Korosho: Viongozi vyama vya ushirika wanapigwa ili wataje kangomba

NAMTUMBA

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,939
594
Hali ni mbaya. Wakati Malipo ya korosho hakuna kinachoeleweka mpaka sasa viongozi wa vyama vya ushirika wanapigwa ili wataje majina ya Kangomba. Wanakamatwa, wanafungwa kisha wanapigwa na wanapewa vikaratasi ili kila kiongozi analazimishwa aandike majina matano au zaidi ya kangomba.kwasasa sio ukaguzi tena, wanaandikisha majina kwablazima. Hatakama viongozi hawajui majina kinafuata ni kipigo kikali, wanarushwa kichurachura, wanafagia boma lote, wanatishwa, na mateso ya kila namna hadi kila mmoja aandike majina matano ndo wanaachwa. Lengo lao kupunguza idadi ya wakulima ili walipwe watu wachache.

Chomachoma in nani?
Hapa kuna makundi kama manne hivi.
1. Kundi la kwanza la chomachoma ni wajasiriamali ambao wanakopesha pembejeo wakulima. Pembejeo kama vile madawa, vifaa vya kupuliza madawa, na pesa tasilimu kwa ajili ya mkulima kuhudumia shamba kwa palizi na mambo mengine kwa makubaliano ya kulipwa kipindi ambapo korosho itakuwa zimezaa. Mikopo hii wanakopeshwa mienzi kama nane kabla ya msimu wa mavuno kwakuwa wanakopeshana mwezi wa march na April, hivyo pesa ya huyu mjasiriamali ambae anaitwa kangomba pesa yake inakaa kwa mkulima kwamiezi nane au zaidi. Ni aina ya mkopo ambao hata benki hawawezi kukopesha mkulima. Lakini chomachoma yeye ana take risk pesa yake inakaa kwa mkulima kwa miezi nane, lakini pia kipindi hiki chote chomachoma anakuwa anapeleka marejesho benki kwa kutumia vyanzo vingine vya mapato ukizingatia chomachoma wengi ni wale wenye maduka na biashara zingine hivyo wanakuwa na sifa za kukopesheka benki tofauti na mkulima ambae hana sifa za kukopa benki hivyo kimbilio pekee la mkulima ni kwenda dukani kwa chomachoma kukopa pembejeo au pesa. Kumwambia chomachoma anadhulumu wakulima sio kweli huu ni onevu wa wazi. Ukimwondoa chomachoma kwenye mfumo huu ni kuumiza wakulima labda Kabla serikali haijamuondoa chomachoma lazima wakubali kukopesha wakulima kwa mfumo uleule wa chomachoma ambapo repayment inaanza miezi nane hadi kumi tangu siku ya kukopeshana. Na hili swala la kwamba mkulima anapewa riba kubwa ni hivi; Chomachoma anakopa benki kwa riba, nae ana kopesha mkulima kwa riba, hivyo ni automatically mkulima atalipa riba ambayo ni double. Chomachoma hawezi kukopa benki alafu yeye amkopeshe mkulima bila riba na ukizingatia repayment muda mrefu, ni haiwezekani. Serikali ikitaka kumuokoa mkulima kutokana na hiki kitanzi cha chomachoma lazima ikubali kuanzisha mfuko au benki maalumu kukokopesha wakulima at high risk kama chomachoma anavyokopesha.

2. Kundi la pili ni wajasiriamali ambao wanakopesha wakulima pesa tasilimu kwa kulipwa pesa kwa pesa au pesa kwa korosho. Hawa ndo wale wanatajwa kwamba wanakula maua. Lakini chanzo kikubwa cha mfumo huu ni bei kubwa ya pembejeo za kulimia korosho hivyo mkulima anashindwa kumudu garama na kuamua kutafuta vyanzo vya pesa za ziada zitakazomwenzesha kuhudumia shamba. Msimu wa mavuno ukifika mkulima anachukua kiasi kidogo cha korosho kulipa deni au kwa wale waliokubaliana kulipwa pesa kwa pesa hulipwa pesa kwa kadiri mikataba walivyokubaliana.

3. Kundi la tatu hawa wananunua korosho kabisa. Ingawa wanazunguka na mizani mashambani kununua korosho lakini maranyingi wakulima wenyewe ndo wanaenda na korosho zao kuziuza kwa chomachoma ili wapate pesa ya kujikimu. Na wanauza kiasi kidogo sana. Mfano kwa mkulima mwenye gunia hamsini za korosho anaweza kuuza kilo 50 hadi 100 kwa lengo la kutatua shida ndogondogo za nyumbani lakini mzigo mkubwa anapeleka galani kuikopesha serikali. Sio kweli kwamba mkulima anauza korosho zote kwa chomachoma, na sio kweli kwamba mkulima chomachoma wanadhulumu wakulima. Wakulima wanajitambua. Chomachoma wanatumia fursa hii kwakuwa serikali inachelewa kuwalipa wakulima hivyo kama ilivyo kwa wajasiriamali wa bidhaa zingine kama vile nyanya, vitunguu, mahindi nk. pia hawa wakorosho mfumo ni uleule wa bidhaa nyingine.

4. Kundi la nne hawa wanapewa mashamba na wakulima wenyewe iwapo mkulima ameshindwa kuhudumia hivyo kwa kuhofia shamba kuungua moto au mikorosho kwakukosa huduma anaamua kukodisha kwa mjasiriamali ambae anauwezo wakuhudumia shamba. Wanaweka makubaliano fulani au mikataba. Lakini kuna mashamba ambayo wakulima wametelekeza hivyo baadhi wanaomba kuhudumia kutoka kwa ndugu wa karibu au kutoka kwa mkulima mwenywewe lakini wengi wao ni wale wakulima waliofariki au wamehama kijiji.

sikiliza audio hapo chini.
 

Attachments

  • Record20190106075556.aac
    7.5 MB · Views: 18
  • Record20190106080556.aac
    7.7 MB · Views: 15
Mwamwindi alimpelekea Moto RC Dr Kleruu kwa ujinga ujinga Kama huo

Alipofikishwa Mahakamani Mara zote alikiri Na mpaka anatembelewa Na Mtoto wake hakuonekana kujutia kile Kitendo
 
Hahaha..eti alimpelekea moto..
Alafu kumbuka Kleruu hakumpiga ila tu alikuwa 'anamtomasa tomasa' na kifimbo,, je angempiga.?
Mwamwindi alimpelekea Moto RC Dr Kleruu kwa ujinga ujinga Kama huo

Alipofikishwa Mahakamani Mara zote alikiri Na mpaka anatembelewa Na Mtoto wake hakuonekana kujutia kile Kitendo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri mkuu,Nape Nauye, Hawa ghasia,Salma kikwete na mzee Mkapa,pamoja na wabunge wenu mko wapi? Aliposema nitawavunja viuno shangazi zenu ataanzia jimbo la waziri mkuu je yameanza kutimia? IVI WATANI ZANGU,MMEKAA NA KUJIULIZA,KWANINI WAMAKONDE TU!? Au ndiyo vita yenyewe ya kiuchumi imegeukia kwenu? Maana lilipokuja suala la gas kusafirishiwa Dar, mkagoma mkitaka maendeleo ya Mtwara kwanza, MKASEMA HAITOKI. Kikwete akawaletea Polisi,waliposhindwa akawaletea jw. Mlilala saa12 jioni bila kupenda,na sijui kama ndoa ilipata nafasi. Korosho zenu, mkazurumiwa 200+billions. Leo yanapotokea haya je mwajiuliza kwa nini wa machinga tu!? Kabla ya korosho, yalikuwepo mazao ya biashara mfano, kahawa kwa wachaga,wahaya na wamatengo mbinga. Chai huko rungwe na mfindi. Tumbaku huko tabora,singida na songea. MADALALI WALIKUWEPO, walinunua kwa wakulima wakauza ktk vyama, je mmejiuliza kwanini hayakutokea haya,na kwanini korosho tu! Kule ziwa victory walikuwepo wauzaji Samaki viwandani, wavuvi wakitoka na Samaki wanauzia wanaokwenda uza viwandani. KWANINI LEO KANGOMBA? VITA VYA KIUCHUMI! NILIOWATAJA HAPO JUU, NABII MUSA ALILELEWA KTK NYUMBA LA FARAO,LAKINI ALIPOONA NDUGUZE ISRAE WAKITESEKA THAMANI YEYE KUENDELEA KULA RAHA KWENYE KASRI LA KIFALME HAKUINA, ALIONA HERI KUPATA SHIDA PAMOJA NA NDUGUZE. JE NINYI???????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
It's obvious that hawana pesa na hawakujiandaa kuwapora wafanyabiashara deal Hilo la Korosho...wanachokifanya Sasa NI kuwadhulumu tuu wakulima...aliambiwa jiwe lakin na wabunge wa KUSINI akawaletea kiburi...anavuna Sasa jeuri yake
 
Wewe ni wakala wa kangomba. Jasho litakutoka mwaka huu.
Nchi ina mambo ya kis. Nge hii,, kwan hao kangomba si watanzania wenzetu,na wananunua kihalali toka kwa wakulima,, AU kuna mkulima amelalamika kuwa ameibiwa,, yaani Magufuri hataki wananchi Wake wanunue mazao ya wakulima na wao wakauze wapate faida mbili tatu za kula na familia Zao...sijui anataka watu wafanye shuhuri gani huyu Baba,, sasa unataifisha mali ya mtu ambayo ni halali sio bange wala drugs, wala bunduki, miaka yote hao kangomba wananunua korosho na wala kulikuwa hamna malalamiko yoyote toka popote,

AU mwaka juzi wakulimA walivyouza korosho had kilo moja Kwa tsh 4000/= kangomba hawakuwepo??


Yaani Kama M/mungu hajamuadhibu huyu Baba hadi kwisha awamu yake au mwisho wa mwaka huu juu ya dhuluma aliyoifanya na washirika Wake,, ntaamini Kweli Mungu yupo pamoja nawafanyao dhuluma,
 
Back
Top Bottom