Korti yaamuru Nabii Mwingira akamatwe

kuchagua wa kumtii ni jambo la muhimu kwa mtu anayejitambua na kuwa na akili timamu, huwezi ukawa unatii kila kitu, we labda uwe mlevi anayeamua kutukana kila mtu au kusalimia kila mtu, iweje ufundishwe namna ya kuutumia utii? usipochagua pa kupeleka utii wako, utawatii hata wachawi, walawiti, wafiraji, na waongo, harafu unategemea nini ukiwatii watu hao? Mahama za Tanzania nyingi zimekuwa hazitendi haki, kama hazitendi haki maana yake zinaongozwa kishetani, Kwa sababu Mungu ni wa haki hivyo hazikutoka kwake, kwa hiyo kuzipuuza ni kumpuza shetani nba mahakama zake

Argument zako zinakinzana sana ndugu yangu.......

Mtumishi wa Mungu amekosea kuidharau amri ya mahakama. yeye mwenyewe hajatenda haki kwa kuchukua sheria mkononi wakati kesi iko mahakamani bado. Unajua mpendwa unachukulia hili suala kiimani zaidi bila kufuata ukweli ulivyo.

Wewe kwa imani yako unaonekana huamini kama "MTUME NA NABII" kama anavyojiita hawezi kukosea,yuko right all the time. Mahakama ina nguvu zake bwana,serikali imepewa pia mamlaka na Mungu.
 
Argument zako zinakinzana sana ndugu yangu.......

Mtumishi wa Mungu amekosea kuidharau amri ya mahakama. yeye mwenyewe hajatenda haki kwa kuchukua sheria mkononi wakati kesi iko mahakamani bado. Unajua mpendwa unachukulia hili suala kiimani zaidi bila kufuata ukweli ulivyo.

Wewe kwa imani yako unaonekana huamini kama "MTUME NA NABII" kama anavyojiita hawezi kukosea,yuko right all the time. Mahakama ina nguvu zake bwana,serikali imepewa pia mamlaka na Mungu.
pengine wewe umeanza leo kutuma post juu ya swala hili, binafsi sijatetea kwa kile alichokifanya, kwanza uelewe hilo, as a human being he have the so called weckness sasa ninachojaribu mimi kukitetea ni kwale wanaojaribu kuihusisha Biblia na udhaifu wa mtu, nje ya utumishi Mwingira ni mtu wa kawaida tu awezaye kukosea kama mtu mwingine, tatizo nililoliona tangu Thread hii imetumwa wapo walioweza kuona kama kwamba kwa kufanya hivyo Mwingira basi kaagizwa na maandiko sijui kama hupo hapo ....
 
thibitisha hilo la uhalali....

Mahakama ilitoa amri kuwa kitu chochote kisiendelee mpaka uamuzi utakapotoka. Uamuzi ungeweza kuwa positive kwa Mwingira kama kweli ana haki na hilo eneo. Haki inaweza ikawa yako lakini kwa papara na kutotulia unaikosa (Kumbuka suala la Esau na Yakobo wana wa Isaka).

Mahakama ina haki kisheria kuzuia ujenzi au shughuli fulani kuendelea mpaka itakapotoa maamuzi. Mimi kama mtanzania na mkristo naamini natakiwa kutii sheria za Tanzania na amri halali za mahakama. Kuna amri ambazo si halali,naweza kuzipinga kupitia mahakama za juu zaidi lakini si kukaidi. Unaweza usitii ila pia usikaidi. Tatizo la Mwingira amekaidi amri.

Kusema "Mahakama zinaendeshwa kishetani" hiyo ni kufuru kabisa. Haki ina mkondo wake na unatakiwa uufuate mkondo ili uipate. Mfano binadamu Mungu katuumba tufanikiwe,lakini bila kufuata mkondo wa mafanikio,hayawezikukufuata ukiwa umelala. Kufanikiwa ni haki yetu, lakini kwanini tunafanyia kazi mafanikio yetu? Unahukumu mahakama (sehemu ya serikali) za kitanzania kuwa zinaendeshwa kishetani huku ukisahau kuwa serikali hiyo hiyo ndiyo imetoa uhuru wa kuabudu (ambao wafanyabiashara wa neno la Mungu wanautumia vibaya).

Mtumishi wan Mungu anatakiwa kufuata sheria za nchi. Waumini mnamezeshwa sumu kiasi kwamba hamuoni kabisa. Mnafumbia macho hata maovu ya wazi kabisa. Historia inaonyesha kuwa waumini wa namna hii hata makanisani kwao huwa hawasomewi hata hesabu za mwaka na wala hawahoji.

Mtumishi wa Mungu hayuko juu ya sheria. Sheria imewekwa na Mungu kwani Mungu ndiye anayeipa nguvu dola (Kumbuka wana wa Israel walimuomba Mungu awape mfalme).
 
sasa tupeni update Je Nabii Mwingira amekamatwa Tayari?
MIMI namuamini sana Mwingira mapambano yakudai haki, huyu si kama Wale Waanglicana wa Ilala walioporwa ardhi yao na mwarabu wa mafuta pale buguruni.
 
Hey,ndugu yangu mbona unanitusi bure?unajua maana ya unafiki?mimi nilichosema ni kwamba kama kiongozi wa dini anatakiwa kuwa mfano..Kuupuza mahakama sio mafano mzuri hata kama angekuwa na sababu za muhimu.Biblia iansema tuheshimu mamlaka zilizowekwa....acha hasira ndugu yangu,jenga hoja.Pole kama nimekuudhi sio lemgo langu..

Na je mahakama ikikuamuru uvue nguo na utembee uchi barabarani utaitii...?
cha msingi hapa ni madai ya mwingira, je aliuziwa kweli? na kama ni kweli kwa nini soza plastic wameweka pingamizi.
 
Hata biblia inasema "Tiini mamlaka zilizoko ulimwenguni" hapa huyu mfanyabiashara wa neno la Mungu hajatii anayofundisha.

Nimeipenda sana hii'MFANYA BIASHARA WA NENO A MUNGU'
 
ladies and gentlement, what is called utii in the bible is subject to some conditions. Watu hawalazimika kutii amri hata zile zisizolingano na vigezo vya Mungu.
 
sasa tupeni update Je Nabii Mwingira amekamatwa Tayari?
MIMI namuamini sana Mwingira mapambano yakudai haki, huyu si kama Wale Waanglicana wa Ilala walioporwa ardhi yao na mwarabu wa mafuta pale buguruni.
kwishnei!!!!
 
Mwingira asiogope kukamatwa hata Mtume Paul alikamatwa na kuswekwa lupango mara nyingi tu. Vile vile Nabii Jeremiah alikamatwa mpaka akatupwa kwenye kisima na kuokolewa na Mu-Ethiopia.
 
Mahakama ilitoa amri kuwa kitu chochote kisiendelee mpaka uamuzi utakapotoka. Uamuzi ungeweza kuwa positive kwa Mwingira kama kweli ana haki na hilo eneo. Haki inaweza ikawa yako lakini kwa papara na kutotulia unaikosa (Kumbuka suala la Esau na Yakobo wana wa Isaka).

Mungu ndiye anayeipa nguvu dola (Kumbuka wana wa Israel walimuomba Mungu awape mfalme).

Hii Mahakama ilikuwa wapi muda wote kumkamata mpaka inamkamata leo hii? kwa sababu yale majengo amejenga toka muda mrefu kwa nini wasimzuie mapema?
 
mahakama inajishushia hadhi yenyewe, ikipuuzwa na serikali inilmaba miguu, watu binafsi ndio nasikia amri ya kukamatwa inatolewa. kama inataka kuheshimiwa ithibitishe kwanza kwa matendo yake, itoe haki kwa watu masikini, sio ikubali kutumiwa kuwatupa magerezani............
Kwa hiyo unamaanisha kila mtu afanye anavyoona sawa?????? [Anarchy]
Nilikuwa natarajia majibu/mchango wenye logic ili sisi hohehahe wa ujuzi wa mambo tujifunze.
 
kweli hii nchi ni ngumu sana kuoikomboa.Watu wamejaa ushabiki zaidi kuliko ukweli...Tunaposema kutii mamalaka hatusemi kila unaloambiwa hata kama ni kutembea uchi kama mmjoa wetu humu alivyodai..Na hakuna mamlaka itakayo kutaka uvue nguzo labda ya kutoka kwa Jezebeli..Ukweli ni huu Mwingira amekosea,amefanya dhambi na anapaswa kukuri kwamba amekosea.hebu tufunguke macho jamani..
 
Mada nyingi zenye kuhusisha imani zetu moja kwa moja au kwa kupitia zinasumbua sana kupata jibu, wengi hujadili kishabiki zaidi na wanauacha ukweli mbali.

Ukweli lazima usemwe,mtumishi kama kweli kafanya hivyo kakosea kwa sababu ni dola hiyo hiyo aliyoidharau ambayo imempa usajiri,imempa leseni ya benki na ndio iliyompa hati za viwanja na mashamba.

Tukikosea tukubali na kutubu. period.
 
Hivi ili sndilo lile Kanisa la Mashoga au nijingine? na sindiye yule mchungaji millionair anaewavuna kondoo wake ambae pia ni shoga?
 
That's the funny thing about Tanzania. watu wamevamia open space wanaanza biashara alafu wakitakiwa kuondoka kupisha maendeleo eti wanauliza waende wapi? Na serikali inasuasua cha kuwajibu... Halaaa! Si mrudi mlikokuwa kabla hamjavamia... Mimi huudhika kweli watu wanavyoifanya serikali kama shangazi yao , na serikali kuwadekeza kama wajukuu wao..... au kwa vile uchaguzi unakaribia nini?
 
Hivi ili sndilo lile Kanisa la Mashoga au nijingine? na sindiye yule mchungaji millionair anaewavuna kondoo wake ambae pia ni shoga?
I doubt if he is the one. May God have mercy on you for posting something you are not even sure of
 
Back
Top Bottom