyosajiliwa?
Acacia kwa mujibu wa kifungu cha 324 cha sheria ya Makampuni haipaswi kusajiliwa bali kubadilisha jina tu na kukusanya kodi ni sahihi kabisa kwa sababu kampuni tanzu ambayo ni African Barrick Gold imesajiliwa na hakuna kujisajili mara mbili kwa shughuli ileile labda wamiliki wauze au kufilisiwa mazingira ambayo hayapo kwenye hili suala
 
Pamoja na washauri wao wote na wapenzi wao na washika bendera wao, Acacia wameshindwa kukumbuka kitu kidogo sana kama kusajili kampuni au kubadilisha jina. Hii inaweza hata kuwanyima haki ya kushtaki popote pale duniani. Ndio maana Magufuli anasema wasisajiliwe mpaka watubu na kukubali makosa yao
Mawakala wao wako kazini, wataipata fresh mwaka huu, hehe..
 
Tatizo la kudadia sheria bila kuelewa sheria ya makampuni ya cap 212 ilishafutwa bali kuna sheria namba 12 ya makampuni 2002 ambayo inakanuni mpya nso maana hata ada za usajiri zilishabasirika hata taratibu zake bia nazo ni tofauti,tafadhali jielimishe kusoma sheria zinazotumika
Ni hiyo hiyo
 
Wewe Acacia hawatakuchukua. Lissu amekula na bado taarifa ya makinikia haijawaacha salama.
99c0ed69f562954d26c42a41e4e03e1a.jpg
 
Tatizo la kudadia sheria bila kuelewa sheria ya makampuni ya cap 212 ilishafutwa bali kuna sheria namba 12 ya makampuni 2002 ambayo inakanuni mpya nso maana hata ada za usajiri zilishabasirika hata taratibu zake bia nazo ni tofauti,tafadhali jielimishe kusoma sheria zinazotumika
Acha kupotosha sheria ni sura ya 212(2002)
 
Mmiliki ni African Barrick Gold na menejimenti kaikabidhi kwa Acacia sasa mwajiriwa hujisajili au hubadili jina tu kama alizembea mdai buku lakini huwezi kumfilisi au kumzuia kufanya shughuli zake
Mkuu hakuna lugha utakayotumia ueleweke na hawa watu ambao wameaminishwa na kuamini kwamba, hiyo kampuni haina usajili na haina leseni. Wanachotaka kusikia ni kwamba Accacia wakiri kwamba waliiba na warudishe matrilioni walioiba ndiyo wasajiliwe. Hivyo ndivyo JPM alivyooagiza, kwa hiyo pamoja na jitihada zako za kuleta sheria na kuelezea bado wapo ambao hawatakuelewa.
 
Mmiliki ni African Barrick Gold na menejimenti kaikabidhi kwa Acacia sasa mwajiriwa hujisajili au hubadili jina tu kama alizembea mdai buku lakini huwezi kumfilisi au kumzuia kufanya shughuli zake
Unapo unganisha kampuni au kuuza kampuni ambayo inajihusisha na uchumi wa nchi husika (economical interest) lazima mwenye nchi ajulishwe tena kupitia njia halali. Hawa jamaa wamepeana huko huko na hawakufuata taratubi zilizo wekwa wakitegemea kama hakuna wa kuwauliza kitu.
 
Pamoja na washauri wao wote na wapenzi wao na washika bendera wao, Acacia wameshindwa kukumbuka kitu kidogo sana kama kusajili kampuni au kubadilisha jina. Hii inaweza hata kuwanyima haki ya kushtaki popote pale duniani. Ndio maana Magufuli anasema wasisajiliwe mpaka watubu na kukubali makosa yao
Sasa hapo anayeonekana mpumbafu ni nani kama sio serikali?? Yani mtu anachimba madini kila siku kumbe hajasajiliwa??
 
kupelwa waweza,ongelea kidogo kuhusu hio sheria mpya?
Vipi,hiyo faini ya kutokubadilisha jina,kwa sheria ya sasa,faini ni shilingi ngapi?
 
Sasa hapo anayeonekana mpumbafu ni nani kama sio serikali?? Yani mtu anachimba madini kila siku kumbe hajasajiliwa??
Ndio tatizo la watu tuliowaamini kulinda lago kuu walirubuniwa wakatusaliti. Lakini askari kabadilishwa na huyu askari harubuniwi hata kwa kipande cha dhahabu.
 
Back
Top Bottom