Kosa kubwa la Gwajima ni lipi?

Kosa kubwa la Gwajima ni lipi?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,882
Reaction score
828,449
Wakati alipokuwa na kashfa ya ngono kipindi kile.. ccm walisimama naye kumtetea mpaka wakapovuka... Yalitokea mazonge yake mengi tu lakini walifunika kombe mwana haramu akapita...

Nyakati zikapita.. Watu wameumbiwa kusahau maisha yakasonga.. Yalaendelea kuwatokea Watanganyika mengi mabovu ya kuumiza sana! Hakuna hata mwana ccm mmoja aliyesimama kidete na kwa uwazi kuyakemea..

Hatimaye hali ilipozidi kuwa mbaya sana, pamoja na sababu zingine za kisiasa Gwajima akaibuka tena! Lakini this time akiwa kavaa koti la uzalendo.. Akakosoa na kushauri kama mwananchi Mtanganyika huru..

Hakuongea cha ajabu kwakuwa yote yalikuwa marudio tu yaliyosemwa sana na wapimzani na yakawaletea matatizo makubwa sana.. Kaongea sauti ya wananchi.. Kapoza kiu ya wengi waliotamani kusikia aliyoyasema kutoka nje ya upinzani na ndani ya ccm

Hajakashifu mtu, hajatukana mtu kaongea fact tupu. Na akatoa sababu za wazi kwanini hakuyaongea bungeni.. Na kwanini hakuyaongea kwenye vikao vya chama na kwanini hakuongea binafsi na mkuu wa nchi
Aliweza kuweka uwiano sawia kwenye mazungumzo yake na waandishi wa habari
Sasa kituko kiko hapa.. Wamejitokeza makada wenzake kumjibu.. Si kwa hoja bali kwa mipasho, kejeli na vitisho... Mpaka mtu unajiuliza kwani hawakumsikiliza vema? Hawakumuelewa?

Kumbe ndani ya ccm ukitenda uovu ni rahisi kutetewa kuliko ukiamua kusimama na watanganyika na kuwatetea ama ukisimama na kutoa ushauri kwa maslahi mapana ya Tanganyika?
Mpaka sasa waliomjibu kwa vioja, kejeli na vitisho ni hawa
Mwijaku chawa
Jerry Muro kada mhamiaji
Msukuma MB
Abas Tarimba MB

Gwajima amesema hatakaa kimya hiyo naye kawajibu kwamba yeye ana leseni kubwa.. Hawezi kuwajibu wenye leseni ya bajaj
Je ccm kosa la Gwajima ni lipi?

View: https://vm.tiktok.com/ZMSjPMQh2/
 
Kosa lake ni kusaliti kamb ya kumfagilia rais kinafiki na kuamua kuwa mkweli
Kama yeye anaweza kufanyiwa hivi vp kuhusu wapinzani
IMG-20250527-WA0002.jpg
 
Hivi umegunda jana usiku JF kulikuwa na genge pamoja na mods kufuta kila mada au kubadilisha mada.chunguzeni mada zenu na kama kuna mada zilionekana kuhusu CCm zote zimefutwa
Lakini JF haikuwa sehemu ya kalamu ya mama.🥺🤔
IMG-20250526-WA0023.jpg
 
Hivi umegunda jana usiku JF kulikuwa na genge pamoja na mods kufuta kila mada au kubadilisha mada.chunguzeni mada zenu na kama kuna mada zilionekana kuhusu CCm zote zimefutwa
Kama ni kweli uko wapi ule uhuru wa vyombo vya habari?

Kumpinga Gwajima ni sawa na kukataa uhai, hoja zake zipo wazi sana na zinaeleweka hadi na mtoto wa darasa la pili. Sijui hali ya kujitoa ufahamu kwa baadhi ya watu kisa siasa itaendelea hadi lini. Tunajidanganya.
 
Wamefuta kila uzi kuhusu CCm mabaya yao.chunguzeni mada zenu kama utaona kuhusu CCM na mada mbaya
Ohhh🥺🥺🥺🥺🥺😭😭😭😭
 
Wakati alipokuwa na kashfa ya ngono kipindi kile.. ccm walisimama naye kumtetea mpaka wakapovuka... Yalitokea mazonge yake mengi tu lakini walifunika kombe mwana haramu akapita...

Nyakati zikapita.. Watu wameumbiwa kusahau maisha yakasonga.. Yalaendelea kuwatokea Watanganyika mengi mabovu ya kuumiza sana! Hakuna hata mwana ccm mmoja aliyesimama kidete na kwa uwazi kuyakemea..

Hatimaye hali ilipozidi kuwa mbaya sana, pamoja na sababu zingine za kisiasa Gwajima akaibuka tena! Lakini this time akiwa kavaa koti la uzalendo.. Akakosoa na kushauri kama mwananchi Mtanganyika huru..

Hakuongea cha ajabu kwakuwa yote yalikuwa marudio tu yaliyosemwa sana na wapimzani na yakawaletea matatizo makubwa sana.. Kaongea sauti ya wananchi.. Kapoza kiu ya wengi waliotamani kusikia aliyoyasema kutoka nje ya upinzani na ndani ya ccm

Hajakashifu mtu, hajatukana mtu kaongea fact tupu. Na akatoa sababu za wazi kwanini hakuyaongea bungeni.. Na kwanini hakuyaongea kwenye vikao vya chama na kwanini hakuongea binafsi na mkuu wa nchi
Aliweza kuweka uwiano sawia kwenye mazungumzo yake na waandishi wa habari
Sasa kituko kiko hapa.. Wamejitokeza makada wenzake kumjibu.. Si kwa hoja bali kwa mipasho, kejeli na vitisho... Mpaka mtu unajiuliza kwani hawakumsikiliza vema? Hawakumuelewa?

Kumbe ndani ya ccm ukitenda uovu ni rahisi kutetewa kuliko ukiamua kusimama na watanganyika na kuwatetea ama ukisimama na kutoa ushauri kwa maslahi mapana ya Tanganyika?
Mpaka sasa waliomjibu kwa vioja, kejeli na vitisho ni hawa
Mwijaku chawa
Jerry Muro kada mhamiaji
Msukuma MB
Abas Tarimba MB

Gwajima amesema hatakaa kimya hiyo naye kawajibu kwamba yeye ana leseni kubwa.. Hawezi kuwajibu wenye leseni ya bajaj
Je ccm kosa la Gwajima ni lipi?
Kichwa kinaendeshwa na tumbo badala ya ubongo..unategemea nini hapo ?

Akina Jerry Muro wanajitokeza wazi kuelezea namna walivyokotwa kutoka Jalalani.
Kuokotwa kwake toka kwenye ukata ndio point yake anayojibia hoja za Gwajima,Very hopeless.
 
Kwa taarifa yako, nchi hii hakuna kitu kinaitwa kashfa ya ngono. Labda ubake mtoto chini ya miaka 18.
Kama kuna mwanaume wa kitanzania hana nyumba ndogo au kutembea na malaya ujue huyo ni mgonjwa au hana pesa.
 
View: https://www.facebook.com/share/p/1ApEDge5w4/?mibextid=xfxF2i
Kuna hii taasisi imemjibu😁
GWAJIMA ULIVULIWA UASKOFU TAYARI
Gwajima alikuwa Askofu mtukutu mno, anayeropoka na asiyejali nini anasema na kwa wakati gani. Askofu huyu wa zamani wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, aliwahi kuzivunja Sheria za Mungu Muumba ndani ya madhabahu yake.
Alikuwa ni msichana mrembo kutoka Dar Es Salaam, aliyekwenda kufanyiwa maombi na Askofu bandia huyu Kisha wakainajisi nyumba ya Yesu pasina kujali. Mwili mzima wa huyu Askofu ulionekana tena ni hodari katika kuwala kondoo wake wasiokuwa na hatia.
Yesu hajafundisha Kondoo waliwe maana hawana hatia, na kama huyo mdada alikuwa malaya, basi hata wewe Askofu wa Mchongo Gwajima pia ni malaya na haufai kuwa kiongozi wa nchi Wala jamii ya kitanzania.
NINACHOKIONA KWAKO BWANA GWAJIMA NI UDINI MWINGI, WEWE UNAWABAGUA VIONGOZI WASIOKUWA WA DINI YAKO.
Watanzania hatutaki utuchonganishe na Viongozi wetu maana Uaskofu wako huo ulikuvuka wakati unazini na huyo kondoo wako wa Mchongo.
Watanzania tunawapenda Viongozi wetu wote pasina kujali dini, rangi Wala kabila ya mtu. Naona Uchungaji umekushinda sasa ni lazima uchungwe..na wewe kama kondoo.
 
Hivi umegunda jana usiku JF kulikuwa na genge pamoja na mods kufuta kila mada au kubadilisha mada.chunguzeni mada zenu na kama kuna mada zilionekana kuhusu CCm zote zimefutwa
Kama Jf nao wamekuwa ni machawa, ku log off kunanihusu.
 
Gwajima kama Simba SC tu, barua moja tu hatuchezi wengine mpaka leo bado wanaitisha press 😄😄
 
Hivi CCM ni wachawi au ni mashetani?
Yaani mtu anaongelea watu kutekwa anasema Gwajima anatoa mifano ya kutosha?
Kwahiyo yeye Mdude hana wazazi?
Au yeye wazazi wake hawakumzaa na kumlea

CCM ni mitaahira.
Wengine hawa hapa
IMG-20250527-WA0010.jpg
 
Na umri wangu huu sijawahi kusikia kauli za kikatili kama alizotoa huyu mwanamke. Mdomo wake unatema cheche za moto. Kwa maadili na imani yangu hata adui yako huwezi kumtamkia vile hadharani. Tena hakuna hadhara kubwa kama bungeni. Nilipokuwa namsikiliza moyo wangu ulikuwa ukitetemeka. Namsikitikia sana. Kimya cha bunge kwa kauli kama hizi kinatia mashaka makubwa. Hakika huyu aombe rehema kwa Mungu.

Lakini pia kauli zake zimenifikirisha sana juu ya uelewa na mtazamo wa jamii juu ya ukatili wa kijinsia. Tulizoea kufikiri kwamba wakatili ni wanaume kwa wanawake. Huyu leo katudhihirishia kwamba ukatili uko pande zote. Nadhani kwa wacha Mungu wakati umefika wa kuomba na kutoa sauti ya unabii zaidi juu ya taifa letu. Wanaweza kututeka na kutuua lakini kabla hawajatumaliza Bwana atawajilia wao.
FB_IMG_1748355324755.jpg
 
Back
Top Bottom