Kosa kuu la tatu la UKAWA

Avatar uliyoweka na kitu ulichoandika kina-tudhalilisha sisi academician. Please try to change it or change your mindset.
 
Kosa kubwa zaidi la ukawa ni kumsimamisha Lowasa kuwa mgombea wao.

Haya mengine ni mazalia tu.!
 

MBOWE anahaha kuibrand tena CHADEMA baada ya kulamba 5B , kwa mgongo wa mabadiliko.
 
Siku zote ukiwa na kiongozi anayetazama mwisho mahali aliposimama ndiyo madhara yake maana kama mbowe ndiyo kila kitu ukawa mtapotezwa sana.

mimi sijui hata MBOWE amewapa nin sijui ndo mambo ya kungarisha nyota kwa mtakatifu TB JESHUA, maana kila wanaloambiwa na MBOWE wao wanafuata nyuma kama BEBERU , na zitto naye pamoja na kutukanwa sana baye ameanza kuwafuata , hii sio bure MBOWE amewapa kitu hawa akina ester , bulaya
 
Sasa Mkuu hoja watazitolea wapi ati wakati wanajibu hoja kanuni ovu zinainuka wanakalishwa chini au hata kusimamishwa kuhudhuria bunge kwa hili la kujibu hoja kwa hoja umechemka mjumbe toa njia nyingine mbadala zaidi ya hii kwani nguvu zao kwa number ni chache sana.
 
Kile CCM kimewapa mpaka sasa kufikia hatua ya kukata viuno kwa ile kusoma namba ambapo imewageukia na mnaisoma kisawa sawa hadi sasa mnatumbuliwa majipu ndio hicho wao wamepewa na kinawapeleka pazuri nanyi mnaona ndio maana mnapiga kelele humu.
 
lowasa aamshe nn mkuu....acha utani kwenye kampeni bila sumae kumuongelea sijui angefanyaje...dk 5 tu ndio lowasa alikuwa anaongea...that was a technical mistake to mr mboe though he is powerless to admit the failure...
 
mkuu usishangilie haya siyo maamuzi ya kushangilia kwani ukishangilia mpasuko ktkt jamii inaonekana buitakii mema nchi hii.

kumbuka wapinzani wana kura milioni sita
na bado zinaweza kuongezeka sidhani kama ni watanzania wangapi wenye furaha ya bunge lao kuonyeshwa likiwa limehaririwa tena usiku waanane.
 
Lini umesikia jambo upinzani wameshikilia tena kwa hoja yenye mashiko ikapita kwa kula za ndio naona kabs ujumbe wako we sio mpinzani kabs
 
Mbowe is a disgrace to the opposition. Hivi huyu jamaa ana mandate ya kuwa mwenyekiti wa CDM kwa miaka mingapi? He's got to step down now!!
Kwa uliyoyaandika hapa inaelekea unaikubali role ya upinzani katika mfumo uongozi isipokuwa unaona tatizo ni Mbowe.Kama ndivyo ni kwa nini wewe usichukue jukumu hilo la kuupeleka upinzani kunakostahili? Hebu tuambie ni nani kati yako wewe mwenye Brain Map murua usiyechukua hatua yoyote na Mbowe mwenye Spoiled Brain Map anayechukua hatua ni nani nafuu?
 
Mleta mada ni limbukeni haswa wa mambo yote. Moja hajijui katika maana hii: mwanadamu yeyote yule ni tokeo la historia, na kama anabahatika kuwepo, lazima atafute maana ya maisha yake. Kutoshiriki ukawa kwa hujuma za CCM siyo kushindwa kwa UKAWA, bali ni hatua nyingine mpya ya kuijenga fikra hai kwa kuhainisha "uovu" wa utawala dhalimu. Pili, mwanadamu ni tunda na sehemu ya jamii husika. Hivyo, misuguano ya sasa siyo ukwepaji wa muda na wakati wafikiriao funyu kama mleta mada. Watu hujifunza kutokana na wakati, na wakati ule huwa historia na somo la kwenda kule wasipokujua. Hivyo, UKAWA hawajapoteza chochote, bali wanaujenga utashi sahihi wa umma wa Watanzania kumjua mchawi wao halisi. Historia ni mwalimu mzuri sana. Ndiyo maana wenzetu waliopitia mitikiso hii husema, " usipofanya utafiti, na usipokuwa na tafiti, huna mamlaka yoyote ya kuongea. Mleta mada usifikiri Watanzania wa leo ni limbukeni kama ulivyo.
 
Najaribu kuangalia namna nzuri ya kuionyesha dunia kama Tanzania hakuna haki tena kuwaonyesha kwa amani kama tunadhurumiwa ni kufanya hayo ambayo wewe umeyaita MAKOSA NA KUYAPA NAMBA tofauti na hapo tunaweza kuionyesha dunia kama tunadhurumiwa kwa VITA ambayo sio nzuri sana(tunaweza kuandamana,kugoma/kususia au kupigana vita ili kudai haki itendeke sasa wewe unaona njia ipi inafaa?)
 
Je, lowasa anahukumu gani kwa kosa gani kama siyo shutuma za mitaani? Kama kulikuwa na kosa kwa nini kwa miaka 8 aliendelea kuwa huru kwa serikali makini ya CCM? Je, yaliyotokea Zanzibar katika uchaguzi yana akisi utawala wa haki katika demokrasia ya usawa na haki? Je, yanayotokea Bungeni yanaakisi haki na ukweli? Je, huyu Spika na Naibu Spika wapo hapo kweli kwa maslahi na hitaji la Taifa hili leo na sasa, au wapo hapo kwa maslahi ya chama? Ni nani basi aliyewapendekeza? Je, ni wewe kama mwananchi au chama na maslahi yake? Ifike mahali tuache ulimbukeni!!!!!
 
Duhhhhhh,hujitambui!!!!
 
uchaguzi uliopita ulinigumbua macho juu ya siasa za Tanzania! Ya sasa hayanishangazi sana!!
 
Muheshimiwa Mbowe ameyashika magamba pabaya...yamebakia kulalamika tuu...Mbowe ni msumari wa moto sana kwenye makalio ya magamba safi sana.
 
Huwa sielewi Mbowe kawapa nini, anacheza na akili za watu wazima tena wengine wasomi kwa namna anavyotaka.

Watanzania tubadilike, kuwa mpinzani au CHADEMA siyo kushabikia hadi mambo ya kijinga yasiyo na faida kwa Chama wala Taifa.
 
Huwa sielewi Mbowe kawapa nini, anacheza na akili za watu wazima tena wengine wasomi kwa namna anavyotaka.

Watanzania tubadilike, kuwa mpinzani au Chadema siyo kushabikia hadi mambo ya kijinga yasiyo na faida kwa Chama wala Taifa.
Hivi anaechezea akili za watu ni Mbowe au ni CCM? Kuna wabunge wangapi wa CCM na Magu akawaona wote hawafai akawachagulia Tulia, halafu wanasema eti bunge ni muhimili unaojitegemea! Kweli? Magu si ndio analiendesha bunge? au unabisha hilo? Mwingine anayecheza na akili za wabunge wa ccm ni Chenge! Hivi jiulize Nape na Kinana chini ya JK si walituhubiria habari za magamba? Na wakataja mapacha watatu? Chenge akiwa mmoja wapo na Lowasa? Chenge sasa ni nani Bungeni? Au wabunge wa CCM sio wasomi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…