Kosa la kutobadilisha jina la African Barrick Gold na Acacia kama lipo faini yake ni elfu moja tu!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
187,380
2,000
Tumesikia Acacia haijasajiliwa lakini kampuni mama African Barrick Gold imesajiliwa.

Kusajiliwa kwa African Barrick Gold kunaiondolea Acacia umuhimu wa kusajiliwa mara ya pili bali kubadilisha jina kutoka African Barrick Gold na kuwa Acacia.

Kama hilo halijafanyika ni kosa la kwanza na adhabu yake ni kulipa faini ya Tshs 1,000/= wakirudia watatakiwa kila siku kosa linaendelea walipe faini ya Tshs 5,000/= ambayo nina uhakika Barrick hawana bifu na hilo. Kifungu cha 324 & 327 vya CAP 212 vya sheria ya makampuni ndivyo vinavyotamka

Kichekesho ni kutoitofautisha African Barrick Gold na Acacia hivyo kuja na khoja za kijiweni eti ni kampuni mbili tofauti.

Mwanzisha khoja ni kampuni mbili tofauti ndiye mwenye jukumu la kutoa nyaraka za lini, wapi na kwa kiasi gani Acacia iliinunua African Barrick Gold.

Someni sheria ya kuanzisha makampuni nchini Cap 212 walifuta na kufuta BUKU kwa sheria ya no. 12.

Ushauri

Tudai BUKU kwa sheria iliyofutwa kwani hii mpya hakuna adhabu kwa kuchelewesha kubadilisha jina!
 
Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
5,637
2,000
Pamoja na washauri wao wote na wapenzi wao na washika bendera wao, Acacia wameshindwa kukumbuka kitu kidogo sana kama kusajili kampuni au kubadilisha jina. Hii inaweza hata kuwanyima haki ya kushtaki popote pale duniani. Ndio maana Magufuli anasema wasisajiliwe mpaka watubu na kukubali makosa yao
 
kupelwa

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
1,066
1,500
Tumesikia Acacia haijasajiliwa lakini kampuni mama African Barrick Gold imesajiliwa.

Kusajiliwa kwa African Barrick Gold kunaiondolea Acacia umuhimu wa kusajiliwa mara ya pili bali kubadilisha jina kutoka African Barrick Gold na kuwa Acacia.

Kama hilo halijafanyika ni kosa la kwanza na adhabu yake ni kulipa faini ya Tshs 1,000/= wakirudia watatakiwa kila siku kosa linaendelea walipe faini ya Tshs 5,000/= ambayo nina uhakika Barrick hawana bifu na hilo. Kifungu cha 324 & 327 vya CAP 212 vya sheria ya makampuni ndivyo vinavyotamka

Kichekesho ni kuitofautisha African Barrick Gold na Acacia hivyo kuja na khoja za kijiweni eti ni kampuni mbili tofauti.

Mwanzisha khoja ni kampuni mbili tofauti ndiye mwenye jukumu la kutoa nyaraka za lini, wapi na kwa kiasi gani Acacia iliinunua African Barrick Gold.

Someni sheria ya kuanzisha makampuni nchini Cap 212.
Tatizo la kudadia sheria bila kuelewa sheria ya makampuni ya cap 212 ilishafutwa bali kuna sheria namba 12 ya makampuni 2002 ambayo inakanuni mpya nso maana hata ada za usajiri zilishabasirika hata taratibu zake bia nazo ni tofauti,tafadhali jielimishe kusoma sheria zinazotumika
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom