Danny Jully
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 4,416
- 3,860
Sasa mkuu wakishachenjua dhahabu huo mchanga waurudishe tena nchini? Tambua kwamba yale ni mabaki baada ya dhahabu( pure gold) kutolewa. Kiasi kinachabaki kwenye huo mchanga hakuna kinu( smelter) hapa nchini ya kuichenjua na ndio maana wakaruhusiwa kupeleka hayo tunayoita makinikia ambayo yana madini mengine huko wanakojua wao wakachenjue.Hapana, wameruhusiwa kucheguwa dhahabu tu, na sio madini mengine. Hata wao wanajuwa hilo na ndio Maana hawajatoa kauli kukataa kama wanapata zaidi ya dhahabu. Mkataba ni mibovu nakubali, lakini kama na wao ni waaminifu kwanini mpaka wakakataa mkuu wa mkoa au mtu yoyote wa serikali hata kuona kilicho ndani ya ndege wanazosafirisha dhahabu nje ya nchi. Mkataba mibovu kisiwe kigezo cha kufuta dhambi zao za nyuma. Wamekwepa kodi, watoa taarifa za uwongo, wamedanganya hata kiwango cha mchanga wanchosafirisha kwenda nje.
Elewa jambo moja mkuu, kama wasingeruhusiwa kupeleka hayo makinikia huko wanakojua wao, yangebaki hapa nchini na wala leo hii habari tunayoijadili isingekuwepo. Labda tungekuwa tunajadili namna serikali itavyojenga hicho kinu( smelter) ili hayo makanikia tuyachenjue wenyewe.