Muongozo wa maadili wa CCM (mwaka 2002) unasema hivi:
kwa maneno mengine Ibara ya 15:1 inaendelea kusimama.
Mambo ndiyo hayo!
Huu ni uthibitisho wa umimi wa Chama cha Mapinduzi dhidi umma wa waTanzania. Mimi nilitegemea kosa kubwa kwa Chama ni kutotekeleza sera na kanuni zake.
Issue ya kushindwa katika uchaguzi has nothing to do with personalities but strategies. Huu pia ni muendelezo wa umimi kuwa Chama Chaq Mapinduzi kikisimama katika uchaguzi wowote ni lazima kishinde, kama ikitokea kikashindwa, kwa mujibu wa CCM, kuna usaliti na kuna mtu amefanya kishindwe. Hapa lazima wamtafute mchawi. Hii inaqmaana mchawi wa kipigo cha Tarime anatafutwa. Najua kwa Mbeya -Vijijini, CCM ni ushindi wa
mteremko kama kumsukuma mlevi.
Hata hoja kukichafua chama na kukifanye kinuke mbele ya umma ni ule ule umimi kuwa CCM ni Chama kitakatifu, kitukufu, hakiwezi kuchafuka, labda kichafuliwe. Na kikinuka mbele ya umma kinaamini kuna mtu amekipaka **** ndio maana kinanuka. Hivi kinanyoachia rushwa itawale mpaka chaguzi zake za ndani mfano UWT juzi juzi, Mama Kahama kalia, ushahidi kapeleka kwa Mwenyekiti, alipuuzwa na kuonekana msaliti- anaipaka CCM **** ya harufu ya rushwa hivyo Mwenyekiti akaona bora bora ampigie debe aliyeshinda. CCM ni Chafu, Imeoza kwa Rushwa na Inanuka!. Ila wanaCCM na viongozi wake mpaka Mwenyekiti, hawaisikii hiyo harufu ya uozo wa rushwa kwa sababu pua zao zimeshazoea na kuiona ni harufu ya kawaida kama unapoingia soko la samaki Feri unapokelewa na harufu ila baada ya muda mfupi, pua zinazoea na kuiona ni harufu ya kawaida.
Umimi wa CCM unatokana na kuweweseka na ndoto za enzi za Chama Dola na utaendelea mpaka kutakapokuja kujichomoza chama mbadala.
Mimi ni mmoja wa wengi ambao tumeipigia kura CCM na tutaendelea kuipigia na CCM itaendelea kutawala, sio kwa sababu tunaipenda, tunaipigia kura CCM kwa sababu hatujaona any serious mbadala.
Baada ya Chadema kuonyesha imeweza Tarime, tunaiangalia kwa makini jee kitaifa Chadema inaweza?.
Kwa Chadema ilivyo sasa, bila kuungana na wapinzani wengine, Chademe peke yake haiwezi. Kwa mwendo wa wapinzani ulivyo sasa, hakuna serious commitment kuungana, hivyo came 2010, pamoja na kuoza kote, na kunuka kote mbele ya umma, CCM itapeta tena kama kawaida huku ikijiamini ni kutokana na usafi wake!.
Najua ni ngumu kidogo kwa mimi kueleweka, lakini nawakilisha tabaka la waTanzania walio wengi wanaipigia kura CCM kwa sababu hawana jinsi.